Do we need a Price Regulatory Authority in Tanzania?


Mkuu Kobello haya malinganisho sijui huwa mnayafanya kwa sayansi gani ya kiuchumi.
Eti we pay 0.12$/Kwh while in the US 0.3/Kwh and went on to conclude 0.12$ is cheap??
Soda UK yaweza kuwa 90p (Tsh 2,250) wakati Reginald Mengi anatuuzia Tsh 500 which one is cheap to you??
Nimesoma mahali kwamba upo USA, naomba nikukumbushe kuwa per capita income yetu bado tumekwama $255 sasa ukitulinganisha na huko ulipo $33,000 ni sawa na kututukana tu kaka.

Kama umeme wetu ungekuwa cheap Minjingu wangetengeza mbolea ya bei ya chini kuliko ile inayotoka Russia.
Bei ya simenti itokayo Pakistan iko nafuu kuliko inayozalishwa Wazo hill.

Nchi imepotea wala hatujui (sisi na kiongozi) tuendako na hatujui tumepotea kiasi gani ila one thing I am convinced of "we need our own Hugo Chaves" atutoe tulipo kwanza then tujipange upya!
 
lakini katika soko huria kuna tabia ya wafanyabiashara kujiunga nakupanga bei ili lazima lidhibitiwe kwa uwepo wa tume ya ushindani na hii tume itaratibu ushindani na bei za vitu pasipo kuingiliwa na umoja wa wafanyabiashara yani bei zinatakiwa ziachwe free float ziamuliwe na soko. kama tusipokuwa waangalifu wafanyabiashara wanaweza kuunda umoja wao(catel) na kusababisha madhara makubwa kwa watumiaji na hii hasa hutokea kwenye biashara ambayo ina wasambazaji wachache kuliko wanunuzi kama vile umeme,simu,mafuta,mishahara
 
In fact, Kwa upande wa Tanzania hatuna kitu kinachoitwa Consumer Association. CA wangekuwa na wajibu wa kusimamia Bidhaa pamoja na Huduma mabalimbali katika kuangalia suala zima la Bei na Ubora wake. Kwa mfano wenzetu wakenya na nchi nyingine za Kibepari wanavyo vyama hivi ambavyo vinasimamia mwenendo mzima wa bei na ubora wa huduma pamoja na Bidhaa mbalimbali kwa mtumiaji wa mwicho. Katika mfumo wa nchi yetu jukumu hilo limeachiwa na TBS,SUMATRA, na EWURA. Kwa ujumla wameshinda kuwajibika kwavile wanamajukumu mengi na wakati mwingine mgongano wa majukumu baina yao. Ni fursa nzuri kwa wanauchumi wetu kuanzisha CA.
 

mheshimiwa kipo chama cha Consumer Association sema wanaokiendesha wamekifanya ni chombo cha kupata posho na kutowatetea wahusika kuna kikao kimoja kati ya SUMATRA na wadau wa usafirishaji wawakilishi wa chama hiki badala wawatetea watumiaji wao wanatetea wenye mabasi
 

wrong!! Hapa unavuka mipaka ya price control. I have experienced the same situation katika nchi zilizoendelea. Huwezi kupangia mwenye duka Mlimani City bei ya vitu vyake. Kama una shida na bei, fungua duka lako mshindane!

Price regulation inatakiwa kwenye vitu kama umeme, maji na usafiri! Hivi ni vitu ambavyo consumer hana nguvu ya ku-control. Kungekuwa na kiwanda kimoja na duka moja tu la viatu Tz, regulation yake ingekuwa sahihi. Lakini katika free economy and in relation to consumer goods, hakutakiwi kuwe na interference yeyote!!
 

wewe unachanganya mambo ya competition law/antitrust law na price regulation! Nadhani utakuwa ndio umetoka tu kujifunza hii kitu darasani. Embu pitia tena maelezo ya lecturer wako na jaribu kudadisi tofauti ya vitu unavyoongelea.
Kuna tofauti kubwa sana kwenye ishu za ku-regulate monopolies na price regulations ya mtu mwenye duka hapo mlimani.

Alafu kuna post ulizungumzia Obama administration na interference yake kwenye bei za nyumba. Note that i have used the word interference maana ni hicho tu ndio wanachoweza kufanya. Hawawezi ku-determine bei za nyumba, lakini wanaweza ku-interfere na ku-manipulate hizo bei kwa kucheza na interest rates na vitu vingine. I believe una-confuse two distinct ideas.
 
Kama shida ipo kwenye prices za consumer goods, we can start by having a public system of sharing price information.
 
Nadharia ni nzuri lakini mazingira yetu nayo ni unique ukiapply theories bila kujali hilo siku zote utakuta umekosea. Ushindani utatoka wapi wakati mtunga sera ndiyo 'mfanyabiashara mkuu'? Ewura na Sumatra wanajaza vaccum ya true consumer association. EWURA anaposema anaangalia gharama za kuzalisha umeme ndipo akubali ni muongo. Huhitaji kuwa na CPA au ACCA kujua kuwa hesabu za Tanesco hazireflect uhalisia wa gharama sehemu kubwa ni gharama za ufisadi thru IPTL, Dowans, Songas etc. Tunachohitaji ni chama imara cha walaji kinachoweza kusema bei hii haikubaliki na ikawa hivyo. WALAJI WA TZ TUNAKUWA PARTICIPATED NA HAYA MA EWURA NA SUMATRA they are there to protect their master while they PARTICIPATE US! Tufumbue macho- jk alisema anandaa bila ya kutenga siasa na biashara -where is it?
 

