Dorothy Gwajima, Paul Makonda na Jumaa Aweso majina yao ni miongoni mwa wanaoweza kuteuliwa kuwa Waziri Mkuu

Mkalukungone Mwamba

JF-Expert Member
Joined
Aug 29, 2022
Posts
2,435
Reaction score
5,228
Hapa bado kwa walitajwa hapa! Binafsi namtazama zaidi Dotto Biteko na bila shaka kuteuliwa kuwa Naibu Waziri Mkuu ilikuwa ni kupata uzoefu zaidi!

Ila tusubiri tuone ila kwa Makonda kazi itakuwepo, Aweso anafanya kazi nzuri ila bado kushika nyadhifa kubwa kama hii
==============
Majina ya vigogo hao watatu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) — Mhe. Paul Makonda, Mhe. Dkt. Dorothy Gwajima, na Mhe. Jumaa Aweso — yameanza kutajwa kuwa miongoni mwa wanaoweza kuteuliwa kuwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, endapo mabadiliko ya uongozi yatahitajika baada ya uchaguzi mkuu.

Wananchi na wachambuzi wa siasa wanasubiri kwa hamu kuona iwapo Rais Samia Suluhu Hassan atafanya mabadiliko yoyote katika safu ya juu ya uongozi wa serikali. Majina haya yameibuliwa kutokana na rekodi zao za kiuongozi, weledi na umaarufu ndani ya chama na serikali.

Paul Makonda
Aliwahi kuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam na baadaye Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM. Anajulikana kwa kauli thabiti, utendaji wa haraka, na uwezo mkubwa wa kushawishi makundi ya vijana.

Dkt. Dorothy Gwajima
Ni Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum. Amewahi pia kushika Wizara ya Afya. Ana rekodi nzuri ya utumishi wa umma, na ni mtaalamu wa utawala wa afya kwa zaidi ya miaka 20.

Jumaa Aweso

Ni Waziri wa Maji, anayesifika kwa usimamizi wa miradi mikubwa ya maji vijijini na mijini. Amejipatia umaarufu kutokana na ukaribu wake na wananchi na uwezo wa kusimamia utekelezaji wa sera

Je ni yupi anafaa endapo ikitokea kama inavyosemekana* ?

 
Bashite tena na Uwaziri mkuu 🤔🤔🤔
 
Watajuana wenyewe, mauaji makubwa.

Akitaka amuweke hata mumewe awe waziri mkuu for all we care.
 
Makonda akiwa waziri mkuu nahama Tanzania Mapema January mwakani..

Fikiria Samiu,jumlisha bashite awe waziri mkuu,tutakua na nini ?A clown republic???
 
Makonda akiwa waziri mkuu nahama Tanzania Mapema January mwakani..

Fikiria Samiu akili ndogo,jumlisha bashite awe waziri mkuu,tutakua na nini ?A clown republic???
We are already a clown republic.
 
Hahahaha Ila watanzania bhn sasa Dorothy Gwajima ni mbunge wa kuchaguliwa wa jimbo gani? Kiranga
 
Dorothy Gwajima hana sifa wala vigezo vya kuwa waziri Mkuu.

"Waziri Mkuu atatokana miongini mwa wabunge wa kuchaguliwa"

Dorothy Gwajima hakugombea ubunge popote
Mkuu sorry nje ya Mada,why hakugombea?alitoa statement yeyote??
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…