Dk. Slaa kidume | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Dk. Slaa kidume

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mlengo wa Kati, Apr 30, 2011.

 1. Mlengo wa Kati

  Mlengo wa Kati JF-Expert Member

  #1
  Apr 30, 2011
  Joined: Feb 16, 2011
  Messages: 2,733
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  *Kesi ya Chadema Arusha yaibua mapya
  *Mahakama yaelezwa Josephine mjamzito
  Na Eliya Mbonea, Arusha
  [​IMG]KATIBU Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dk. Wilbrod Slaa, anatarajia kupata mtoto kutoka kwa Josephine Mushumbusi.
  Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha ilielezwa jana kwamba Josephine ambaye anatajwa na Dk. Slaa kuwa ni mchumba wake, ana ujauzito wa miezi minane na wiki tatu. Katika hali ya kawaida, mjamzito anaweza kujifungua baada ya miezi tisa.
  Kutokana na hali hiyo, ilielezwa kwamba alishindwa kuhudhuria mahakamani kama alivyotakiwa.
  Eminiel Mahimbo, ambaye anadai kuwa Josephine ni mkewe, mwaka jana alifungua kesi dhidi ya Dk. Slaa ambayo pamoja na mambo mengine, anataka alipwe fidia na mshitakiwa.
  Pia, mlalamikaji aliomba Mahakama imwekee zuio Dk. Slaa ili asishiriki tendo la ndoa wakati kesi ya msingi ikiwa haijaamuliwa.
  Josephine ni mtuhumiwa wa nane katika kesi inayowakabili viongozi na wafuasi 19 wa Chadema waliofunguliwa mashitaka manane.
  Mashitaka dhidi ya watuhumiwa hao yalifunguliwa Januari 5, mwaka huu. Pamoja na mambo mengine, wanatuhumiwa kufanya mkusanyiko usio halali na pia kuendesha vitendo vya uchochezi.
  Wakili wa utetezi, Method Kimomogolo, akitoa taarifa ya mtuhumiwa Josephine mbele ya Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Arusha, Charles Magesa, alidai kwamba mteja wake amepewa ruhusa na daktari ya kupumzika kutokana na hali inayomkabili kwa sasa.
  “Mheshimiwa mtuhumiwa wa nane, Josephine amepewa ruhusa na daktari ya kupumzika kutokana na ujauzito wa miezi minane na wiki tatu,” alisema.
  Hata hivyo, wakati wakili Komomogolo akitoa taarifa hiyo, Hakimu Magesa alionyesha kupinga kuipokea kwa maelezo kwamba hapakuwa na vyeti vya daktari vinavyoonyesha ruhusa hiyo.
  “Tunaomba vyeti vya daktari, si taarifa ya mdomo Mahakama itajiaminisha vipi katika hili? Alihoji.
  Wakili Kimomogolo alijitahidi kuifafanulia Mahakama hiyo kuwa walishindwa kufika na vyeti vya ruhusa kutokana na Josephine kuwa chini ya uangalizi kwenye hospitali binafsi.
  “Mheshimiwa kama nilivyoeleza mtuhumiwa ana ujauzito wa miezi minane na daktari anayemwangalia hakuwapo, na lazima yeye ndiye anayehusika na uandikaji wa ruhusa yake,” alidai Wakili Kimomogolo.
  Utetezi huo uliendelea kupingwa na Hakimu Magesa kwa kumweleza Kimomogolo kwamba yeye hakuwa ameuliza mtuhumiwa ana mimba ya muda gani.
  “Sijauliza ana mimba ya miezi mingapi, kwani leo si mlijua ni siku ya kesi? Kwanini hamkuandaa taarifa hizo mapema?” Alihoji.
  Wakati mtuhumiwa huyo akiwa ameshindwa kufika mahakamani, mtuhumiwa wa 6, Mathias Valerian, naye hakutokea mahakamani, hatua iliyosababisha kuibuka kwa mvutano wa kisheria wa, ama kuendelea na usikilizwaji wa awali wa kesi, au kuahirisha hadi watuhumiwa wote watakapokuwapo.
  Hatua hiyo iliibuliwa na Wakili wa Serikali, Neema Ringo, baada ya kuomba Mahakama iahirishe kesi hiyo kutokana na watuhumiwa wawili kutokuwapo mahakamani, huku akiwa hana taarifa za mtuhumiwa wa 16.
  Akijibu hoja hiyo, wakili wa utetezi, Albert Msando, aliiambia Mahakama kwamba kwa vile kesi hiyo ipo kwenye hatua ya usikilizwaji wa awali na kesi husika ina watuhumiwa 19, huenda ikawa vigumu kuwapata wote kwa wakati mmoja, hivyo ni busara upande wa mashitaka ukaendelea kusoma maelezo ya awali.
  Naye, wakili wa Serikali aliyekuwa akisaidiana na Ringo, Awamu Mbangwa, alipiga hoja ya wakili Msando akidai hoja hiyo haikuwa sahihi.
  Huku akinukuu kesi mbalimbali, wakili Mbangwa alidai kuwapo kwa watuhumiwa wote mahakamani wakati wa usikilizwaji wa awali ni jambo la lazima na si ombi kwa watuhumiwa.
  “Mheshimiwa Hakimu kutokana na mazingira haya kesi hii haiwezi kuendelea pasipo washitakiwa wenyewe kuwapo,” alidai Wakili Mbangwa.
  Kutokana na hoja hizo, ilimlazimu tena wakili Msando kuieleza Mahakama kwamba kuwapo kwa mshitakiwa mahakamani ni lazima, lakini bado hakuizuii Mahakama kuendelea na kesi.
  Akinukuu Sheria ya Makosa ya Jinai ya mwaka 1992, Act namba 9 ambayo ndiyo ilifanyiwa marekebisho, wakili Mbando alidai kwamba marekebisho hayo ya kuliondoa neno “and” na kuwekwa “all” yanatoa mwanya wa kuruhusu kesi zisiendelee kucheleweshwa.
  Akijibu hoja za pande zote mbili ambazo pia zililazimu mahakama hiyo kuahirishwa kwa muda wa dakika 45 hivi, Hakimu Magesa alisema kwamba ili kesi hiyo iweze kuendelea na hatua ya usikilizwaji wa awali, ni lazima watuhumiwa wote wawepo mahakamani.
  “Kama leo tukiendelea na hatua ya usikilizwaji wa awali ina maana kwamba watuhumiwa ambao hawapo leo itabidi siku wakija tuwasomee tena maelezo haya ili wakubali au wakatae,” alisema Hakimu Magesa.
  Kutokana na uamuzi huo wa Hakimu Magesa, pande zote mbili katika kesi hiyo zilikubaliana kuahirisha kesi hiyo hadi Mei 27, mwaka huu.
   
