Dk. Slaa: Nitashinda | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Dk. Slaa: Nitashinda

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by The King, Oct 30, 2010.

 1. T

  The King JF-Expert Member

  #1
  Oct 30, 2010
  Joined: Oct 20, 2010
  Messages: 357
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Dk. Slaa: Nitashinda
  • Kuhitimisha kampeni Mbeya leo

  na Mwandishi wetu


  [​IMG]
  MGOMBEA urais kwa tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dk. Willibrod Slaa, amesema Watanzania wamemkubali kuwa rais wa awamu ya tano wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
  Kutokana na hali hiyo, amewasisitiza wananchi kulinda kura zao kesho kwa kupuuza maagizo potofu yanayotolewa na Jeshi la Polisi.
  Akihutubia mikutano ya hadhara maeneo mbalimbali katika mikoa ya Iringa na Ruvuma kwa nyakati tofauti jana, Dk. Slaa alisema Watanzania wamechoka kutawaliwa na Chama Cha Mapinduzi (CCM), na kwamba kazi iliyobaki ni kupiga kura na kuzilinda, kwa maana CCM kwa kutumia vyombo vya serikali, inafanya njama za kuiba kura zao.
  Aliwataka kupuuza matangazo yanayowataka kupiga kura na kwenda nyumbani na badala yake akawataka wakishapiga kura wasogee umbali wa mita 300 kutoka vituoni, wasubiri matokeo.
  "Hakuna mtu anayeweza kubadili sheria, si OCD wala IGP anayeweza kubadili sheria ya uchaguzi…Sheria inasema ukishapiga kura yako, sogea umbali wa mita 100 kutoka kituoni…sasa mimi nasema, vijana kaeni mita 300, lindeni kura zenu…msipige kelele, msibebe mabango wala bendera," alisema Dk. Slaa.
  Amewaagiza wananchi wote nchini kuhakiki majina yao kwenye vituo walivyojiandikisha na kwamba wale ambao hawataona majina yao kwenye orodha ya wapiga kura, wafikishe taarifa hizo kwa viongozi wa CHADEMA, ili taarifa hizo na majina yao yatumwe kwa faksi makao makuu ya CHADEMA Dar es Salaam kwa ajili ya utekelezaji.
  Ameagiza nakala asilia ya majina hayo, ipelekwe kwa Mkurugenzi wa Uchaguzi makao makuu, kuhoji sababu ya wapiga kura kutokuonekana kwenye orodha; na akasisitiza: "Kama kuna watu hawaonekani kwenye orodha ni mchezo mchafu."
  Alisema ni jambo lisiloingia akili kwamba Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), imekuwa na miaka mitano ya kuandaa daftari la kupigia kura, lakini bado watu wengi nchi nzima wamekuwa wanalalamikia majina yao kutokuonekana kwenye orodha.
  Alisisitiza kuwa nchi iko tayari kwa mabadiliko na kwamba dhamira yake ya kutekeleza ahadi alizotoa kuhusu dira mpya ya taifa ziko palepale.
  "Nazungumza kwa imani na matumaini makubwa, kwa sababu Tanzania nzima vijijini na mijini imenikubali, wananchi wanasema wamechoka kutawaliwa na CCM," alisema.
  Akiwa mjini Songea, huku akipangua propaganda zinazosambazwa na CCM kupotosha ahadi yake ya kuboresha makazi, alisisitiza kwamba anayo taarifa rasmi kuwa gharama ya uzalishaji wa mfuko mmoja wa sementi haizidi sh 4,000 na kwamba ahadi yake ya kushusha gharama ya mfuko huo iko palepale.
  "Na ahadi yetu ya kushusha gharama ya bati kutoka sh 15,000 hadi sh 5,000 imebaki pale pale," alisema huku akishangiliwa na umati.
  Alisema anakwenda Ikulu kusimamia rasilimali za Tanzania ziwanufaishe Watanzania kwanza. "Watanzania kwanza, wengine baadaye. Hatuna nia ya kuwafukuza wawekezaji, lakini waje kwa masharti yetu, si kwa masharti yao," alisema.
  Alisisitiza pia kwamba miongoni mwa kazi atakazofanya katika miezi sita ya kwanza akiwa rais ni kuboresha masilahi na mafao ya watumishi, ikiwa ni pamoja na kuwapandisha vyeo waliosahaulika kwa muda mrefu.
  Alisema mbali na mafao mengine ya watumishi kuhusu afya, elimu, makazi na kadhalika, kima cha chini cha mshahara ya watumishi kitapanda kutoka sh 135,000 ya sasa hadi sh 315,000.
  Dk. Slaa aliwakajeli CCM kwamba kwa miaka 10, iliyopita wamekuwa wakitekeleza kauli zake, na kwamba sasa baada ya kusikia ahadi zake kwenye kampeni, wameanza kuiga baadhi ya sera zake kuhsu elimu.
  Alisema wakati Rais Jakaya Kikwete na mwenyekiti wa kampeni zake, Abdulrahman Kinana, wanasema haiwezekani kutoa elimu bure, Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Profesa Jumanne Maghembe, amesema wanadhamiria kuanza kutoa elimu bure hadi kidato cha nne.
  Dk. Slaa ameahidi kutoa elimu bure hadi kidato cha sita, ambayo pia itakuwa ndiyo elimu ya msingi (ya lazima) kwa kila mtoto wa Tanzania. Alisema hata CCM wakiiga hawawezi kuitekeleza kwa kuwa si sera yao asilia.
  Habari zinasema, maandalizi makubwa yanamsubiri Dk. Slaa mjini Mbeya ambako leo anatarajia kuhitimisha kampeni zake. Tayari wananchi kutoka wilaya mbalimbali, wameshaanza maandalizi kuelekea Mbeya mjini kwa ajili ya mkutano huo unaotarajiwa kuanza saa 4 asubuhi hadi saa 10 jioni. Jana Dk. Slaa alifanya mikutano katika maeneo ya Iringa, Njombe Mashariki, Njombe Magharibi, Mbamba Bay na Songea Mjini.
   
 2. T

  The King JF-Expert Member

  #2
  Oct 30, 2010
  Joined: Oct 20, 2010
  Messages: 357
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kila la heri Dr Slaa. Watanzania tulio wengi tuna imani na uwezo wako wa kuiongoza nchi yetu na tunausubiri ushindi wako wa kishindo kwa hamu kuu na nchi italipuka kwa furaha kubwa sana ambayo haijawahi kuonekana katika historia ya nchi yetu.:peace:
   
 3. h

  harrysonful Member

  #3
  Oct 30, 2010
  Joined: Oct 27, 2010
  Messages: 34
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  and huu ndo mda mwafaka wa CCM kujua kuwa watanzania kesho watawaaibisha na waloku wanapigia kampeni kwa mbwembwe wajiandae kurudisha fedha zetu kama mhe. rais mtarajiwa mhe. dk Wilbroad peter slaa alivoagiza kuwa kufikia tarehe 31oct fedha zote ziwe zimerudi na asubuhi atabanana nao tarehe1 atakapoapishwa....KIKWETEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEE PLZ GET OUTTTTTTTTTTTTTTTTTTTTTTTTTTT OF THAT PALACE,, SIO MAHALI STAHIKI KWAKO... HATUTAKI RAISI ANAECHEKACHEKA TU HOVYO HATA KTK MASWALA YANAYOGUSA MAISHA YA WATU...
   
 4. b

  bojuka Senior Member

  #4
  Oct 30, 2010
  Joined: Sep 9, 2010
  Messages: 128
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  we are waiting to escote you in the palace on 4/11/2010
   
 5. c

  chanai JF-Expert Member

  #5
  Oct 30, 2010
  Joined: Oct 9, 2010
  Messages: 279
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kila la heli Dr Slaa. Kesho watanzania watakuonyesha kiu yao ya mabadiliko
   
 6. T

  The King JF-Expert Member

  #6
  Oct 30, 2010
  Joined: Oct 20, 2010
  Messages: 357
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Tena kubwa sana katika kila kona ya nchi.
   
 7. minda

  minda JF-Expert Member

  #7
  Oct 30, 2010
  Joined: Oct 2, 2009
  Messages: 1,070
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 135
  mungu akutangulie katika hili dr ws.
   
 8. Dingswayo

  Dingswayo JF-Expert Member

  #8
  Oct 30, 2010
  Joined: May 26, 2009
  Messages: 4,011
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 145
  Kila la heri Dr. Slaa. Mungu akubariki sana. Mungu inbariki Tanzania!
   
 9. Jile79

  Jile79 JF-Expert Member

  #9
  Oct 30, 2010
  Joined: May 28, 2009
  Messages: 11,373
  Likes Received: 3,132
  Trophy Points: 280
  Ahsante mungu kwa kutuletea dr.slaa (dr wa ukweli)_kiongozi wa mabadiliko........watz wanakuunga mkono......isipokuwa mafisadi na watoto wao
   
Loading...