Dkt. Kigwangala fanyia kazi mapungufu yako haya

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Jul 13, 2013
56,516
108,793
Nimekuwa nikikufuatilia sana tokea ulipoamua kujikita katika siasa badala ya kuendelea kutibu watu au kutoa huduma za kiafya kama fani yako uliyoisomea. Navutiwa mno na harakati zako za kisiasa unazozifanya kama kijana japo nikiri kuwa hujaweza kumfikia mwanasiasa kijana mwenzio Zitto Kabwe.

Pia mheshimiwa nilivutiwa mno na zile sera zako wakati na wewe ulipojitutumua kugombea urais mwaka jana japo nina uhakika kuwa nyingi ya zile sera zako hazikuwa applicable kwa nchi yetu kutokana na sababu za kimazingira na za kimkakati na ni kama vile ulikuwa unajifurahisha tu na angalau sera za mwenzako Mwigulu Nchemba zilikuwa na mashiko japo aliyewashindeni nyote alikuwa ni january makamba kwani sera zake zilikuwa zimetukuka.

Huo ulikuwa ni utangulizi tu ila kama kawaida yangu sipendi kupepesa au kutikisa naomba leo niseme ukweli kuwa tokea uchaguliwe kuwa katika hiyo nafasi ya naibu waziri wa hizo wizara husika kuna vijitabia ambavyo nahisi labda ni hulka yako na unavyo au umeviubua tu ambavyo kama mimi naona usipoviacha mapema vinaweza vikakupoteza kisiasa au ukaonekana ndivyo sivyo kwa jamii au wanaokutazama na pengine kutaka kujifunza kutoka kwako.

Mheshimiwa tokea uteuliwe umekuwa na haya yafuatayo:

  1. Unapenda sana kukurupuka katika shughuli zako.

  2. Unapenda mno attentionhata pasipohitajika.

  3. Umekuwa ni mtu mwenye hasira na hata sura yako inathibitisha hilo.

  4. Umekuwa ni mtu mwenye nyodo na dharau ambazo zimetukuka.

  5. Unaonekana ni mtu unayetaka kumfunika bosi wako kiutendaji.

  6. Acha kujiamini kupita kiasi kwani tunaokujua tunajua kuwa upo vizuri ila unazidisha.

  7. Unaubabe sana mkuu wakati kwa nafasi uliyonayo busara na hekima ndiyo kipaumbele.

    Fanyia kazi hayo mkuu na nakuhakikishia huko mbele utakuja kuwa bonge la kiongozi kwani unaonekana una uwezo mkubwa na mzuri tu wa kuwa hata rais au waziri mkuu huko mbele na usiyachukulie haya kama labda nina chuki binafsi nawe bali jua kwamba binafsi nakukubali kunakotukuka na sitaki upotee.

Akhsante!
 
..teh.! Ushauri mzuri, ila kama ungetolea mfano wa HOJA zako kwa kile alichokifanya toka amepewa nafasi aliyonayo,ingenoga zaidi.All in all,umetoa Ushauri mzuri.JAPOKUWA hayo yote yanawezekana zaidi iawapo mtu anakua na HOFU ya Mungu,mtu asipokuwa na HOFU ya Mungu ni vigumu kubadili tabia na hulka yake.!
 
....

..... "Mukulu" ulimbukeni ni sehemu ya ugonjwa !!!

big remerciements .....
 
Anapretend kuwa yupo serious sana..!na hakika asipoyafanyia kazi atapotea kwenye ramani ya siasa
 
Nimekuwa nikikufuatilia sana tokea ulipoamua kujikita katika siasa badala ya kuendelea kutibu watu au kutoa huduma za kiafya kama fani yako uliyoisomea. Navutiwa mno na harakati zako za kisiasa unazozifanya kama kijana japo nikiri kuwa hujaweza kumfikia mwanasiasa kijana mwenzio Zitto Kabwe.

Pia mheshimiwa nilivutiwa mno na zile sera zako wakati na wewe ulipojitutumua kugombea urais mwaka jana japo nina uhakika kuwa nyingi ya zile sera zako hazikuwa applicable kwa nchi yetu kutokana na sababu za kimazingira na za kimkakati na ni kama vile ulikuwa unajifurahisha tu na angalau sera za mwenzako Mwigulu Nchemba zilikuwa na mashiko japo aliyewashindeni nyote alikuwa ni january makamba kwani sera zake zilikuwa zimetukuka.

Huo ulikuwa ni utangulizi tu ila kama kawaida yangu sipendi kupepesa au kutikisa naomba leo niseme ukweli kuwa tokea uchaguliwe kuwa katika hiyo nafasi ya naibu waziri wa hizo wizara husika kuna vijitabia ambavyo nahisi labda ni hulka yako na unavyo au umeviubua tu ambavyo kama mimi naona usipoviacha mapema vinaweza vikakupoteza kisiasa au ukaonekana ndivyo sivyo kwa jamii au wanaokutazama na pengine kutaka kujifunza kutoka kwako.

Mheshimiwa tokea uteuliwe umekuwa na haya yafuatayo:

  1. Unapenda sana kukurupuka katika shughuli zako.

  2. Unapenda mno attentionhata pasipohitajika.

  3. Umekuwa ni mtu mwenye hasira na hata sura yako inathibitisha hilo.

  4. Umekuwa ni mtu mwenye nyodo na dharau ambazo zimetukuka.

  5. Unaonekana ni mtu unayetaka kumfunika bosi wako kiutendaji.

  6. Acha kujiamini kupita kiasi kwani tunaokujua tunajua kuwa upo vizuri ila unazidisha.

  7. Unaubabe sana mkuu wakati kwa nafasi uliyonayo busara na hekima ndiyo kipaumbele.

    Fanyia kazi hayo mkuu na nakuhakikishia huko mbele utakuja kuwa bonge la kiongozi kwani unaonekana una uwezo mkubwa na mzuri tu wa kuwa hata rais au waziri mkuu huko mbele na usiyachukulie haya kama labda nina chuki binafsi nawe bali jua kwamba binafsi nakukubali kunakotukuka na sitaki upotee.

Akhsante!
Kigwangallah ni Leo/ Simba kinyota! Ulioyazungumza yanaweza kuwa ni nature ya watu wa nyota husika japo si yote! Mbona mimi ni Leo na nina wadhifa kulingana na mazingira nilipo lakini niko humble! Kuna vitu anatakiwa apunguze..hasa attention! Najua atapita hapa "mate" wangu huyu!
 
naona kuchafuana huku, kati ya mawaziri makini huyu ni mmoja wao, sema tatizo ni kwamba anapenda sana media
 
ahahahhaha.....rais wetu ajayeeee. kuweni makini na comments zenu yasijekuwakuta yaliyomkuta dr. mwaka. nyie haya nyieeee...shauri yenu.
 
Back
Top Bottom