Dkt. Doto Biteko ndiye Waziri Mkuu ajaye kuanzia 2025 - 2030

Kwa jicho la kiuchambuzi kwa mbalii sana namuona Dotto Mashaka Biteko akiwa Waziri Mkuu katika serikali ya awamu ya 6 kipindi cha pili chini ya Rais Samia Suluhu Hassan. Mh. Kassim Majaliwa atahitimisha kipindi chake cha miaka 10 mwaka 2025 na huo ndio utakua mwisho wake kisiasa katika nafasi za uongozi wa juu katika nchi hii.

Sababu ni hizi zifuatazo:

1. Atakua ameshatumikia miaka 10 kama ilivyo desturi ya mawaziri wakuu aliyeshika zaidi ya miaka 10 ni Mwl. Julius Nyerere pekee wengine ni chini ya hapo au 10 net.

2. Kasi ya utendaji wake kwa sasa hairidhishi ni kama ameshachoka kuongoza au ana tatizo la kiafya hivyo anahitaji kupumzika na pia inawezekana kabisa yeye mwenyewe binafsi ameshauriana na Mh. Rais atafutiwe msaidizi wa majukumu aliyonayo ndio maana akateuliwa Dotto kama naibu wa Waziri Mkuu.

3. Kutokana na siasa za Upinzani za mwaka 2025 na hasa ukizingatia Mh. Rais ameruhusu utawala wa kidemokrasia tutegemee kuwepo kwa makundi ya vyama vya upinzani yatakayojaribu kuwania urais hivyo kuleta ushindani kwa Mgombea wa chama tawala Mama Samia Suluhu Hassan hivyo uteuzi wa Dotto Mashaka Biteko umechukuliwa kama " counter offensive " kwaajili ya mwaka 2025 wote tunajuwa ukanda wa lake zones kuna wapiga kura wa kutosha na CHADEMA wameweka kambi mikoa hiyo ili kujaribu bahati yao.

Sababu kuu hizi tatu zinanishawishi kwa kiasi kikubwa sana kuamini Doto Mashaka Biteko ndio Waziri Mkuu anaekuja mwaka 2025.

Kila la heri kijana unaonekana upo smart naomba uiangalie EWURA kwa jicho la karibu sana wananchi tunaumia na bei za mafuta wafanyabiashara wanatamba kuiweka serikali mfukoni.

Onesha uwezo wako mama keshawapa rungu siyo mpaka msubiri maelekezo kutoka juu. Mwenzako kipara kalewa posho kasahau shida za wananchi.
Ikitokea hivyo basi pongezi nyingi sana itabidi zimwendee Mh. Job Ndugai

Mh. Biteko alianza kuwa nurtured kipindi cha Ndugai, nadhani baada ya Ndugai kumuona kuwa alikuwa ana sifa hizo

Kwa mara ya kwanza Mh. Biteko alianza kusikika vizuri sana kwenye ile kamati ya Almasi au tanzanite iliyoundwa na Mh. Ndugai, wakati wa kipindi cha JPM (RIP)

Kamati hiyo ilikuwa chini ya Mh. Biteko na baada ya kuwasilisha ripoti yake, nasikia hadi JPM alimuuliza Ndugai akisema huyu kijana ulimpata wapi?
 
Mbona mnazungumzia Nyanza tu ya enzi hizo mnasahau SHIREKU ya shinyanga! ya akina Paulo Ng'wani nayo ilifanya kazi sana na ushirika uliisha hapo.
Ila Ukimwi uliwafagia wafanyakazi wa Shirecu kama vumbi linavyofagiliwa.
 
Unataka kutuaminisha kwamba 2025 hakuna haja ya uchaguzi kwa kuwa Samia tayari ni raisi hadi 2030? Je, wananchi wasipomchagua ataendelea kuwa raisi? Hivi ninyi watu kiburi cha shetani mnaking'ang'ania cha nini? Hamjifunzi tu.
Wananchi kwa maendeleo haya hatuna sababu ya kuacha kumchagua. Kwenye chama tayari kapitishwa au unaota Tundu lissu wa chadema ndio atachuguliwa?
 
Rais hakuwahi kufia madarakani,hii ni Awamu ya 5, Rais wa SITA.

Aliyepo hakupigiwa kura, hivyo wanachama wataruhusiwa kuchukua FOMU,

Ndo ujue, HATOGOMBEA!!
Sisi tumeshamaliza Huku CCM au ushasahau kikao cha mkutano mkuu wa Taifa JK aliongea nini? Samia hana mpinzani nje wala ndani ya CCM jiandae kisaikolojia usije ukafa kwa presha bure .
 
Ikitokea hivyo basi pongezi nyingi sana itabidi zimwendee Mh. Job Ndugai

Mh. Biteko alianza kuwa nurtured kipindi cha Ndugai, nadhani baada ya Ndugai kumuona kuwa alikuwa ana sifa hizo

Kwa mara ya kwanza Mh. Biteko alianza kusikika vizuri sana kwenye ile kamati ya Almasi au tanzanite iliyoundwa na Mh. Ndugai, wakati wa kipindi cha JPM (RIP)

Kamati hiyo ilikuwa chini ya Mh. Biteko na baada ya kuwasilisha ripoti yake, nasikia hadi JPM alimuuliza Ndugai akisema huyu kijana ulimpata wapi?
Jamaa yupo vizuri.
 
Natabiri ccm kuparanganyika endapo ccm watalazimisha samia kugombea na kuwazuia wengine kuchukua form.
Hilo unalowaza siyo geni umesahau 2015 lowasa na genge lake walifanyaje? CCM ni kisima kirefu sana wapo watu wanaojua kudeal na wahuni wanaotaka kuvuruga chama hivyo hizo ndoto zako hazitafanikiwa.
 
Hilo unalowaza siyo geni umesahau 2015 lowasa na genge lake walifanyaje? CCM ni kisima kirefu sana wapo watu wanaojua kudeal na wahuni wanaotaka kuvuruga chama hivyo hizo ndoto zako hazitafanikiwa.
Wakati wa Lowasa tuliwekwa dilemma baada ya chama kumkata Lowasa na kutuletea chuma kingine Magufuli mzalendo, mlinzi wa maliasili za taifa, tukasema hamna shida kwa maana Magu alionyesha uhodari wake toka kwenye uwaziri wa ujenzi. Lakini kwa huyu mama ni tofauti sana. Kweli anayo mazuri yake mengi tu, lakini kadiri anavyojitahidi kutenda mema watanganyika hawamwelewi kabisa. Bora hata 2025 akagombea majaliwa pamoja na fix zake kuliko mama. Huo ndio ukweli.
 
Back
Top Bottom