Mkurugenzi wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), Dkt. Anna Henga, amesema kuwa kati ya manusura 10 wa matukio ya ukatili wa kijinsia, saba ni wanawake.
“Changamoto bado ni kubwa, na ukatili huo unaonekana kutokea zaidi katika kundi la wasichana na wanawake wenye umri wa miaka 15 hadi 49,” amesema.
Ameeleza kuwa aina kuu za ukatili unaoripotiwa ni ukatili wa kipigo, ukatili unaofanywa na wenza, mauaji ya wenza, pamoja na matukio ya ubakaji. Hata hivyo, amebainisha kuwa pia kumekuwepo na ukatili wa kiuchumi unaowaathiri wanawake wengi.
Aidha, amesema kuwa ripoti ya mwaka 2024 kuhusu hali ya haki za binadamu nchini inaonesha kuwa Mkoa wa Dar es Salaam unaongoza kwa matukio ya ukatili wa kijinsia. Ameeleza kuwa hali hiyo inachangiwa na sababu mbalimbali, ikiwemo wingi wa watu, shughuli nyingi za kiuchumi, pamoja na mambo mengine ya kijamii.
Hayo ameyasema Machi 5, 2026, wakati wa maadhimisho ya kuelekea Siku ya Wanawake Duniani, ambapo LHRC ilishiriki kwa kutoa mafunzo na elimu kwa wahudumu wa afya kuhusu utoaji wa huduma kwa manusura wa ukatili wa kijinsia.
Maadhimisho hayo yamefanyika katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Mwananyamala, jijini Dar es Salaam, ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya kilele cha maadhimisho ya kimataifa ya Siku ya Wanawake Duniani yanayofanyika kila mwaka tarehe 8 Machi.
LHRC pia imesisitiza umuhimu wa vituo vya huduma ya pamoja (One Stop Centers) katika kuwasaidia manusura kupata haki kwa haraka na kulinda ushahidi muhimu katika kesi za ukatili wa kijinsia. Hata hivyo, imebainisha kuwa vituo hivyo nchini bado vinakabiliwa na changamoto zinazopunguza ufanisi wake