Dogo Aslay ndio alikuwa mbadala wa Diamond kwenye bongofleva. Ila kwa nini anachukuliwa poa hivi?

mr gentleman

JF-Expert Member
Aug 1, 2012
3,223
4,681
Binafsi kwa sasa sijaona msanii mwenye kipaji cha aina ya Aslay kwenye bongofleva kwa sasa. Huyu kijana ana uwezo mkubwa mpaka sioni wa kumfananisha nae kwa sasa, kumekuwa na mjadala Diamond kijiti chake anastahili kumuachia nani? Mimi nasema wazi Aslay ndio mrithi wa Diamond, sioni mwingine.

Nisichoelewa ni kwa nini watanzania wanamchukulia poa. Ata management yake sijui kwa nini haimpi uwanja anaostahili! Ya Moto bila Aslay ni kama kisu bila makali, naamaanisha Aslay ndio anaibeba ya moto. Na kiukweli Ya Moto imeshakinai wananchi, nashauri Fela aache vijana waende solo sasa ili dunia ianze kufaidi kipaji cha Aslay.

Tuna mifano ya kidunia ya wasanii walioenda solo na kupaa zaidi na zaidi, Wycliffe Jean, Beyonce, Sisqo, Omarion, Prof Jay nk.

Naisikiliza 'kidawa' 'tete' na 'rudi!' nazidi kumvisha nyota nyingi mabega yote Dogo Aslay. The next big Super Dupa Star.
 
Dogo asubiri kuokota makopo kagombana na miungu wa muziki Tanzania

Ila kusimama mwenyewe anaweza lakini fela, tale hawatakubaliana na hilo
 
N kwl mkuu hata mi nimeona hicho kitu ray vanny platnumz naye alikuwa chini ya kina madeale lkn hakuwah kusikika mpaka alipopata promo kutoka wcb siyo kwamba anapuuzwa promo na kujibeba ndo vimekosekana ila kijana yuko vzr kwl
 
Kweli mkuu.

kiuwezo Diamond amfikii hata ManFongo kinachombeba ni hizo Kiki na promo anazopewa na kina Tale.
 
Kweli mkuu.

kiuwezo Diamond amfikii hata ManFongo kinachombeba ni hizo Kiki na promo anazopewa na kina Tale.
Ningeshangaa sana kama usingeleta pua yako huku utakufa kwa roho mbaya
5d99c0352526fa6ae2c1285c8049b690.jpg
hapo ni omani siyo tz unasikia aje
 
Duh enzi hizo Aslay ndio sehemu yao ya kupunguza sumu zao...Hapa walikuwa wanafarijiana Diamond kashapotea ni muda wa Aslay 😂😂😂😂
 
Back
Top Bottom