Dk. Slaa: Nina siri nyingine nzito

BAK

JF-Expert Member
Feb 11, 2007
124,790
288,109
Dk. Slaa: Nina siri nyingine nzito

na Peter Nyanje
Tanzania Daima

WAKATI Watanzania wakitafakari hatua ya Rais Jakaya Kikwete kutengua uteuzi wa aliyekuwa Gavana wa Benki Kuu (BoT), Dk. Daudi Balali kutokana na kashfa ya akaunti ya malipo ya madeni ya nje (EPA), muasisi wa tuhuma zilizosababisha uchunguzi wa akaunti hiyo, Dk. Willibrod Slaa, ameibuka na siri nyingine kuhusu tuhuma za ufisadi wa viongozi walio serikalini.
Akizungumza na gazeti hili katika mahojiano maalum juzi, Dk. Slaa alisema kuwa anayo majina ya viongozi wakubwa serikalini, ambao walishiriki kuhujumu fedha za nchi kupitia kampuni nyingine kubwa zaidi ya zile zilizotajwa katika ripoti ya Ernst & Young iliyochunguza akaunti ya EPA.

“Nimesikiliza kilichotangazwa, kwanza si ripoti ya uchunguzi wa Ernst & Young kama tulivyoambiwa. Tunachotaka waitoe ripoti nzima kama walivyoahidi.

“Walichokitangaza ni kitu kidogo sana katika ripoti hiyo. Wameficha wanayotaka kuficha na kutangaza wanayotaka kutangaza… haya mambo ni makubwa sana na wameamua kutangaza madogo madogo na kuacha yake makubwa,” alisema Dk. Slaa.

Aliliambia gazeti hili kuwa, ingawa serikali imeshindwa kutimiza ahadi yake ya kutoa hadharani ripoti hiyo ya uchunguzi, yeye anayo majina na kampuni kubwa zilizofanya ubadhirifu wa mabilioni ya fedha za umma.

Pamoja na majina ya kampuni hizo, Dk. Slaa alilithibitishia gazeti hili kuwa, anayo pia majina ya viongozi wakubwa serikalini, ambao wanahusika katika kampuni hizo.

“Wao si wametaja kampuni 22, zile ni za watu wadogo sana, hata ukichunguza utagundua kuwa ni za watu wadogo. Kuna kampuni kubwa za watu wakubwa zimefichwa… Tunataka watueleze kuhusu Deep Green, Meremeta na Tangold, huko ndiko kwenye vigogo,” alisisitiza Dk. Slaa.

Alisema kuwa anayafahamu mambo hayo, iwapo serikali isipotoa ripoti ya uchunguzi uliofanywa na Ernst & Young, yeye atayataja majina ya viongozi hao, kampuni wanazohusika nazo na tuhuma zinazowakabili.

Kwa upande mwingine, Dk. Slaa alifichua kwa gazeti hili kuwa, taarifa alizozitumia kuibua ufisadi huo alizipata pia kutoka kwa maofisa waandamizi kutoka katika idara nyeti ndani ya serikali, ambao wana uchungu na ufisadi wa kutisha unaofanywa ndani ya asasi za umma.

“Huwa tunafanya utafiti, tunasoma na kuperuzi kwenye mitandao. Ndio maana ukiwa pale bungeni utaona kuwa ofisi ya kambi ya upinzani inafanya kazi mpaka saa 8:00 usiku, tunatafuta vitu kama hivi.

“Lakini baada ya kuweka wazi majina ya mafisadi katika mkutano wa hadhara pale Mwembe Yanga mwezi Septemba, Watanzania wengine wenye uchungu na nchi yao, wenye dhamira hai na wanaipenda nchi yao, wakiwemo watumishi wa idara nyeti za serikali, walituletea taarifa nyingi.

“Si kwamba walikuwa wanavujisha siri, hizi si siri, ni ufisadi, kwa hiyo hawabanwi na ile sheria ya siri za serikali… kiongozi huwezi kuwa mwizi serikalini halafu mtu akatoa taarifa hizo, na wewe ukamshitaki eti ametoa siri za serikali,” alifafamua.

Dk. Sla alisema kuwa taarifa nyingine alizipata kwenye mtandao wa intaneti, na kusema hilo limekuwa ni pigo kwa serikali lililotokana na matendo yake yenyewe.

Akifafanua, alisema kuwa wakati sheria ya kuruhusu ushahidi kutoka kwenye mtandao ilipoletwa bungeni, yeye aliipinga, lakini kutokana na uwingi wao, wabunge wa CCM waliipitisha.

“Leo hii sheria hiyo hiyo inahalalisha madai tunayoyatoa na nadhani wanaona ubaya wa walichokipitisha,” alisema.

Kuhusu ripoti ya Ernst & Young, Dk. Slaa alisema kuwa wataendelea kudai itolewe hadharani kwa sababu serikali yenyewe iliahidi kuianika.

Alisema madai yao hayo yatalenga kuwawezesha Watanzania kufahamu kila kitu kilichomo kwenye ripoti hiyo, kwani hatua ya rais kutengua uteuzi wa gavana ni nzito na inathibitisha kuwa kuna kasoro nyingi zilizobainika.

“Rais na serikali si wamiliki wa rasilimali za nchi. Wanapewa dhamana ya kuongoza, si waamuzi wa mwisho, wanatakiwa kuwajibika kwa Watanzania ambao ndio wanaotakiwa kuwa na uamuzi wa mwisho,” alisema.

Kwa upande mwingine, Dk. Slaa alisisitiza kuwa, kuondoka kwa Balali nchini, ilikuwa ni njama mahsusi zilizopangwa ili kuficha baadhi ya mambo.

“Nina taarifa za uhakika nilizozipata kutoka kwa mmoja wa viongozi wa serikali kuwa, Balali alishauriwa aondoke baada ya sisi kufichua ufisadi ili asitoe siri. Nitataja ni nani aliniambia wakati muafaka utakapofika,” alisema.

Alipoulizwa iwapo hana wasiwasi na maisha yake kutokana na mambo yanayotokea hivi sasa, Dk. Slaa alisema kuwa yeye alishayavulia maji nguo na ni lazima ayaoge.

“Ninafanya hivi kutekeleza wajibu wangu kama mwakilishi wa wananchi, wao ndio mawakili wangu, na hivi sasa nimekuwa nikifanya mikutano ya hadhara na kuwaambia siri zote ninazozifahamu ili hata kama kitatokea kitu chochote wananchi wajue ni nini nilikuwa nacho,” alisema.

Tunataka watueleze kuhusu Deep Green, Meremeta na Tangold, huko ndiko kwenye vigogo,”

CCM ! CCM ! CCM !

“Nimesikiliza kilichotangazwa, kwanza si ripoti ya uchunguzi wa Ernst & Young kama tulivyoambiwa. Tunachotaka waitoe ripoti nzima kama walivyoahidi.

CCM ! CCM ! CCM ! Give me a break! Kama wanaweza kuwaibia watanzania through fictitious companies mentioned above, la ajabu ni lipi kutugeuzia kibao na kuibana hiyo ripoti. Subiri kama utaiona hiyo ripoti hadharani toka kwao, ng'o! Na hata hao waliotajwa hata mmoja rumande haendi mtu na hat shillingi moja haiyarudishwa. Mimi siyo nabii ila ni mtanzania na nimeona mengi. So long as Sokoine is still dead; hakuna kumfunga wala kumfilisi mweye pesa Tanzania, tena kama ni za wizi ndiyo sahau.

Alipoulizwa iwapo hana wasiwasi na maisha yake kutokana na mambo yanayotokea hivi sasa, Dk. Slaa alisema kuwa yeye alishayavulia maji nguo na ni lazima ayaoge.

And for your Dr, Mungu ameahidi kumlida yule ambaye anayaweka maisha yake online kutetea haki, hasa haki za wanyonge. Dr. Slaa you will be remembered by generations and generations to come. Mungu akubariki na akulinde! You have played your part as a true patriot!

BIG BOYS DON'T CRY - The late Lucy Dube!
 
Kikwete hii ripoti ya ukaguzi ambao CCM iliukataa kwa madai kwamba hizo kashfa za BOT zilikuwa ni uwongo mpaka pale siri kali iliposhinikizwa na nchi wafadhili, wapinzani na wananchi kwa ujumla haikutayarishwa kwa ajili yako bali imetayarishwa kwa manufaa ya Watanzania wote. Kukataa kuiweka ripoti hiyo hadharani ili Watanzania wote wajue nini kilichomo katika ripoti hiyo ni aina nyingine ya ufisadi kwa kuwaficha ukweli Watanzania.

Tunataka ripoti hiyo itolewe hadharani ili kampuni iliyofanya ukaguzi huo Erns & Young iwathibitishie Watanzania kwamba ripoti iliyowekwa hadharani ndio ripoti halali waliyoiandika wao na hakuna hata paragraph moja iliyofutwa au kubadilishwa kwa manufaa ya mafisadi na waroho wa utajiri wa haraka haraka.
 
Mwacheni Mzee wa watu ale pensheni baada ya kazi nzito ya kuijenga CDM.
 
Dk. Slaa: Nina siri nyingine nzito

na Peter Nyanje
Tanzania Daima

WAKATI Watanzania wakitafakari hatua ya Rais Jakaya Kikwete kutengua uteuzi wa aliyekuwa Gavana wa Benki Kuu (BoT), Dk. Daudi Balali kutokana na kashfa ya akaunti ya malipo ya madeni ya nje (EPA), muasisi wa tuhuma zilizosababisha uchunguzi wa akaunti hiyo, Dk. Willibrod Slaa, ameibuka na siri nyingine kuhusu tuhuma za ufisadi wa viongozi walio serikalini.
Akizungumza na gazeti hili katika mahojiano maalum juzi, Dk. Slaa alisema kuwa anayo majina ya viongozi wakubwa serikalini, ambao walishiriki kuhujumu fedha za nchi kupitia kampuni nyingine kubwa zaidi ya zile zilizotajwa katika ripoti ya Ernst & Young iliyochunguza akaunti ya EPA.

“Nimesikiliza kilichotangazwa, kwanza si ripoti ya uchunguzi wa Ernst & Young kama tulivyoambiwa. Tunachotaka waitoe ripoti nzima kama walivyoahidi.

“Walichokitangaza ni kitu kidogo sana katika ripoti hiyo. Wameficha wanayotaka kuficha na kutangaza wanayotaka kutangaza… haya mambo ni makubwa sana na wameamua kutangaza madogo madogo na kuacha yake makubwa,” alisema Dk. Slaa.

Aliliambia gazeti hili kuwa, ingawa serikali imeshindwa kutimiza ahadi yake ya kutoa hadharani ripoti hiyo ya uchunguzi, yeye anayo majina na kampuni kubwa zilizofanya ubadhirifu wa mabilioni ya fedha za umma.

Pamoja na majina ya kampuni hizo, Dk. Slaa alilithibitishia gazeti hili kuwa, anayo pia majina ya viongozi wakubwa serikalini, ambao wanahusika katika kampuni hizo.

“Wao si wametaja kampuni 22, zile ni za watu wadogo sana, hata ukichunguza utagundua kuwa ni za watu wadogo. Kuna kampuni kubwa za watu wakubwa zimefichwa… Tunataka watueleze kuhusu Deep Green, Meremeta na Tangold, huko ndiko kwenye vigogo,” alisisitiza Dk. Slaa.

Alisema kuwa anayafahamu mambo hayo, iwapo serikali isipotoa ripoti ya uchunguzi uliofanywa na Ernst & Young, yeye atayataja majina ya viongozi hao, kampuni wanazohusika nazo na tuhuma zinazowakabili.

Kwa upande mwingine, Dk. Slaa alifichua kwa gazeti hili kuwa, taarifa alizozitumia kuibua ufisadi huo alizipata pia kutoka kwa maofisa waandamizi kutoka katika idara nyeti ndani ya serikali, ambao wana uchungu na ufisadi wa kutisha unaofanywa ndani ya asasi za umma.

