Dkt. Kisenge: Ukivuta shisha moja sawa na sigara 100

Mkalukungone Mwamba

JF-Expert Member
Joined
Aug 29, 2022
Posts
2,450
Reaction score
5,279
Wavuta shisha habari iwafikie
===========
Aprili 1, 2026 Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI), Dkt. Peter Kisenge, amesema kuwa matumizi ya tumbaku yanaendelea kuwa chanzo kikubwa cha magonjwa ya moyo, yakisababisha vifo vya takribani watu milioni 20 duniani.

Akizungumza leo jijini Dar es Salaam wakati wa uzinduzi wa ripoti ya Tobacco Industry Interference Index 2025, Dkt. Kisenge alieleza kuwa uvutaji wa sigara na shisha unaathiri vibaya afya ya moyo, mishipa ya damu, mapafu pamoja na kuongeza hatari ya kiharusi.

Soma Pia: Dkt. Peter Kisenge: Unywaji wa pombe uliokithiri unachangia magonjwa ya moyo

Alifafanua kuwa kuvuta shisha moja ni sawa na kuvuta sigara 100, hali inayoongeza uwezekano wa mgando wa damu kwenye mishipa ya moyo. Aidha, alibainisha kuwa magonjwa yasiyoambukiza kama shinikizo la damu na kisukari yanaongezeka kwa kasi nchini Tanzania, huku matumizi ya tumbaku yakichangia kwa kiasi kikubwa hali hiyo.

Bora bangi haijatajwa,woooiii sema halla Kwa bangi🔥🔥🔥🔥🔥🔥
 
Tafiti za kisenge hizi huwa zinavutia sana
 
Back
Top Bottom