Dola yaendelea kupaa

trplmike

JF-Expert Member
Apr 2, 2012
701
776
Leo nimeona bei ya kuuza dola huku mtaaani ni 2170 na ya kununua dola 2200.

Inaendelea kupanda kwa kasi
20160108_140532-jpg.315591
 
Attachments

  • 20160108_140532.jpg
    20160108_140532.jpg
    138.1 KB · Views: 182
Last edited by a moderator:
Mkuu ulikuwa wapi ? Au sio mtu wa Current Affairs.. ?

Sio yaanza kupaa bali yaendelea kupaa..., haijaanza jana wala juzi
 
ndo effect ya wafanyabiashara kuficha ela? nadhan kama wanafanya makusud maguful anatakiwa awashukie kwa rungu zito sana!!!
 
ndo effect ya wafanyabiashara kuficha ela? nadhan kama wanafanya makusud maguful anatakiwa awashukie kwa rungu zito sana!!!
Na ndio maana tulitaka rais abadili hela ya tanzania.
 
Tuanze kutumia dola kama Zimbabwe, hizi hela za madafu ya msoga haziwezi kupanda thamani kabisa
 
Yaani their buying price of Euro ni chini ya buying price ya dollar? Nipelekeni shule
 
Ukweli uko hivi, dola imepanda dhidi ya fedha nyingi , kwa mfano dola sasa hivi impepanda hata dhidi ya pound ya uingereza. kuna maamuzi yamefanyika katika nchi ya marekani inayoifanya dola iwe na thamani sana. ukiangalia hata leo nchi ya china imeshusha thamani ya fedha yeke dhidi ya dola NA SIO dhidi ya fedha nyingine za nchi jirani na china. wataalam wa masuala ya fedha wanaweza fafanua zaidi.
 
Ndullu na genge lake hapo BOT wanatakiwa wachukue hatua za kulinda thamani ya fedha yetu; marekani wamependisha interest rate hivyo wawekezaji wengi wanakimbilia kuwekeza huko na hivyo demand ya dollar duniani inakuwa kubwa na thamani ya fedha kama madafu yetu lazima ipungue kwani utatumia shilingi nyingi kununua dollar moja!!

Hali ilivyo hapo BOT inaelekea huyo gavana hana uwezo tena wa kuongoza chombo hicho baada ya kashfa za escrow na kadhalika hivyo Magufuli hana budi kuanza kutafuta replacement itakayoendana na vision yake kwani huyo na mkweree lao ni moja kumuacha hapo ni kufuga kirusi!!
 
Leo nimeona bei ya kuuza dola huku mtaaani ni 2170 na ya kununua dola 2200.

Inaendelea kupanda kwa kasi
20160108_140532-jpg.315591
Mimi swali langu halihusiani na kupanda au kushuka kwa dola. ila naona bills ndogo ndogo ($1, 5, 10 &20) wauzaji wote wanazinunua kwa gharama pungufufu ya zile kubwa ($50 &100), ni kwa sababu gani? Na kwa kuzingatia sababu hiyo hiyo, kwa nini wao wanaziuza kwa thamani sawa na zile kubwa kubwa? Mfano, angalia tangazo lililonukuliwa.

Najua mpo humu wamiliki wa Bureau de Change, hebu tuelimisheni juu ya hilo.
 
Ndugu yangu Utotole, huu ujinga unalindwa na BOT. Huo mchezo kwamba small denominations za dola zinanunuliwa bei tofauti na noti ya dola 100 na 50, upo Tanzania tu. Nchi niynigne dola ni dola na gharama yake ni ile ile bila kujali denominations. BOT inabidi waingilie kati kufuta upuuzi huu. Hao wa Bureau De Change hawawezi kukupa jibu lolote kwani wao wanafaidika sana na upuuzi huu.

Tiba
 
Yaani dola imekuwa na bei kubwa kuliko Euro? Haya ni maajabu ya mwaka mpya 2016.
Mkuu Tiba Euro iko juu kidogo sana ya dola kwa sasa.Lakini kwa sababu demand ya Euro sio kubwa sana kwa Tanzania ndio sababu dola ni ghali kuliko Euro kwenye soko la chenji Tanzania.Hii ni kwenye kuuza lakini kwenye kununua Euro ni ghali kwa kuuzwa 2300 kwa Euro 1 na dola 1 kuuzwa 2200.
 
Last edited:
Back
Top Bottom