GE2025 Dkt. Mwinyi aahidi kuwapa Wajasiriamali wadogo mikopo na mitaji midogo Zanzibar

GE2025 Dkt. Mwinyi aahidi kuwapa Wajasiriamali wadogo mikopo na mitaji midogo Zanzibar

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

PAYE

JF-Expert Member
Joined
Jun 19, 2025
Posts
354
Reaction score
395
Mgombea wa nafasi ya Urais wa Zanzibar kupitia tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dkt. Hussein Ali Mwinyi, amesema katika kipindi cha miaka mitano ijayo atahakikisha anawafikia wajasiriamali wadogo mahala walipo kwa kuwapatia mitaji midogo.

1760078624122.png

Kauli hiyo ameitoa wakati akizungumza na wajasiriamali wadogo katika ukumbi wa Idrisa Abdul Wakil uliopo wilaya ya Mjini mkoa wa Mjini Magharibi.

“Tutawafikia wajasiriamali hao wadogo kwa wanaohitaji mitaji ya TSh. 300,000 hadi TSh.500,000 tutawafikia walipo ili tuwape mitaji hiyo lakini kwa wale wajasiriamali wa kati ambao tayari wanausajiri ambao tayari wana akaunti za benki tutahakikisha wanapatiwa mikopo,” amesema

Dkt. Mwinyi amesema serikali itaendelea kuweka mafungu makubwa ya kukopesha bila ya riba kama ilivyofanyika kipindi kilichopita na kwamba safari hii itafanywa kwa kuyatambua nani anayeweza kusajiriwa nani asiyeweza kusajiriwa.

Mbali na hilo, Dkt. Mwinyi amesema katika kipindi kijacho atahakikisha anajenga mazingira mazuri ya wajasiriamali wadogo ya kufanyiabiashara.

“Hilo ni moja ya dhamira yangu nikirudi madarakani tutahakikisha tunajenga mazingira mazuri,”amesema
 
Dkt. Mwinyi amesema serikali itaendelea kuweka mafungu makubwa ya kukopesha bila ya riba kama ilivyofanyika kipindi kilichopita
Pesa ya Tanganyika,
Ila Watanganyika hawapewi hizo fursa
 
Back
Top Bottom