Mbeya ni Dr Tulia na Dr Tulia ndio Mbeya. Huyo ndio chaguo la wana Mbeya,ndio Tumaini la wana Mbeya ,ndio hitaji la wana Mbeya,ndiye aliyepitishwa na mioyo ya wana Mbeya.Dr Tulia hana mpinzani wala wa kushindanishwa naye katika sanduku la kura Hakuna mwenye ubavu wa kumzuia wala kumkwamisha Dr Tulia Mbeya mjini.sauti za wana Mbeya zinapazwa na zinasikika zikiendelea kuhitaji utumishi wa Dr Tulia Mbeya mjini.
Kwa mambo makubwa na ya kuacha alama Mbeya mjini imefanya vijana kwa wazee kwa akina mama kuungana kwa pamoja kumuunga mkono Dr Tulia uchaguzi ujao.
Kwa kuwa ni uwepo na ushawishi wa Dr Tulia imepelekea kupelekwa mabilioni kwa mabilioni ya miradi ya maendeleo jiji la Mbeya na mkoa mzima wa Mbeya ,Ni kupitia yeye sasa zaidi ya Km 237.9 za barabara za njia nne zinakwenda kujengwa kuanzia Igawa mpaka Tunduma mkoani Songwe.
Ni kupitia Dr Tulia leo Mbeya inaheshimika na kupewa kila aina ya fursa ya maendeleo.ni kupitia Dr Tulia tumeona vijana , akina mama ,watu wenye ulemavu na makundi mengine mengi yakipewa na kuwezeshwa mitaji kwa ajili ya kufanya shughuli za kujipatia kipato.tumeona vijana wakipewa pikipiki pamoja na bajaji bure kabisaa kwa ajili ya kufanyia biashara na kujipatia fedha zinazowasaidia kuondokana na utegemezi wa kipato.
Ni kupitia uchapa kazi na nguvu ya Dr Tulia tunaona maonyesho ya nane nane mkoani Mbeya yakipewa heshima ya kipekee na kuhudhuriwa na viongozi wakuu wa Taifa letu. Tumeona namna mh Tulia anavyofanya kazi zilizogusa kila eneo ambalo ukienda lazima ukute mikono ya Dr Tulia.Tumeona majuzi hapa amewezesha shule ya sekondari Samora kujenga na kukamilisha mabweni ya wanafunzi wa kike yatakayochochea ufaulu na kuleta utulivu wajisomeapo.
Hakuna utakakokwenda usikute alama na mikono ya Dr Tulia,hakuna ambapo utakwenda usikute mchango wa Dr Tulia,hakuna ambako utapita usionyeshwe juhudi na kazi za Dr Tulia katika kuleta matumaini, Tabasamu,furaha na vicheko vya furaha kwa wanambeya. Ni Dr Tulia kila sehemu ni utulivu kila mahali na ni maendeleo kila eneo kutokana na maono makubwa na upendo mkubwa alio nao Dr Tulia kwa wana Mbeya na Mbeya nzima kwa ujumla wake.