Pistol
Senior Member
- Oct 13, 2015
- 194
- 86
Serikali kwa kushirikiana na benki ya dunia imekamilisha ujenzi wa kituo cha kusambaza umeme msongo wa Kilovolt 400 kilichopo mjini Dodoma kitakachosaidia kupunguza tatizo la ukosefu wa umeme katika mkoani huo pamoja na mikoa ya jirani.
Akizungumza wakati wa kutembelea mradi huo wa Backbone, Meneja mradi Bwana Oscar Kanyama,amesema mradi huo unatokea Iringa hadi Dodoma umefadhiliwa na benki ya dunia kwa jumla ya dola Milioni 134.5 ujenzi ambao unafanywa na kampuni ya Kimatifa ya KC toka nchi India.
Kwa upande wake Mhandisi kutoka wizara ya nishati na Madini Bwana.Salum Inegeja amesema mradi huo Backbone ni sehemu ya mradi mkubwa wa unaounganisha Kenya,Tanzania na Zambia nchi hizo zilikubalina kila nchi kutekeleza sehemu ya mradi huo kwa upande wake.
Aidha wakizungumzia jinsi wanavyonufaika na mradi huo baadhi ya wakazi wa mkoa wa Dodoma walihamishwa katika maeneo yao kupisha ujenzi wa mtandao wa usambazaji umeme wamepongeza jitihada za Serikali na benki ya dunia katika kuondoa tatizo la umeme mkoani hapo huku wengine wakionesha namna walivyonufaika kwa kujenga nyumba za kisasa kutokana na malipo ya fidia.