PAYE
JF-Expert Member
- Jun 19, 2025
- 354
- 395
Januari 10, 2026, Mkurugenzi wa Taasisi ya Tulia Trust ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Uyole, Spika Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani(IPU) Mhe. Dkt. Tulia Ackson amegawa vifaa vya shule kwa wanafunzi wenye uhitaji Jimbo la Uyole.
Dkt. Tulia anatoa msaada wa Sare za Shule na Daftari kwa Wanafunzi Elfu Tatu (3,000) wenye uhitaji zaidi kutoka kata 13 za Jimbo la Uyole ikiwa ni muendelezo wake wa kuwasaidia watoto wasio jiweza kipindi cha kufungua shule kwa kutoa msaada huo.
Aidha, Dkt. Tulia amewataka wazazi na walimu kuwa mstari wa mbele kuhakikisha na kusimamia watoto wanakwenda shule na wanapata Elimu bora kwani kufaulu kwa wanafunzi inategemea na walimu na wazazi kwa pamoja kutia bidii katika kuyatekeleza hayo.
Amemaliza Dkt. Tulia kwa kumshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa uwekezaji wake katika sekta ya elimu haswa kwenye miundombinu, Serikali ya awamu ya sita imefanikiwa kujenga shule, madarasa na kuboresha miundombinu mingine mashuleni kitendo kitakachopelekea Elimu kukua kwa kasi zaidi na kushawishi wanafunzi kufanya vizuri zaidi.