 2. ADAM MILLINGA

  ADAM MILLINGA Senior Member

  #2
  Apr 30, 2011
  Joined: Apr 27, 2011
  Messages: 117
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Wametumwa hao hawana jipya ila kwakweli daktar ww ni kidume na mafisad wanaogopa sana kuja kwa mtoto wako wanajua kuwa mtoto wa nyoka nyoka ivyo songa mbele baba wew ndo mkomboz wa taifa hili tanzania a beautiful county controlled by blind people baba slaa tunakupenda tunakuitaji hakika wewe ni mpambanaj wataongea lakn cku moja watashindwa kwan njia ya muongo fup
   
 3. L

  LAT JF-Expert Member

  #3
  Apr 30, 2011
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 4,523
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 0
  sipendi udaku na umbea ..... ! wahi B bar pale sinza kama huna cha kufanya kuna chakula safi sana
   
 4. Mlengo wa Kati

  Mlengo wa Kati JF-Expert Member

  #4
  Apr 30, 2011
  Joined: Feb 16, 2011
  Messages: 2,733
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Asonge mbele kupata watoto zaidi????????????????????
   
 5. M

  Mr.Mak JF-Expert Member

  #5
  Apr 30, 2011
  Joined: Feb 23, 2011
  Messages: 2,635
  Likes Received: 496
  Trophy Points: 180
  Jamaa mwenye mke alivoona hii post atakuwa amelia sana. ivi jichukue wewe halafu jiweke kwenye nafasi ya yule mdume ambae Slaa kamuibia mkewe halafu uwe wewe ndio umesikia Slaa kampa mimba mkewe utajisikiaje? Je huyo mtoto akizaliwa kanisa linamtambuaje na kwa ndoa gani? Slaa amefanya aibu na anaendelea kuifanya hiyo aibu kubwa ambayo kanisa linapaswa kumpa kisogo,mambo kama hayo atleast yakifanywa na mtu ambaye hakukulia kanisani watu hawashangai sana. Ivi mungu gani ambaye Slaa anamuamini? maana kama ni yule ambaye wakatoliki wanamuamini hiyo vitendo aliviharamisha. anaishi katika zinaa Dr mzima?
   
 6. m

  mkuki moyoni Senior Member

  #6
  Apr 30, 2011
  Joined: Apr 29, 2011
  Messages: 116
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  okay...hakuna anayetumwa wewe kijana acha hizo kazi unazofanya humu,mbona hauheshimu mawazo ya wenzako? ila Dr hapo hatuna cha kusema tena kwani kilichokuwa kinatuudhi ni kesi il ilivyokuwa ikipelekwa fasta na ccm kisa urais...haya sasa ya mke wa mtu hayawahusu watanzania kabisaaaaa....na kesi yenyewe hatuioni tena....je, kama slaa amemliki na mwenye mke haonekan tena unadhani nn kitatokea? ila sipendi wewe unayesma watu wametumwa humu, au umetumwa wewe na nani aliyekutuma mtu mropokaji hivyo?la hasha ni medula yako tu hiyo.
   
 7. Dr-of-three-Phd

  Dr-of-three-Phd Senior Member

  #7
  Apr 30, 2011
  Joined: Oct 20, 2010
  Messages: 194
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  umbeya mtupu, acha umbeya wewe! andika ya kwao tukudadavue?
   
 8. F

  Ferds JF-Expert Member

  #8
  Apr 30, 2011
  Joined: Oct 27, 2010
  Messages: 1,267
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135
  crap..............................crap..................................................crap
   
 9. BONGOLALA

  BONGOLALA JF-Expert Member

  #9
  Apr 30, 2011
  Joined: Sep 14, 2009
  Messages: 13,785
  Likes Received: 2,397
  Trophy Points: 280
  Ina maana atapata mtoto nje ya ndoa?au walishafunga ndoa
   
 10. L

  LAT JF-Expert Member

  #10
  Apr 30, 2011
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 4,523
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 0
  id yako .... maneno huumba
   
 11. m

  mmaroroi JF-Expert Member

  #11
  Apr 30, 2011
  Joined: May 8, 2008
  Messages: 2,536
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Dr.Slaa ni nyota inayong'aa Tanzania na ni mkombozi wa nchi hii. Mungu ambariki Dr. ili siku moja awe Rais wa TZ kwa maendeleo yake.
   
 12. VIKWAZO

  VIKWAZO JF-Expert Member

  #12
  Apr 30, 2011
  Joined: Apr 9, 2011
  Messages: 1,910
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  hata kama hayo no masuhala yao ya kiroho, mbona wewe hatujakuuliza ulizaliwa ndani ya ndoa au la?
  mbona mbona mzee wa watu mnamchimba hivyo, Je kikwete kwa kusamehe wezi kwa dini yake anakwenda wapi moto au peponi ?
   
 13. S

  Songasonga Senior Member

  #13
  Apr 30, 2011
  Joined: Mar 13, 2011
  Messages: 152
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Jina la mtoto? CCM Gamba
   
 14. only83

  only83 JF-Expert Member

  #14
  Apr 30, 2011
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 5,252
  Likes Received: 445
  Trophy Points: 180
  Nothing to comment in this thread...nonsense!!!! aka crap...
   
 15. Mlengo wa Kati

  Mlengo wa Kati JF-Expert Member

  #15
  Apr 30, 2011
  Joined: Feb 16, 2011
  Messages: 2,733
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Hahahaha Dr Slaa(Phd)!
   
 16. Kishongo

  Kishongo JF-Expert Member

  #16
  Apr 30, 2011
  Joined: May 4, 2010
  Messages: 932
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Matunda ya uzinzi.
   
 17. Bepari

  Bepari JF-Expert Member

  #17
  Apr 30, 2011
  Joined: Feb 17, 2011
  Messages: 814
  Likes Received: 245
  Trophy Points: 60
  Usijali 1st lady mtarajiwa, ni maneno ya wakosaji tu hayo.
  Hivi mimba ilitunga kipindi cha kampeni eegh, du kweli mumeo mpya kidume kama unavyosema...
   
 18. Leonard Robert

  Leonard Robert JF-Expert Member

  #18
  May 1, 2011
  Joined: Apr 22, 2011
  Messages: 9,150
  Likes Received: 2,467
  Trophy Points: 280
  Dr.slaa i salute you,wewe ni mbadala wa jk
   
 19. m

  mkuki moyoni Senior Member

  #19
  May 1, 2011
  Joined: Apr 29, 2011
  Messages: 116
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  umri na kazi wazeeeee
   
 20. Kobello

  Kobello JF-Expert Member

  #20
  May 1, 2011
  Joined: Feb 20, 2011
  Messages: 5,689
  Likes Received: 656
  Trophy Points: 280
  Sidhani kama ni mtu wa dini,hiyo hamna ubishi!,ila mtoto ni mtoto
   
Loading...