Dola 250,000 zaibwa CCM UK?

Niliwahi kusema haya huko nyuma kuwa walioko nje ya nchi ambao ni wapenzi wa ccm wengi ni wanufaika na system ya kibongo (Mtoto kama baba). Ndio maana pamoja na kubahatika kwa vipindi fulani kuwepo huko UK, sikuweza kuwa na imani na vijana wa kibongo niliokuwa nikikutana nao kwa upenzi wa nchi yao. Inanikumbusha hata wale wenye kampuni za kuthibitisha ubora wa magari yaingizwayo kutoka uk. Naamini hii mbegu iliyopandwa na ccm ni mbaya, na matunda yake bila kujali yanachumwa kutoka tawi gani (uk au US) bado ni mabovu!

Haiingii akilini mnafursa za kubeba maboksi huko mkatengeneza paundi kuliko daladala hapa bongo, halafu fedha ya msukuma mkokoteni huku ndio tunakutumieni. Kweli hiki chama kimetunajisi!
 
Hii nchi ni shamba la bibi unachota maji bombani unayapeleka baharini duh!
 
Kama ni kweli hili limetokea, basi hiki chama kimejaa wezi watupu. na huu mchongo utakuwa umetengenezwa hapahapa bongo na hela zitakuwa zimegawanywa hapa hapa bongo ila kule itakuwa reference tu, wameangalia kuiba serikarini chadema ipo macho wakaona waibe kwenye chama chao, nawatia moyo waendelee kutafuna mi hela, sababu bado kitambo kidogo watazikosa, sasa wasije jilaumu nawashauri na matawi ya Italy na USA wachangamke huu ndio wakati wa mavuno!
 
walau wameanza kuwajibishana..japo imechukua miaka 4
 
walau wameanza kuwajibishana..japo imechukua miaka 4
Hakuna mtu aliekula pesa, hizo hela zilikuwa za mradi, mradi umefanywa na mtu mmoja ambae ilibidi aende re-mortage nyumba yake, kasafiri sana China na kurudi kwa gharama zake na kaenda sana Lumumba kudai hela zake baada ya kutimiza upande wake.

Mwishowe kawapa zawadi CCM mradi ulipotokea hili chama kiwe na kiasi kadhaa cha akiba. Watu wanataka nusu ya faida bila ya kujali gharama za mwenzao, idea yake na hela yenyewe imelipwa taratibu mno. Hadithi tu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…