Jiji la Abuja huko Nigeria..
Ramani ya Mji huu inasadikika ilichukuliwa kwenye ramani ya Ujenzi wa Mji mkuu wa Tanzania-Dodoma lakini wakati CDA wakibaki na makaratasi tu miaka nenda rudi mpaka Magufuli alipokuja kuivunja CDA, Nigeria wao walioomba hii Ramani na kuifanyia kazi Taifa ambalo lilikumbwa na migogoro ya wenyewe kwa wenyewe,Mapinduzi ya Kijeshi ya Mara kwa mara, na changamoto chungumzima lakin ndio Taifa lenye Uchumi mkubwa zaidi Afrika.
Nigeria inasifiwa kwakua uchumi wake haukuhusisha watu weupe kama ilovyo Afrika Kusini,Bali maendeleo yote ya Nigeria yametokana na wao wenyewe (weusi)
Hii ndio sababu inayowaponza kwani mataifa ya Magharibi yanaumia kuona taifa ambalo halina mkoko wa Mzungu inakuaje liwe na Uchumi mkubwa kuizidi Afrika Kusini ambayo Uchumi wake umekolezwa ,zadi na uwepo wa Makaburu wazungu wahamiaji kutoka Uholanzi kabla ya Ukoloni?
Makaburu waliopo Afrika Kusini ni zao la wazungu ambao walitoka Uholanzi karne nyingi kwa nia ya kwenda India kutafuta maisha kwa kuzunguka bara la Afrika kupitia Kusini lakini walipofika Afrika Kusini wakaona walichokuwa wanakifata India kipo pale wakapiga kambi na kulowea hapo,
Hata ilipofika kipindi cha Ukoloni Waingereza walipofika pale wakawakuta watu weupe na iliwapa ugumu sana kuitawala Afrika Kusini kwakua wale weupe hawakukubali kirahisi ndipo Waingereza wakawahadaa waafrika kuwa waholanzi wale wanawanyonya wao wamekuja kuwasaidia ndipo walipowashinda makaburu kwa kushirikiana na mtu mweusi, jambo hilo liliongeza chuki kwa Waholanzi kwani awali waliishi na wenyeji vizuri lakini wakagombanishwa ndipo uhasama ukaanza ,hata baada ya Uhuru Makaburu waliposhika nchi wakaendeleza visasi ndipo Waafrika walipokoma sasa kichaa kapewa rungu.
Makaburu wakatengwa na Ulimwengu kwa kuwanyanyasa weusi (wenyeji) kama Ilivyo Irani na Korea Kaskazini,ukitengwa unajitahidi ujitegemee kwa kila kitu,wakaanza kutengeneza Uchumi wao makaburu ili wawe imara wasitishwe au kuvamiwa wakaunda mpaka silaha za nyuklia,