Consumer Protection haitakulinda na bei kubwa ila itakulinda na bidhaa feki au sub standard. Hauwei ukampangia mtu bei ya kuuza, market ndo inadetermine, kama kungekuwa hakuna mtu wa kununua hicho kiatu kwa hiyo bei ingebidi ashushe.

Kwa mfano kuna sehemu Dar bia moja inafika zaidi ya 7,000/= na hizo sehemu watu wanajaa na wanakunywa, so demand ipo ndo maana wanaweza kupanga bei hiyo. Bei ya bidhaa haipangwi kwa kuangalia cost tu, inapangwa kwa kuangalia market ipo tayari kulipa kiasi gani.

Pia kwenye mahesabu yako umesahau Tax unayotakiwa kulipa kama umenunua bidhaa kutoka nje na pia umesahau kuwa yule jamaa wa Mlimani anahitaji kulipia rent ambayo nina uhakika sio ndogo PLUS apate faida juu yake.
 
Tatizo ni mafuta! oil bei yake iko universal hapa duniani.Makampuni ya nje yanasita kuinvest kwenye umeme hapa tanzania na sababu mojawapo ni bei ndogo ya umeme! vitu kama soda na mkate bei zake huwezi kulinganisha na bei za nishati.Kugenerate umeme kwa kutumia mafuta,gharama zake ziko sawa duniani pote,ila kutengeneza soda na mkate,gharama zake zinatofautiana sana between countries.
 
WanaJF, nadhani wengi tunabisha ili kubisha na sio kingine. Huwezi kuwa na free market bila regulations. Lakini regulations ni lazima ziwe zenye kusupport ushindani. Tanzania kuna chama cha wenye mabasi ambacho kinakaa chini na kupanga bei ya nauli ambazo mabasi yote yatoze, lakini hakuna chama cha wananchi cha kuwapa wananchi nguvu ya kubargain.

Sasa ili force za pure demand and supply zitumike ni lazima tuondoe hii monopolization kama ya OPEC. Hapo ndio tutasema tuna free trade, huwezi kusema Tanzania tupo kwenye free trade wakati corporation zipo kwenye union.

Tupitishe sheria ambayo inavunjilia mbali hivi vyama mbali mbali vya wafanya biashara, maana vinapanga bei. Then baada ya hapo tunaweza kusema tunaachia nguvu za supply and demand zi determine price.
 

Mtanganyika nashukuru sana ndugu yangu.
On top,kuna walakini na elimu inayotolewa kwa vijana wetu.Angalia wengi waliotoa maoni hapo juu utaelewa kitu ambacho kila mara kimekuwa kero kubwa kwangu binafsi hasa kwenye hizi forums za mitandaoni.Ubishi usio na tija.
 
Australia ambayo ni nchi ya kibepari they have ACCC ( Australian Competition and Consumer Commision)

"The ACCC promotes competition and fair trade in the market place to benefit consumers, businesses and the community. It also regulates national infrastructure services. Its primary responsibility is to ensure that individuals and businesses comply with the Commonwealth competition, fair trading and consumer protection laws."


Unaweza kubofya hapa for more details: ACCC WEBSITE


Just a note, Nakumbuka wakati ule wa mafuriko kulikuwa kunatolewa matangazo ya kutopandisha bei za vitu na kwamba kufanya hivyo ni illegal!
 

This is my point na sio wananchi waanzishe bali serikali iwe na kitengo cha kuangalia Consumer protection na kiwe na meno ya kutosha kufikisha mtu mahakamani. Hilo litasaidia wafanyabiashara wasijipangie mabei kiholela. But guess what ni kina nani wafanyabiashara Tanzania? You will found out ni viongozi wenyewe hivyo basi inakuwa unawaambia wajiandalie moto wao wenyewe....
 

This my idea mkuu lakini wafanyabiasha ndio viongozi wenyewe sasa kwanza tuanze na kulifutilia mbali Azimio la Zanzibar na kutenganisha uongozi na biashara. Ndipo tufuatie hiki ama sivyo inakuwa tunatwanga maji kwenye kinu maana itapelekwa kisiasa mpaka watu wakate tamaa.
 

Umeifafanua vizuri sana Mtanganyika kwani inafika mahali Tanzania mteja anakubali kama kisima kukukaribisha ndoo yeyote safi, chafu, kubwa, ndogo, ya bati, yambao nk.. Mtumiaji Tanzania hana pahala pa kukimbilia kupeleka malalamiko yake ndio sababu kubwa bidhaa feki zina soko Tanzania kwakuwa bidhaa halisi hazinunuliki. Watu wanatembea kwa miguu au kudandia lifti Tanzania kwasababu mabasi yakipandisha nauli hakuna wa kuyapinga wala kuwazuia. Wauza mafuta Tanzania wanapata supernormal profit lakini watumiaji wanalalama chini kwa chini. Who is there in Tanzania to protect consumers? jibu hakuna.
 