“Huwa tunafanya utafiti, tunasoma na kuperuzi kwenye mitandao. Ndio maana ukiwa pale bungeni utaona kuwa ofisi ya kambi ya upinzani inafanya kazi mpaka saa 8:00 usiku, tunatafuta vitu kama hivi.

“Lakini baada ya kuweka wazi majina ya mafisadi katika mkutano wa hadhara pale Mwembe Yanga mwezi Septemba, Watanzania wengine wenye uchungu na nchi yao, wenye dhamira hai na wanaipenda nchi yao, wakiwemo watumishi wa idara nyeti za serikali, walituletea taarifa nyingi.

“Si kwamba walikuwa wanavujisha siri, hizi si siri, ni ufisadi, kwa hiyo hawabanwi na ile sheria ya siri za serikali… kiongozi huwezi kuwa mwizi serikalini halafu mtu akatoa taarifa hizo, na wewe ukamshitaki eti ametoa siri za serikali,” alifafamua.

Dk. Sla alisema kuwa taarifa nyingine alizipata kwenye mtandao wa intaneti, na kusema hilo limekuwa ni pigo kwa serikali lililotokana na matendo yake yenyewe.

Akifafanua, alisema kuwa wakati sheria ya kuruhusu ushahidi kutoka kwenye mtandao ilipoletwa bungeni, yeye aliipinga, lakini kutokana na uwingi wao, wabunge wa CCM waliipitisha.

“Leo hii sheria hiyo hiyo inahalalisha madai tunayoyatoa na nadhani wanaona ubaya wa walichokipitisha,” alisema.

Kuhusu ripoti ya Ernst & Young, Dk. Slaa alisema kuwa wataendelea kudai itolewe hadharani kwa sababu serikali yenyewe iliahidi kuianika.

Alisema madai yao hayo yatalenga kuwawezesha Watanzania kufahamu kila kitu kilichomo kwenye ripoti hiyo, kwani hatua ya rais kutengua uteuzi wa gavana ni nzito na inathibitisha kuwa kuna kasoro nyingi zilizobainika.

“Rais na serikali si wamiliki wa rasilimali za nchi. Wanapewa dhamana ya kuongoza, si waamuzi wa mwisho, wanatakiwa kuwajibika kwa Watanzania ambao ndio wanaotakiwa kuwa na uamuzi wa mwisho,” alisema.

Kwa upande mwingine, Dk. Slaa alisisitiza kuwa, kuondoka kwa Balali nchini, ilikuwa ni njama mahsusi zilizopangwa ili kuficha baadhi ya mambo.

“Nina taarifa za uhakika nilizozipata kutoka kwa mmoja wa viongozi wa serikali kuwa, Balali alishauriwa aondoke baada ya sisi kufichua ufisadi ili asitoe siri. Nitataja ni nani aliniambia wakati muafaka utakapofika,” alisema.

Alipoulizwa iwapo hana wasiwasi na maisha yake kutokana na mambo yanayotokea hivi sasa, Dk. Slaa alisema kuwa yeye alishayavulia maji nguo na ni lazima ayaoge.

“Ninafanya hivi kutekeleza wajibu wangu kama mwakilishi wa wananchi, wao ndio mawakili wangu, na hivi sasa nimekuwa nikifanya mikutano ya hadhara na kuwaambia siri zote ninazozifahamu ili hata kama kitatokea kitu chochote wananchi wajue ni nini nilikuwa nacho,” alisema.

Sijui wazimu gani uliwapata Chadema hadi wakampiga teke huyu na wakampa favour Lowassa.
Chadema ya sasa haina kikohozi kabisa.
Haishtui...imekuwa goigoi.
Kelele zilibakia za Lissu tu...
Na Lissu alikuwa anapiga kelele kama yatima. hakuna cha Mbowe, Mashinji au Lowassa waliokuwa naye kwenye huo mpambano
 
Back
Top Bottom