Haya mambo yalimshinda Marmo alipotaka kuyaibua ktk bunge lililopita ila sasa naona jamaa wamebanwa ktk kona mbaya.
Ila nilichojifunza hapa ni kwamba SERIKALI inaficha maradhi yaani hizo siri zinazotakiwa kufichwa ni WIZI MTUPU. mikataba feki, vijimemo vya wizi kule hazina na taka taka zinginezo.
Mmbona hakuna nyaraka hata moja inayonyumbua masuala ya ulinzi na usalama mbayo imewekwa hewani au peupe? Serikali na wadau wake watambue kuwa wao ni watanzania kama sisi na nchi ni yetu wanachi hivyo kama kuna mambo zanayogusa maslahi ya taifa yanafanyika gizani basi hiyo ni dalili ya UHAINI ambao sasa unawatokea puani.
Wakati umefika kwa Tanzania kuwa na wabunge wa kujitolea badala ya kuwa na wawakilishi wanaokwenda bungeni kuchuma. Wabunge wamefikia hatua ya kumnyanyasa Dr Slaa ati kwa sababu kasema ukweli kuwa analipwa mishahara mikubwa, wanataka iwe siri yao. Inatosha, tupate wabunge wa kujitolea ambao kweli watakuwa wanatetea maslahi ya wananchi badala ya kuganga njaa zao na kujitarisha. Mnaonaje wana JF?
....Wabunge watatu wa CCM, Bw. Lazaro Nyalandu (Singida Kaskazini), Bw. Ponsiano Nyami (Nkasi) na Bw. George Simbachawene (Kibakwe) walisema wanaungana na Serikali na kwamba hatua ya kutoa onyo imechelewa kwa maelezo kwamba tayari tabia hiyo imeiletea nchi dosari kubwa mbele ya Mataifa mengine ya nje.
"Kwanza kabisa Serikali imechelewa kuchukua hatua na hata hivyo hatutarajii kuona akiachwa hivi hivi. Tunataka Serikali imchukulie hatua za kisheria haraka aliyekwishahusika na hilo kosa, tayari tumepata athari watu wa nje wanatuona kama watu waliochanganyikiwa," alidai Bw. Nyami akiungwa mkono na wenzake wawili.
Naye Bw. Simbachawene alisema amesikitishwa na hali hiyo na kueleza kwamba chanzo cha tatizo hilo ni hulka ya Watanzania ya kuvumiliana, busara na hekima inayotumiwa na viongozi kutoharakisha kuwachukulia watu hatua wakitaka Watanzania waendelee kuishi kwa amani na utulivu na kuamini kwamba kila mtu akitambua hilo hawezi kufanya kile kilichofanywa na baadhi ya Wabunge kutoa siri za Serikali hadharani.
"Kinachofanywa na Dkt. Slaa ni kutaka kuichanganya Serikali kwa ujumla ili ifikie wakati wananchi wakose imani na Serikali yao jambo ambalo ni hatari sana kwa Taifa. Anataka kutufanya kama watu wote waliochanganyikiwa, hatuwezi kukubali, Mbunge ana njia nyingi za kuishauri Serikali si kutoa siri za nchi tena kwenye mkutano wa hadhara," alidai Mbunge huyo.
Naye Bw. Nyalandu alidai Mbunge kuweka hadharani nyaraka za siri za Serikali katika mkutano wa hadhara ni aibu kwa Taifa kubwa na lenye sifa
njema kama Tanzania na kwamba haliwezi kuvumiliwa.
Kwa upande wake Mbunge wa Bumbuli (CCM), Bw. William Shellukindo alisema kitaratibu zipo nyaraka za Serikali ambazo haziwezi kuwa wazi hadi kufikia kipindi cha miaka 20 au zaidi na kwamba ikibainika umezitoa unaweza kuchukuliwa hatua kali hivyo anaungana na Serikali kuhusu onyo hilo.
"Mimi nimefanya kazi Serikalini muda mrefu, zipo nyaraka za siri ambazo haziwezi kuwa hadharani mpaka miaka 20 ya muda fulani, ukibainika umezitoa unastahili kuchukuliwa hatua za kisheria. Naungana na Serikali kabisa," alisema Mbunge huyo ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Nishati na Madini.
..........SOURCE: MAJIRA
Jibaba BongeWananchi wa majimbo ya wabunge hawa mnataka nini tena?! Mmeshajua aina wa wabunge mlio nao. mnafikiri wanawajali hawa? 2010 hawatakiwi kuendelea na ubunge hawa. Wao wanashughulikia matumbo yao tu- kupitisha nyongeza za ajabu za mishahara yao tu huku walimu, mapolisi na walala hoi wengine wakikosa hata mlo wa siku!? kweli tunawahitaji wabunge wa namna hii?
Hivi kutoa uthibitisho wa EPA, RADA, Twin towers na ufisadi mwingi mwingine ni kutoa siri za serikali? BASI BUNGE LINATAKIWA LIBADILISHE SHERIA INAYOWABANA WABUNGE KUTOA HOJA ZA KWELI NA ZENYE VITHIBITISHO. Mbunge atakapo toa vithibitisho kuhusu hoja inayoihusu serikali kwa vyovyote hivyo vithibitisho vitakuwa nyaraka za serikali na pengine za siri.
Serikali iache kutuzingua hapa - kama hutaki moshi uonekane nje basi usiwashe moto mnasema siri za serikali huku zinahusu kuhamisha fedha za walala hoi kwenda kwa mafisadi na ccm. wizi mtupu!
Herbert,Huu mkuu ni ukweli usiofichika.
Naona pale wanakula per deam tu. Hata hoja wanazoziridhia sidhani kama sinapitiwa kwa undani. Maswali yanayoonyesha kwamba wabunge wanaaply crirical thinking hamna kabisa.
Bunge letu Michosho sana.
Herbert,
Ulichosema ni sahihi kabisa. Juzi mimi na wenzangu wachache tulifanya utafiti mdogo ndani ya Ukumbi wakati wa Bunge zima. Tumegundua kitu cha ajabu sana, na tusipoangalia kitapeleka nchi shimoni kabisa. Kati ya Wabunge 150 waliokuwa ukumbini, ni wabunge wasiozidi 30 walikuwa na Mswada. Wengine wote, na hasa waliokuwa wanapaza sauti kusema "Ndiyo" kupitisha vifungu walikuwa hawana kabisa vitabu, na hivyo ni vigumu kuamini kuwa walikuwa wanafahamu vifungu vyote vilivyokuwa vikipitishwa. Kilichoonekana au ni kupitisha vifungu na muda upite, au kuvipitisha kwa vile mswada umeletwa na Serikali yao. Kwa vile Bunge liko live siku hizi, ni vema waandishi wa Habari walioko kwenye JF nao pia watusaidie. Inawezekana siri ya nchi yetu kupitisha Sheria zisizo na maslahi kwa wananchi, au zinazokinzana ni kutokana na hali hii ya Wabunge kutokusoma miswada inayowasilishwa Bungeni na kuzipitisha kimzaha mzaha tu. Nimestuka sana na hali hii, na hiwezi kuachwa bila kukemewa. Tusaidiane kufanya utafiti ili tuweze kuikemea vizuri. Mapenzi kwa nchi, yanaanzia kwa kutunga sheria nzuri. Sheria nzuri hutungwa na wabunge makini.