Dodoso kuhusu sensa 2022

Dodoso kuhusu sensa 2022

test man

JF-Expert Member
Joined
Aug 13, 2016
Posts
1,014
Reaction score
970
Ndugu zangu naomba niwataarifu kuwa Sensa ya Watu na Makazi 2022 itahusisha madodoso manne:
1: Dodoso la Jamii
2: Dodoso la Sensa ya Watu na Makazi
3: Dodoso la Makundi Maalum
4: Dodoso la Majengo

1. Dodoso la Jamii litaanza kwa kumuhoji mwenyekiti au mjumbe wa kitongoji au mtaa juu ya uwepo wa huduma za kijamii ktk eneo lake. Kama zipo basi karani atambatana na kiongozi wa kitongoji au mtaa kwenda kwa mkuu wa taasisi husika kwenda kumuhoji mambo yanayohusu huduma hiyo. Huduma za kijamii ni kama vile soko, maeneo ya huduma za afya, elimu, mitandao ya mawasiliano na taasisi za dini kwa maana ya misikiti na makanisa. Pia litahoji vitu kama mabadiliko ya tabia za nchi, matukio mbalimbali katika eneo husika n.k.

Dodoso la jamii litahojiwa siku 2 kabla ya siku ya sensa. Yaani litaanza kuhojiwa tarehe 21 hadi 22 Agosti 2022.

2. Dodoso la Makundi Maalum
Katika kuhakikisha kila mtu anahesabiwa na anahesabiwa mara moja tu basi hata watoto wa mitaani ambao hawana makazi, wasafiri ambao walilala stendi, makambi ya wavuvi na wachoma mkaa n.k. wote watahesabiwa kwa kutumia Dodoso la makundi maalum. Makundi haya yatajumuisha pia Askari wetu ambao siku ya sensa itawakuta wakiwa wanalinda mipaka ya nchi yetu. Makarani watakuwepo maeneo ya makundi maalumu saa sita usiku. Yaani, Dodoso hili litaanza kuhojiwa saa sita usiku wa tarehe 22/08/2022.

3. Dodoso la Sensa ya Watu na Makazi. Hili linaitwa Dodoso kuu. Linakadiriwa kuwa na maswali 100. Ni mengi lakini hayachoshi maana ni mahojiano ya ana kwa ana (face - to - interview).
Dodoso hili litahojiwa kwa kila kaya.

Hapa naomba nifafanue maana ya kaya. Kaya ni mtu au watu ambao huwa wanaishi pamoja na kula pamoja. Kaya sio sawa na familia. Familia huwa ni ya watu wenye undugu, lakini kaya inajumuisha watu wote wanaoishi na kula pamoja hata kama hawana undungu.

Kwenye Dodoso la Sensa ya Watu na Makazi ndipo pana swala la kuhesabu watu waliolala kwenye kaya siku ya kuamkia siku ya Sensa (23/08/2022).

Nani ahesabiwe na nani asihesabiwe?

Nani ahesabiwe?
Kila aliyelala na kuamkia siku ya sensa tarehe 23 Agosti 2022 ndani ya mipaka ya Tanzania. Hii haijalishi uraia wake, ilimradi tu amelala na kuamkia nchini Tanzania.

Hapa ifahamike kuwa uhesabuji utaanza saa sita kamili usiku, tarehe 22/08/2022. Hivyo chukulia kama picha inapigwa muda huo kuchukua sura za binadamu walio hai. Hivyo kila binadamu aliye hai atakayetokea kwenye picha hiyo ndio atahesabiwa. Hapa sasa inakuja hoja tunazotakiwa kuzikumbuka.

Je, tutahesabu mtoto aliye tumboni. *Hapana maana kwenye picha hataonekana.

Je tutahesabu maiti ya aliyefariki saa tano na dakika 59 usiku? *Hapana hatuta mwesabu.
Lakini mtoto aliyezaliwa saa tano na dakika 59 atahesabiwa.

Mtoto aliyezaliwa saa sita na dakika moja hapaswi kuhesabiwa maana kwenye picha hajaonekana.

Mtu aliyefariki saa sita na dakika moja anapaswa kuhesabiwa maana kwenye picha alionekana na akafariki baadae.

Kwa hiyo Wasiotakiwa kuhesabiwa ni kama hao niloanza kuwataja watoto waliozaliwa baada ya saa sita na waliokufa kabla ya saa sita. Na wote ambao hawakuwa nchini usiku wa kuamkia siku ya Sensa.

4. Dodoso la Majengo. Hili ni dodoso la mwisho katika mfululizo na ni la mwisho kuhojiwa baada ya dodoso la SENSA ya Watu na Makazi. Hapa serikali inataka kujua tu takwimu za majengo na hali ya umiliki pamoja na thamani ya jengo SI kwa madhumuni ya kuuza hapana. Bali kwa ajili uandaaji wa kanzi data na Mambo mengine yahusuyo Sera.

