Donald Trump atua Iraq kutembelea wanajeshi

Donald Trump atua Iraq kutembelea wanajeshi

Bagamoyo

Platinum Member
Joined
Jan 14, 2010
Posts
32,692
Reaction score
37,575
December 26, 2018
Al Asad Air Base, Iraq

Rais Donald Trump ametembelea wanajeshi wa Marekani nchini Iraq na kuongea na wapiganaji ktk kambi kubwa ya kijeshi nchini Iraq ya Al Asad. Hii ni ziara ya kwanza ya Donald Trump kutembelea wanajeshi wa Kimarekani waliopo Iraq.

Rais Trump na mkewe walitumia masaa matatu ktk Kambi hiyo ya Al Asad iliyopo magharibi mwa Iraq kuwasalimia na kuwashukuru wapiganaji na maofisa hao wa majeshi ya Marekani kwa kujitoa kulinda maisha na mali za watu wa Marekani bila kusahau za wa-Iraq.

Rais Trump pia amebainisha kuwa nchi washirika matajiri kama Saudia n.k ktk mapambano ya kungoa magaidi eneo hilo la Mashariki ya Kati wamewaunga mkono kwa kutoa mchango mkubwa zaidi wa kifedha ktk vita hivyo.

Rais Trump amesisitiza nia na malengo ya kufanya eneo hilo kutokuwa pango la magaidi lipo palepale. Na kuzishukuru nchi washirika kwa mchango wao kutimiza juhudi hizo za kuwasaka na kuwaangamiza kabisa maadui hao. Marekani imetenga zaidi ya U$ 700bn kwa masuala ya ulinzi, Rais Trump amesema.


Source : The White House
 
Hivi nikitaja kuwa mwanajeshi wa marekani nifuate procedures gani?
 
Ila alijitoa
Watu wakajua anamalizia boxing day WHouse kumbe mnyama yuko hewani kwa siri kubwa Iraq.....
 
hii inatia moyo sana kwa kiongozi wako kukujia eneo la vita kwa ajili ya kuthamini kazi unayofanya
Ila alijitoa
Watu wakajua anamalizia boxing day WHouse kumbe mnyama yuko hewani kwa siri kubwa Iraq.....
 
Back
Top Bottom