DODOMA: Mbunge wa Arusha Mjini Mh. Godbless Lema awataka IGP na Mwigulu Nchemba wakauze maandaazi

Hivi punde

JF-Expert Member
Apr 1, 2017
2,554
8,552
Mbunge wa Arusha Mjini (Chadema) Godbless Lema amewataka Waziri wa Mambo ya Ndani Dk Mwigulu Nchemba na Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini Simon Sirro kwenda kuuza maandazi kama wameshindwa kukomesha mauaji, utekaji na unyanyasaji.

Akichangia bajeti ya Wizara ya Mambo ya Ndani kwa mwaka wa fedha 2018/19, Lema amesema kuwa Jeshi la polisi limeharibiwa na kuingiza masuala ya kisiasa.

“Leo unasikia mtu ameuawa Mbeya, leo mdogo wake Heche (Mbunge wa Tarime Vijijini John Heche) amepigwa kisu akiwa kwenye pingu ndani ya gari la polisi, wameenda kutupa mwili dereva bodaboda akaona wakasema, wakapiga kelele.

“Yuko hapa IGP nimekuwapo katika Bunge hili nimeona (wabunge) wakipiga kelele wakisema Harbinder Singh Sethi fedha ni zake lakini bunge hii hili wakisema asulubiwe. Nakwambia kabla jogoo hajawika hao watu waliokutuma kazi leo kuna siku watakuning’iniza, sio kila maelekezo ya kuuumiza watu mnayachukua.”

Lema amesema kuwa Mbunge wa Singida Mashariki (Chadema) Tundu Lissu alipigwa risasi lakini Waziri wa Nishati Medard Kalemani aling’oa kamera (CCTV) nyumbani kwake ili kupoteza ushahidi.

“Ben Saanane amepotea, Azory amepotea, maiti zinaokotwa mchangani Waziri Mwigulu anasema hizi maiti zimeuawa na watu wasiojulikana kama kuna waziri wa Mambo ya Ndani, kuna IGP maiti zinaokotwa zaidi ya 1,000. Unakaa ofisi unafanya nini nenda ukauze maandazi,”amesema.

Lema amesema wanahimiza demokrasia si kwa ajili ya viongozi tu wa upinzani tu bali kwa faida ya Taifa kwa sababu wao wanaweza kufanya biashara na kuachana na siasa.

Chanzo: Mwananchi
 
Wakupuuzwa tu huyu
 
Hapana, siasa tuweke pembeni kwa hili Lema yuko sahihi, anachotaka ni serikali ichukue hatua za haraka kuzuia mambo haya nchini, hivi tujiulize inakuaje Raia anakufa mikononi mwa polisi? kibaya zaidi polisi wanashiriki kwenda kutupa mwili wa mtu kisiri? huu ni unyama ambao hatutakiwi kuukubali, tuseme ukweli katika mawaziri mzigo katika serikali ya Magufuli basi mwigulu ni mmoja wao, hapo anabebwa na ukada wake na Uccm tu lakini ni jipu .
 
Kama Polisi wameshindwa kutimiza wajibu wao watu wote wapige kimya sio?? Mimi nafikiri kuna Watz wenye laana fulani mmoja wapo ni wewe.
Polisi wameomba msaada kwako. Na kwanini hayo mapovu msiyatolee hadharani. Mbona mnatolea kwenye mitandao. Rais kila anapokuwa kwenye ziara zake hutoa fursa kwa wananchi ili watoe kero zao, mbona sijawahi kuona MTU amejitokeza kulielezea hili.
 
Back
Top Bottom