Dkt. Biteko: Madini ya ruby yaliyoko Dubai wamiliki waliyapata miaka 11 iliyopita

Ngao ya Sponji

JF-Expert Member
Jul 26, 2018
341
541
Dodoma. Wakati kukiwa na utata kuhusu jiwe la madini ya rubi linalotarajia kuingia sokoni nchini Dubai, Waziri wa Madini, Dk Dotto Biteko amesema ukweli unataka kufichwa kuhusu jiwe hilo.

Dk Biteko amesema tayari kuna watu wametangaza kuwa ikiwa Tanzania itakubali kuwa jiwe hilo linatoka kwake, itapewa mgawo wa dola 20 milioni.

Waziri wa Madini, Dk Dotto Biteko ametoa kauli hiyo leo Aprili 23 jijini Dodoma alipokuwa akizungumza kwenye semina ya madini kwa wabunge wanawake.

Amesema mazungumzo yameendelea mmiliki wa jiwe hilo ambaye ni raia wa Marekani, wakimtaka atoe cheti halali cha namna gani alilipata jiwe hilo na kulisafirisha baada ya kupitia nyaraka zote na kubaini kuwa hakuna taarifa inayoonyesha kuwa kuna madini yaliyosafirishwa.

Amesema walileta kwa Serikali cheti cha GIA ya Marekani ambayo ilionekana kuwa na upungufu kwani jiwe limetangazwa kuwa na kilo 2.8 lakini yenyewe imeonyesha kuwa na kilo 3.4.

“Baada ya kuona hivyo, tuliwaambia mbona hii inatokana Marekani, tupeni ya kutoka Tanzania, jana tukakubaliana kukutana watu wa Dubai, Marekani na Tanzania.

“Lakini ilipofika mchana wakasema siyo hilo tu tunayo na mawe mengine 12 yanayotoka Tanzania wakisema kuwa waliyapata miaka 11 iliyopita,” amesema Waziri Biteko.

Ameendelea; “Leo asubuhi tulipowaambia kuwa tunataka kufanya press (mkutano wa wanahabari) wakasema wanayo mawe 25 yenye uzito tofauti, sasa naomba tuwe watulivu hamuwezi kujua nini maana yake,” amesema Dk Biteko.

Kwa nyakati tofauti wabunge hao walitaka ukweli wa mambo ujulikane ni kwa nini jiwe hilo linafichwa na kuhoji ni namna gani lilitoroshwa Tanzania.

Madai kuhusu jiwe hilo la rubi lenye uzito wa kilo 2.8 ambalo linatajwa kuwa litaingia sokoni kuuzwa siku 30 baada ya mfumo wa mwezi mtukufu wa Ramadhan, kwam mara ya kwanza yaliibuliwa bungeni na mbunge wa Mkinga Dustan Kitandula April 21, 2022.

Mbunge huyo aliomba kufahamu kuhusu uvumi wa taarifa za mitandao kuwa jiwe hilo kubwa lenye thamani dola 120 milioni (Sh240 bilioni) na akahoji iwapo kuna ukweli wowote kuhusu jiwe hilo ni namna gani Watanzania walinufaika na kodi yake.

Akijibu swali hilo, Naibu Waziri wa Madini Dk Stephen Kiruswa alisema Serikali ilipata taarifa za uwapo wa jiwe hilo tangu Aprili 13, 2022 na kwamba ilifanya mawasiliano na Ubalozi wake Dubai na ndipo katika kufuatilia, wakabaini kuwa mmiliki wake anatoka Marekani katika mji wa California.

Chanzo: Mwananchi
 
Hivi ndivyo uwa wanasafirisha mali zetu wala hatunaga habari.
Haya ni machache kati ya mengi yanayotokea
 
Winza panajulikana ni Kata ya Kibakwe wazungu walikuja kwa kupitia Ruaha, Choghola na hawakutaka kujulikana mwisho mgodi ukachukuliwa na mtoto wa raia kwa kipindi kile alafu ikapigwa as where ndefu so wizi ulifanyika kitambo Mimi nilikuwa mwana appolo bythen Ila madini yapo maeneo yote ya Kinusi, Matonya, Ugewa, Lumuma, Galigali na Mbuga na niseme tu kuwa kule wale wahehe hawana nongwa ingekuwa Mara au Arusha wangeuwana ni utajiri umelala
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom