PreGE2025 Dkt. Mpango: Watu waepuke kauli za kichochezi mitandaoni

PreGE2025 Dkt. Mpango: Watu waepuke kauli za kichochezi mitandaoni

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
4,397
Reaction score
14,503
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Mpango amesema Serikali inalaani vikali na kukemea tukio la kushambuliwa na kuumizwa Katibu Mkuu wa Baraza la Maaskofu Tanzania (TEC) Padre Dkt. Charles Kitima pamoja na matukio mengine kama hayo ya uvunjifu wa sheria.

IMG_4621.jpeg

Makamu wa Rais amesema hayo wakati aliposhiriki katika Misa ya Kumsimika Askofu wa Jimbo Jipya Katoliki la Bagamoyo Mhashamu Askofu Stephano Lameck Musomba pamoja na Sherehe ya Uzinduzi wa Jimbo hilo iliyofanyika katika Uwanja wa St. Mary Wilayani Bagamoyo Mkoani Pwani ambapo amewahakikishia Watanzania na wapenda haki, amani na usalama, kuwa tayari Serikali kupitia Wizara ya Mambo ya Ndani imeviagiza vyombo vya dola kuwatafuta, kuwakamata na kuwachukulia hatua kali za kisheria wahusika wa tukio hilo, na wale wote watakaothibitika kuhusika na matukio kama hayo.

Makamu wa Rais amesisitiza pia umuhimu wa kudumisha amani na utulivu wakati wote wa maandalizi na kampeni za uchaguzi mkuu na amesema ni vema kuepuka kauli za kibaguzi, kichochezi, uzushi na upotoshaji kupitia mitandao ya kijamii na njia nyingine za mawasiliano kwa misingi ya tofauti ya itikadi za kisiasa, kidini, kabila au rangi.

Makamu wa Rais pia amewaasa Vijana kutokubali kutumiwa na Wanasiasa wenye uchu wa madaraka, walio tayari kuwatumia kuchochea vurugu wakati wa uchaguzi kwa manufaa yao wenyewe.
 
Amwambie Amos makala kwanza.
Kisha amalizie na RC wa DAR
 
Back
Top Bottom