Sensa ya mwaka huu ni ya kidijitali. Inapokea na kuchambua taarifa Kwa haraka kupitia mfumo wa kompyuta. Hivyo tuwe tayari kuhesabiwa.

Wengine watasema watakuwa kwenye majuku yao. Tujitahidi kuwaeleza kuwa wsiache kufanya kazi zao bali tuwaambie kuwa

Wahakikishe wanaaacha majina matatu, taarifa za tarehe za kuzaliwa taarifa za hali ya ndoa , elimu paomoja na uhamaji wa watu wote walioamkia kwenye kaya zao siku kuamkia siku ya sensa.

Pia makarani watahoji maswali ya shughuli za kiuchumi. Hivyo Wananchi waweke tayari taarifa ya kila mwanakaya kuwa anajishughulisha na nini?

Pia kutakuwa na maswali ya vizazi na vifo. Hapa mwanamke wa umri wa miaka 10 na kuendelea ataulizwa amezaa watoto wangapi wakiwa hai. Lakini pia kaya imepata misiba mingapi ndani ya mwaka mmoja (miezi 12 iliyopita.)

Tunaomba ushirikiano wako kwa karani atakeyekufikia kwani ni lazima ufikiwe na uhesabiwe mara moja tu.

SENSA KWA MAENDELEO....JIANDAENI KUHESABIWA NAMI NIPO TAYARI KUWAHESABU

*by imbwaghe *
 
Nami nakupa taarifa hii ,katika nchi yoyote RAIA huwa wanasikilizwa na viongozi wao :lakini WATUMWA katika nchi yoyote huwa hawasikilizwi Sasa jiulize Leo wewe na familia yako mko katika nchi ya watumwa au Raia!!!!
 
Duh kwa hii kazi ilivyo ngumu ilipaswa kila karani alipwe walau 2.5M kwa zoezi zima.
 
Tumefanya sensa nyingi sana mpaka sasa na lengo la sensa ni kujua idadi ya watu katika mitaa/vijiji, wilaya, mikoa na nchi kwa ujumla ili kuwezesha usambazaji wa huduma muhimu za kijamii kama vile maji, umeme, hospitali n.k. Lakini haya hayajafanika katika mitaa, vijiji na hata mikoa mingi toka sensa 2002.

Kuna senta, na miji inakua kwa kasi sana na mwenye kujua kuwa inakua kwa kasi na kwa kiwango gani ni serikali kupitia sensa kama hii lakini imeshindwa hata kuandaa mpangilio wa barabara katika maeneo hayo mbali na kusambaza nguzo za umeme, mabomba ya maji, zahanati au hospitali kwendana na idadi ya watu katika maeneo hayo.

Je, serikali itanishawishije kushiriki hili zoezi kwa kukaa masaa mawili na zaidi nikifanyiwa interview na mtu aliyelipwa kodi za wanyonge wenzangu hali zoezi (sensa) lenyewe hususanuni la nyuma halijaweza kuzaa matunda ya mimi kuletewa umeme,maji, huduma za afya tangu nchi hii ipate uhuru?
 
Makarani mmeomba lifti kwenye mtumbwi wa vibwengo
 
Ndugu zangu naomba niwataarifu kuwa Sensa ya Watu na Makazi 2022 itahusisha madodoso manne:
1: Dodoso la Jamii
2: Dodoso la Sensa ya Watu na Makazi
3: Dodoso la Makundi Maalum
4: Dodoso la Majengo

1. Dodoso la Jamii litaanza kwa kumuhoji mwenyekiti au mjumbe wa kitongoji au mtaa juu ya uwepo wa huduma za kijamii ktk eneo lake. Kama zipo basi karani atambatana na kiongozi wa kitongoji au mtaa kwenda kwa mkuu wa taasisi husika kwenda kumuhoji mambo yanayohusu huduma hiyo. Huduma za kijamii ni kama vile soko, maeneo ya huduma za afya, elimu, mitandao ya mawasiliano na taasisi za dini kwa maana ya misikiti na makanisa. Pia litahoji vitu kama mabadiliko ya tabia za nchi, matukio mbalimbali katika eneo husika n.k.

Dodoso la jamii litahojiwa siku 2 kabla ya siku ya sensa. Yaani litaanza kuhojiwa tarehe 21 hadi 22 Agosti 2022.

2. Dodoso la Makundi Maalum
Katika kuhakikisha kila mtu anahesabiwa na anahesabiwa mara moja tu basi hata watoto wa mitaani ambao hawana makazi, wasafiri ambao walilala stendi, makambi ya wavuvi na wachoma mkaa n.k. wote watahesabiwa kwa kutumia Dodoso la makundi maalum. Makundi haya yatajumuisha pia Askari wetu ambao siku ya sensa itawakuta wakiwa wanalinda mipaka ya nchi yetu. Makarani watakuwepo maeneo ya makundi maalumu saa sita usiku. Yaani, Dodoso hili litaanza kuhojiwa saa sita usiku wa tarehe 22/08/2022.

3. Dodoso la Sensa ya Watu na Makazi. Hili linaitwa Dodoso kuu. Linakadiriwa kuwa na maswali 100. Ni mengi lakini hayachoshi maana ni mahojiano ya ana kwa ana (face - to - interview).
Dodoso hili litahojiwa kwa kila kaya.

Hapa naomba nifafanue maana ya kaya. Kaya ni mtu au watu ambao huwa wanaishi pamoja na kula pamoja. Kaya sio sawa na familia. Familia huwa ni ya watu wenye undugu, lakini kaya inajumuisha watu wote wanaoishi na kula pamoja hata kama hawana undungu.

Kwenye Dodoso la Sensa ya Watu na Makazi ndipo pana swala la kuhesabu watu waliolala kwenye kaya siku ya kuamkia siku ya Sensa (23/08/2022).

Nani ahesabiwe na nani asihesabiwe?

Nani ahesabiwe?
Kila aliyelala na kuamkia siku ya sensa tarehe 23 Agosti 2022 ndani ya mipaka ya Tanzania. Hii haijalishi uraia wake, ilimradi tu amelala na kuamkia nchini Tanzania.

Hapa ifahamike kuwa uhesabuji utaanza saa sita kamili usiku, tarehe 22/08/2022. Hivyo chukulia kama picha inapigwa muda huo kuchukua sura za binadamu walio hai. Hivyo kila binadamu aliye hai atakayetokea kwenye picha hiyo ndio atahesabiwa. Hapa sasa inakuja hoja tunazotakiwa kuzikumbuka.

Je, tutahesabu mtoto aliye tumboni. *Hapana maana kwenye picha hataonekana.

Je tutahesabu maiti ya aliyefariki saa tano na dakika 59 usiku? *Hapana hatuta mwesabu.
Lakini mtoto aliyezaliwa saa tano na dakika 59 atahesabiwa.

Mtoto aliyezaliwa saa sita na dakika moja hapaswi kuhesabiwa maana kwenye picha hajaonekana.

Mtu aliyefariki saa sita na dakika moja anapaswa kuhesabiwa maana kwenye picha alionekana na akafariki baadae.

Kwa hiyo Wasiotakiwa kuhesabiwa ni kama hao niloanza kuwataja watoto waliozaliwa baada ya saa sita na waliokufa kabla ya saa sita. Na wote ambao hawakuwa nchini usiku wa kuamkia siku ya Sensa.

4. Dodoso la Majengo. Hili ni dodoso la mwisho katika mfululizo na ni la mwisho kuhojiwa baada ya dodoso la SENSA ya Watu na Makazi. Hapa serikali inataka kujua tu takwimu za majengo na hali ya umiliki pamoja na thamani ya jengo SI kwa madhumuni ya kuuza hapana. Bali kwa ajili uandaaji wa kanzi data na Mambo mengine yahusuyo Sera.

Sensa ya mwaka huu ni ya kidijitali. Inapokea na kuchambua taarifa Kwa haraka kupitia mfumo wa kompyuta. Hivyo tuwe tayari kuhesabiwa.

Wengine watasema watakuwa kwenye majuku yao. Tujitahidi kuwaeleza kuwa wsiache kufanya kazi zao bali tuwaambie kuwa

Wahakikishe wanaaacha majina matatu, taarifa za tarehe za kuzaliwa taarifa za hali ya ndoa , elimu paomoja na uhamaji wa watu wote walioamkia kwenye kaya zao siku kuamkia siku ya sensa.

Pia makarani watahoji maswali ya shughuli za kiuchumi. Hivyo Wananchi waweke tayari taarifa ya kila mwanakaya kuwa anajishughulisha na nini?

Pia kutakuwa na maswali ya vizazi na vifo. Hapa mwanamke wa umri wa miaka 10 na kuendelea ataulizwa amezaa watoto wangapi wakiwa hai. Lakini pia kaya imepata misiba mingapi ndani ya mwaka mmoja (miezi 12 iliyopita.)

Tunaomba ushirikiano wako kwa karani atakeyekufikia kwani ni lazima ufikiwe na uhesabiwe mara moja tu.

SENSA KWA MAENDELEO....JIANDAENI KUHESABIWA NAMI NIPO TAYARI KUWAHESABU

*by imbwaghe *
Nyinyi bana,
Hayo maswali 100 ambayo siyajui hata ni yapi ndo mlitaka nimkaririshe beki tatu ?
 
Back
Top Bottom