Chapakazi,

Hujanielewa my point nikienda kumuuliza muuza duka kwanini pale Mlimani City anauza kiatu laki mbili na nusu wakati huko anapokinunua hadi hapa ni $60 the rest inaenda wapi anaweza kunieleza? Supply and Demand are forces of determining prices ila there has to be some form of regulatory mechanism kuhakikisha this does not go out of control. Mkisema free market iache tu kujitambua yenyewe unaweza kukuta suppliers (wauzaji kama hawa) wakaform a cartel wakapunguza usambazaji kwa nia ya kupandisha bei juu. Na hili ndio linalotokea kwasababu wauzaji wengine huwa wanafahamiana. Wateja wako scattered na hawawezi kuwa na umoja kutokana na kutofautiana in their purchasing power. Consumer protection agency ndio umoja wao inaweza kuangalia whether there is value for their money katika bei zinazopangwa. Kwasasa bei nyingi za tanzania ziko kwa kiwango cha kutisha na sio kila mtu anajua mahali kulipo na alternative option.
 

Hivyo basi,

Unataka kutuambia demand ikiongezeka tu wafanyabiashara wapandishe bei kwakuwa demand ni kubwa sana. Umezungumza bia kama bidhaa moja ya wapo ijapokuwa watu wanaendelea kunywa bia kwa shilingi 7,000 ila wateja wa nyama choma wamepungua umejiuliza kwanini? Vile vile wateja hao hao wa bia wamenunua bia kwa shilingi 7,000 ila chai asubuhi anaywia ofisini maana sukari bei imemshinda maana bei iko juu. Mtanzania leo hii anatembea kwa mguu kuanzia mwananyamala mpaka mjini kuepuka gharama ya nauli. Anatafuta hela ya jioni akapate moja moto moja baridi lakini ya kula hana je nikuulize hiyo 7,000 huoni kuwa inaaffect mustakbali wa maisha ya vitu vengine?

Turudi katika gharama za kile kiatu Tuseme analipa tax Tanzania tax ni 20% VAT, Mishahara na kodi unataka kutuambia hivyo vitu vinagharimu gharama za uzalishaji wa kiatu chenyewe? Maana kiatu kinatengenezwa $25 including VAT weka na gharama za usafirishaji unapata jumla ya gharama $60. Unataka kunieleza kodi ya VAT ya Tanzania, umeme na Corporation Tax na gharama za kuendesha duka zote jumla ni $159!!!! I do not think so. Tatizo Tanzania bei za vitu viko bei ya juu sana kulinganisha na hali halisi na sababu kuu ni kuwa wafanyabiashara wanataka faida kubwa.
 

Nadhani wewe ndio unahitaji kurudi darasani ukasome kwanza nini maana competition, fraud na price regulations.

Competition inajumuisha kuhakikisha market iko competitive na kuprevent unfair trading katika market. Na hilo linajumuisha both at domestic and international perspective kuhakikisha traders do not abuse or monopolise local markets. Tutajuaje kama wauzaji wa madukani na importers huungana katika kusetup prices for their own interest? Wafanyabiasha wengi hata machinga huwa wanafahamiana na wengine hukaa pamoja na kuzungumzia namna gani wakubaliane kupanga bei kwa manufaa ya kwamba wasipoteze wateja na kuhakikisha wanaendelea kupata faida kubwa. Swali ni nani anaweza kuwazuia hawa wasiwaumize wananchi wa kawaida jibu hakuna. FTC huwa inafanya kazi hiyo in US, in UK wana Office of Fair Trading, Federal Cartel office Ujerumani, Conseil de la concurrence France na kwengineko. Hebu soma Act hizi:-

Section 1. Every contract, combination in the form of trust or otherwise, or conspiracy, in restraint of trade or commerce among the several States, or with foreign nations, is declared to be illegal. Every person who shall make any contract or engage in any combination or conspiracy hereby declared to be illegal shall be deemed guilty of a felony, and, on conviction thereof, shall be punished by fine....

Section 2. Every person who shall monopolize, or attempt to monopolize, or combine or conspire with any other person or persons, to monopolize any part of the trade or commerce among the several States, or with foreign nations, shall be deemed guilty of a felony, and, on conviction thereof, shall be punished by fine...."

Hivyo basi ninapoenda kutaka kununua kiatu pale mlimani city nikakubali kukinunua inamaana tushatengeneza mkataba ambao unaendana na kuaminiana kuwa bei nayonunulia ni value for the money I am paying for. Ikiwa muuzaji amenidanganya au kuhadaa hiyo ni conspiracy na hivyo amepoteza uaminifu kwa mteja. He or she is subjected to civil lawsuit. Na hivyo basi muuzaji wa kiatu pale mlimani city anakuwa liable ikionekana amedanganya katika uuzaji wa vitu kwa bei isiyo halali kwa jamii.
 

A very useful reply
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…