Zikomo Songea
JF-Expert Member
- May 15, 2016
- 670
- 580
Gazeti la The Star la Kenya jana liliandika makala kuhusiana na kushuka kwa ushawishi wa Kenya katika Afrika Mashariki. Mwandishi wa makala hiyo "The empire is falling: Why Kenya's influence in East Africa is on a download spiral", bwana Kenneth Okwaroh, anataja matukio katika yanayoashiria kuanguka kwa dola ya Kenya.
Kiasi Iringa cha kwanza anachokitaja ni kushinda kwa Kenya kupata kandarasi ya Kujenga bomba la kusafirisha mafuta kutoka Uganda kupita bandari ya Lamu. Itakumbukwa kuwa Uganda ilianza kuwa bomba hilo litajengwa kupita badari ya Tanga, Tanzania. Pili, ndiyo ya Sudan ya Kusini kujenga bomba la mafuta pia kupita Kenya ni kama zimeyeyuka. Tatu, Uganda na Tanzania tayari zimesaini makubaliano mengine juu ya ujenzi wa reli sambamba na bomba la mafuta. Endapo hilo litanyika, mradi Kenya wa ujenzi wa "Standard Gauge Railway" (SGR) hautaweza kufanya kazi kama ilivyokusudiwa.
Mwandishi anadai kuwa katika siku za nyuma Kenya ilikuwa ni kiungo muhimu kwa maswala mbalimbali ya kiuchumi na kisiasa. Ilikuwa ni kitovu cha usafirishaji, mawasiliano na uwekezaji katika Afrika Mashariki Itiji uniachie eneo kubwa la nchi, rasilimali na idadi kubwa ya watu wake.
Mwandishi anahoji ni wapi Kenya ilianza mpaka ushawishi wake unashuka kwa kasi hii? Nini kimebadilika?
Anasema kwanza, taarifa za ukuaji wa uchumi kwa miaka kadhaa zinaonyesha kuwa uchumi wa Rwanda na Tanzania umekuwa kwa kasi ya 7.0% wakati Kenya ni 5.0% pekee. Pili, tofauti na mshindo ni wake mkuu Tanzania, siasa za Kenya bado zinarudishwa nyuma na ukabila na marumbano ya kisiasa tangu ilipopata uhuru. Zaidi ni kuwa eneo kubwa la ardhi na bahari ya Tanzania libata fursa kwa Tanzania kuwa na rasilimali nyingi, ukiwemo gesi. Tanzania inahifadhi kubwa kabisa ya gesi ikilinganishwa na Kenya. Maslahi binafsi miongoni mwa Wakenya yanatajwa pia kukimbiza wawekezaji ambao wanaogopa gharama kubwa za fidia kwa wananchi. Mfano wa bomba la mafuta hadi Uganda unahusika.
Mwandishi anataja pia majivuno ya kidiplomasia (kama vile migogoro na ICC na kitendo cha kuendelesha mikutano mikubwa ya kimataifa ili kujitutumua) haina tija yoyote kwa taifa. Pigo jingine ni kwamba tafiti za idadi ya watu zinaonyesha Kenya itaachwa mbali na Tanzania kufikia 2030 (kwa sasa Kenya ina watu mil 45.5). Anasema yote hayo yanaifanya Kenya kuwa si chochote katika eneo la Afrika Mashariki.
Watanzania tunasemaje? Karibuni kwa tafakari.