Dodoma: Ambaka bibi kizee wa miaka 77 hadi Kufariki

Kanungila Karim

Verified Member
Apr 29, 2016
17,218
2,000
MUROTO-5.jpg


KAMANDA wa Polisi Mkoa wa Dodoma, Gilles Muroto, amesema jeshi hilo limemkamata kijana William Simon kwa tuhuma za kumbaka Bibi Kizee Jema Macheho (77) na kumsababishia kifo akiwa anapatibiwa Hospitali ya Rufaa Mkoa wa Dodoma.

Aidha, Muroto amesema jeshi hilo linawashikilia watuhumiwa wanne wa makosa mbalimbali yakiwemo wizi wa hati za viwanja, kugushi na kubadili ramani za mpango-mji, kubadili mpango wa matumizi ya ardhi, kuuza viwanja na kuingilia Mifumo ya Utunzaji wa Kumbukumbu za Ardhi na kuuza viwanja kwa njia ya utapeli.

Akizungumza na waandishi wa habari leo, Muroto amesema watu wamekuwa wakisababisha migogoro ya ardhi kwa wananchi kutokana na tabia hiyo.

“Wanasababisha migogoro mingi ya ardhi katika jiji letu la Dodoma, wanashirikiana na watumishi ambao si waaminifu na kupelekea kuingilia mifumo ya halmashauri ya ardhi,” amesema.

Ameongeza kuwa watuhumiwa wote wanahojiwa kuhusiana na tuhuma hizo na walipopekuliwa wamekutwa na nyaraka kadhaa husika na muda wowote watafikishwa mahakamani uchunguzi uatakapokamilika.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom