Do You Remember ?

Red Scorpion

JF-Expert Member
Feb 1, 2012
5,736
4,252
1473142902614.jpg
 
Naikumbuka sana hii kitu aiseeee...... tena ilikua inatengenezwa kwa aluminum, mbaya zaidi ukipewa uji kwenye hiyo Mess Tin lazima ukuunguze mdomoni
 
miaka ya tisini na mbili mpaka na tano hicho kilikuwepo home. baada yahapo kilikusanywa kwenye chuma chakavu

afu ilikua full aluminium
 
Nakumbuka sana nyumbani tulikuwa navyo vingi sana
Basi ujue dingi yako alikuwa ni fisadi wa Vyombo Jeshini....

Sisi tulikuwa na Ndugu kibao jeshini waliporejea vitani walikuwa na vitu vingi vya kijeshi like gas cube na hizo sufuria pia vibag fulani vya kijeshi vidogo vidogo tumeenda navyo sana shule za primary kuwekea madaftari Biskuti za wanajeshi ngumu sana zilikuwa na hazina utamu fresh ila ukiwa na njaa unaona tamu... pia bila kusahau walikuwa na vile visu vya mtutu wa bunduki tunavichezea havina ukali... baadae wakavirejesha Jeshini... ni aina ya aluminum Ngumu sana... sikuwahi viona tena hadi one day miaka ya 2009 au 2011 alikuja jamaa akidai anatafuta sample ya chuma hicho au mtu wa kutengeneza kama anaweza kipata tukamuambia hayo mambo ya jeshi alafu kitambo sana... akadai anatokea huko huko nikamuambia aende Dar Tech akasema wameshindwa nikaona mmh! nikajua chezo hilo maybe wameibiwa so wanachunguza.... Jamani Mambo ya Jeshi waachiwe wenyewe... tuache kuyajadili...
 
Inaitwa MISTINI jeshi hutumia sana hii kitu

Uko sahihi...'mistini'..lugha ya kijeshi ... lakini usahihi nadhani ni 'mess tin'...halafu kijeshi kuna kitu kinaitwa 'lalamu' (utasikia lalamu imepigwa) lakini usahihi nadhani ni 'alarm'...tehtehteh mambo ya jeshi bwana yanafurahisha sana au mkuu wa kikosi anaitwa 'Siyoo' lakini usahihi ni C.O yaani 'Commanding Officer'.... tehtehteh
 
"Niitie yule aliyevaa Green vest ya kijani....."
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom