Dkt. Bashiru Ally jiuzulu ili kulinda heshima yako, kupewa Ubunge wa kuteuliwa ni kudhalilishwa

Muache ale, wanasiasa wote hata wasio bungeni wanatamani kwenda bungeni kutengeneza maisha yao, sio upinzani wala chama tawala, Bashiru aachwe kusimangwa kilichomkuta ni ajali tu za kisiasa ambazo huwakuta wengi.
Aendeshe gari kilevi apate ajali alafu ya kawaida!!!
Amelipwa anachostahili
 
Nawambia bashiru ni mtu makini basi nyie hamjui.kwa sasa atulie.fungu lake lipo hata kama sio leo nawaambia kuna siku bashiru atalipwa.

Naamini alitimiza wajibu.
Kuhusu huyu Bashiru imeisha hiyo arudi kushika chaki UDSM..Kutolewa kwenye nafasi ya KMK hata mwezi haujaisha ni dharau ya hali ya juu
 
Kwanza kabisa kiustaarabu kwa nafasi ya katibu mkuu kiongozi uliyokuwa nayo haikupaswa kuondolewa mapema namna hiyo. Hata kama ulikuwa haufai kuwa na hiyo nafasi ilitakiwa mkuu wa kaya akuvumilie uvute naye siku hata miezi sita.

Lakini ndani ya mwezi na siku kadhaa ukawa umeg'olewa. Ok sio mbaya maana kwa utumishi wa umma unatakiwa uwe tayari kwa lolote. Lakini sio kwa kuteuliwa kuwa mbunge wa viti maalumu.

Madhari umeshatii mamlaka ya uteuzi basi we jiuzulu na uanze zako tena mimi nakushauri achana na masuala ya siasa ili kulinda heshima zako. Kama vipi rudi Bukoba ukaendeleze kilimo na biashara ya matoke. Maana walichokufanyia ni udhalilishaji.

View attachment 1769575
BASHIRU kwa sasa hana tofauti na wale COVID-19, mbunge wa hisani ya kupewa
 
Bashiru ktk uongozi wake Ali overspeed
Roho take mbaya+roho ya mwendazake speed 1000.
Wenzie walikuwa wamwangalia kwenye binocular
Bashiru bado ni mbunge na baada ya miaka mitano tunampa uongozi mwingina nyie roho mbaya na mafisadi mtabaki mkilialia na safari inaendelea.
Bashiru sio type yenu watu wenye vyeti feki na cv za kubumba.
 
Hii inatufundisha kua uongozi ni dhaman ukipewa fanya kwa weledi, simamia misingi ya haki na utu, chunga maneno usemayo kila unapotakiwa kuongea kama kiongozi.
 
Muache ale, wanasiasa wote hata wasio bungeni wanatamani kwenda bungeni kutengeneza maisha yao, sio upinzani wala chama tawala, Bashiru aachwe kusimangwa kilichomkuta ni ajali tu za kisiasa ambazo huwakuta wengi.
Sielewi kwanini huyu mtu anasakamwa sana
 
Hivi unajua kwa mwezi mmoja na siku kadhaa alizo hudumu kama Katibu Mkuu Kiongozi Ikulu amejua siri kiasi gani za nchi! Unafahamu uzito wa hiyo nafasi? Acha kumchochea aanze kutunishiana misuli na STATE kwa kususa Ubunge, atashughurikiwa.
 
Kwa hiyo kulinda heshima yake ni kutunishia mishuli state?
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom