Dkt. John Joseph Pombe Magufuli aandika historia ya aina yake

JOYOPAPASI

JF-Expert Member
Jan 10, 2016
250
408
Napenda niungane na Mamilioni ya Wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Watanzania kwa ujumla kumpongeza Mwenyekiti CCM Taifa na Rais wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kuandika historia ya aina yake kwenye mkutano Mkuu wa CCM Taifa uliofanyika leo Julai 11, 2020 mjini Dodoma.

Kwanza, Dkt. Magufuli amethibitishwa kwa kupigwa kura ya ndio na Wajumbe 1822 wote sawa na asilimia 100 kupeperusha bendera ya CCM kugombea urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwenye uchaguzi Mkuu wa mwaka huu utakaofanyika mwezi Oktoba, 2020.

Haijawahi kutokea katika historia ya miaka yote ndani ya CCM Mgombea kwa nafasi ya Urais kupitishwa kwa asilimia 100. Mwaka 2015 Dkt. Magufuli alipitishwa kwa asilimia 87. Ongezeko hili ni ishara ya kubaliko la uadilifu, uzalendo, ufuatiliaji, uchapa kazi, ukweli na ucha Mungu alionao Dk. Magufuli kiuongozi.

Pili, Dk. Magufuli akiwa Mwenyekiti wa Kikao amewadhihirishia Watanzania na Dunia kwa ujumla juu ya Demokrasia iliyokomaa, uwazi na Uhuru wa uchaguzi ndani ya CCM kwa kura kupigwa wazi wazi na kuhesabiwa wazi wazi tena ikionyeshwa mubashara (live) na vyombo vya habari. Hii rekodi ameivunja na haijawahi kutokea katika historia ya Miaka yote ya chaguzi za CCM kwenye nafasi ya kumpata Mgombea Urais.

Hakika, Dk. Magufuli alivyosema uchaguzi wa mwaka huu atahakikisha unakuwa wa huru na haki alimaanisha na anaonyesha kivitendo kuanzia ndani nyumbani kwake (CCM).

Narudia tena kusema historia aliyoiandika Dkt. Magufuli ni ya aina yake inayompambanua kivitendo kuwa Mwamba na mkufunzi wa Dunia juu ya siasa safi, Demokrasia ya kweli na Uhuru wa uchaguzi.

Mungu Ibariki Tanzania
Mungu Ibariki CCM
Mungu Mbariki Dk. Magufuli.
20200711_125041.jpg
 
eti kaweka histori na kuonesha demokrasia iliyo komaa hahahaha

utaratibu wa upigaji kura umekiuka misingi ya demokrasia kwa sababu

1. upigaji kura ulikuwa wa wazi na haukuwa na siri (lengo ilikuwa kuwatafuta watakao weka alama ya hapana washughulikiwe)

2. kutenga maboksi ya kura kimikoa ilikuwa janja ya pili kuwatafuta watakao sema hapana washughulikiwe

3.baadhi ya wajumbe walionekana kupigiana kura ili hali anayepigiwa kwa niaba ni mzima na haoneshi ulemavu wowote hadi kuhitaji usaidizi wa kupigiwa kura.

4.wajumbe 1822 kufanana akili,mawazo na mtazamo ni ajabu kuna mawili hao wajumbe hawafikirii sawa sawa ama kuna nguvu flani imewabana.yaani chama kinachoongoza kwa kuwa na mbumbumbu isiharibike kura hata 1

NB: aruhusu uchaguzi huru aone kama iyo historia aivunjwi kwa kuwa raisi wa muhura mmoja tu.
 
Hivi wewe unaamini kabisa kwamba wajumbe wote 1822 wamepiga kura ya ndio kwa jiwe?!
 
Hivi wewe unaamini kabisa kwamba wajumbe wote 1822 wamepiga kura ya ndio kwa jiwe?!
Mkuu Ukiambiwa uthibitishe kuwa kuna baadhi ya wajumbe hawakumpigia kura JPM utaweza?

Huyu kaandika hivyo kwa kuwa vyombo na vyanzo vyote vya habari vimeandika kuwa JPM kapata kura zote 1822,lakini pia msimamizi wa kura kasoma hivyo hivyo,kwahiyo tukuamini wewe au tuamini aliyesimamia mchakato wa kura?

Ninyi watu huwa mnakwama wapi?


Sent from my TECNO KB7j using JamiiForums mobile app
 
Mkuu Ukiambiwa uthibitishe kuwa kuna baadhi ya wajumbe hawakumpigia kura JPM utaweza?

Huyu kaandika hivyo kwa kuwa vyombo na vyanzo vyote vya habari vimeandika kuwa JPM kapata kura zote 1822,lakini pia msimamizi wa kura kasoma hivyo hivyo,kwahiyo tukuamini wewe au tuamini aliyesimamia mchakato wa kura?

Ninyi watu huwa mnakwama wapi?


Sent from my TECNO KB7j using JamiiForums mobile app
Ni yale yale ya kesi za corona kubaki 509 tangu March hadi sasa, wewe unaamini hivyo?
 
Sasa mbona mlimzuia Membe asichukue fomu ili achuane na Mwenyekiti!! Si mngemruhusu aje adhalilishwe kwenye huo mkutano na Mwenyekiti wenu wa chama kwa kupata kura yake moja tu huku Mwenyekiti akishinda kwa 99.9% ya kura zote!!
 
Sawa, kama "Yesu" wenu anakubalika sana kiasi hicho mapolisi dhidi ya wapinzani wa nini sasa?

Si awaache tu wapinzani wakaaibike wenyewe huko kwa wananchi ambao wana mahaba na huyo "yesu"?
 
Back
Top Bottom