Dk. Slaa: DC Kiteto afukuzwe kazi

Dk. Slaa: DC Kiteto afukuzwe kazi

Donatila

JF-Expert Member
Joined
Oct 23, 2014
Posts
8,247
Reaction score
25,191
Chadema--November19-2014.jpg

Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Dk. Willibrod Slaa, akihutubia wananchi wa kijiji cha Ludewa Wilaya ya Kilosa mkoani Morogoro katika mkutano wa Operesheni Delete CCM uliofanyika katika Uwanja wa Shule ya Msingi Ludewa juzi

Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chedema) Dk. Willibrod Slaa, amemuweka njia panda Mkuu wa Wilaya ya Kiteto mkoani Manyara, Martha Umbulla, baada ya kumuomba Rais Jakaya Kikwete amfukuze kazi kwa madai ameshindwa kuzuia mapigano ya wafugaji na wakulima ambayo hadi sasa yamesababisha vifo vya watu zaidi ya 10.

Akizungumza katika mkutano wa hadhara uliofanyika kijiji cha Mvuha mkoani Morogoro, alisema kama Rais Kikwete hatamchukulia hatua Mkuu huyo wa wilaya wananchi wanaoona damu ikimwagika hawawezi kumwelewa.

Dk. Slaa aliwaomba wakulima na wafugaji kuacha kupigana na kuuana wakigombea ardhi badala yake waiwajibishe Serikali ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwa madai ndiyo chanzo cha migogoro ya ardhi inayoendelea nchini.

"Migogoro ya ardhi inayoendelea nchini ni matokeo ya serikali ya CCM kushindwa kuwajibika ipasavyo hasa katika kuweka mipango mizuri ya matumizi ya ardhi ambayo ni majukumu ya serikali za mitaa," alisema.

Dk Slaa ambaye jana alianza ziara ya chama hicho iliyopewa jina la ‘Operesheni Delete CCM' akimpokea Mwenyekiti wa Chadema Taifa, Freeman Mbowe, alisema kutoka na chama tawala kushindwa kuweka sera nzuri za ardhi hivyo imefika wakati kwa wananchi kuchukua hatua ya kufanya mabadiliko.

Alisema kuwa umwagikaji wa damu huo usipodhibitiwa na migogoro hiyo kutafutiwa ufumbuzi wa kudumu, Serikali itakuwa imeshindwa moja ya majukumu yake ya msingi ya kulinda raia wake na mali zao.

"Tunavyozungumza hivi sasa kuna matukio ya kutisha yametokea huko Kiteto, Siha, Malinyi na kwingine,wakulima na wafugaji…ninyi wote ni Watanzania. Nawaomba sana muendelee kuishi kama ndugu kama ilivyokuwa huko nyuma," alisema.

"Haya ni matokeo ya Serikali kushindwa majukumu yake. Ni matokeo ya sera za CCM kushindwa. Mipango na matumizi mazuri ya ardhi, ili ardhi ya mifugo ijulikane na ardhi ya kilimo ijulikane na matumizi mengine ni kazi za serikali za mitaa kupitia halmashauri," alisema.

Dk. Slaa alisema chanzo cha mauaji yanayoendelea Kiteto ni baadhi ya wanasiasa wanaoongoza wilaya hiyo akiwamo Mkuu wa Wilaya, Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya na mbunge ambao wameshindwa kuwajibika ipasavyo.

CHANZO: NIPASHE
 
Kwanza lazima atueleze ni lini ameanza kumtambua Rais Kikwete kama ndiyo Commander-in-chief.

Wahenga walisema, ukiwa muongo lazima usiwe msahaurifu.

Kwa sasa ameishasahau kama alisema baada ya matokeo ya Uchaguzi Mkuu mwaka 2010 kuwa hamtambui Rais Kikwete kama Rais wa Tanzania.

Viongozi wakuu wa CHADEMA hawana mpinzani nchini kwenye siasa za kilaghai.
 
kwa hiyo yanayoendelea ni mazuri ??
 
How?

Ameshindwa kuwajibika how, specifically?

Umesema tatizo ni sera ya nchi ya ardhi, sasa Mkuu wa Wilaya abadilishe vipi sera ya ardhi?

Ningetegemea wabunge, no less wabunge wako wa CHADEMA, ndio wangesaidia kubadilisha sera ya ardhi, wamefanya nini? You are simply piggybacking Job Ndugai's feckless call for action. I mean, thats an egregious dereliction of duty on CHADEMA.

Huwezi kusema "Wananchi acheni kupigana" halafu hapo hapo ukasema "tatizo ni sera za ardhi..." ina maana wananchi wakiweza kuacha kupigana then huhitaji tena sera mpya! Au kama tatizo ni sera mbovu basi wananchi hawawezi kuacha kupigana so long as sera za ardhi bado ni zile zile! Huwezi kuwalaumu wananchi kwa hili!
 
kwa hiyo yanayoendelea ni mazuri ??
Ndugu,
Hoja hapa ni yule anayekemea au kutoa ushauri kwa Rais wa Tanzania na siyo matukio yanayofanyika.

Dk. Slaa hana moral authority, political authority and political obligation ya kumwambia Rais Kikwete amwajibishe Mkuu wa Wilaya wakati hamtambui kama ni Rais wa Tanzania, otherwise, atueleze ni lini alimtambua Rais Kikwete kama Rais wa Tanzania.
 
we MwanaDiwani ni hovyo kweli, sisi tunasikitika mauaji mkoani kiteto wewe unazungumzia utambuaji wa rais? Acha upu.mb.aff
 
Last edited by a moderator:
Kwanza lazima atueleze ni lini ameanza kumtambua Rais Kikwete kama ndiyo Commander-in-chief.

Wahenga walisema, ukiwa muongo lazima usiwe msahaurifu.

Kwa sasa ameishasahau kama alisema baada ya matokeo ya Uchaguzi Mkuu mwaka 2010 kuwa hamtambui Rais Kikwete kama Rais wa Tanzania.

Viongozi wakuu wa CHADEMA hawana mpinzani nchini kwenye siasa za kilaghai.

Dada samahani nikuulize kitu eti Profesa kasharudi nchini kutoka USA?
 
Mzee slaa kwani yeye nani mpaka anaiagiza serikali mpaka anaigiza serikali yeye akomee kwa josephine tu kuagiza serikalini asitie mguu atapigwa tifu.
 
Anadhani viongozi wa serikali wanafukuzwa hovyo hovyo kama wao wanavyofukuza "wasaliti" huko CHADEMA kwao?
 
Utakaporudiwa na ufahamu utaelewa kuwa ni haki ya kila raia kuiagiza serikali kutimiza yale ambayo Rais aliapa mbele ya umma kuwa atasimamia usalama wa kila raia na mali zake. Ila kwa sasa nadhani kwa vile kichwani kwako hakujakaa sawa, ndiyo maana unahoji kwa swali la kijinga.

Yeye ni nani mpaka aiagize Serikali!?? Serikali ina taratibu zake za kufanya kazi.
 
Ndugu,
Hoja hapa ni yule anayekemea au kutoa ushauri kwa Rais wa Tanzania na siyo matukio yanayofanyika.

Dk. Slaa hana moral authority, political authority and political obligation ya kumwambia Rais Kikwete amwajibishe Mkuu wa Wilaya wakati hamtambui kama ni Rais wa Tanzania, otherwise, atueleze ni lini alimtambua Rais Kikwete kama Rais wa Tanzania.

Ungekuwa mwanangu ningebadilishana na mkate wa elfu moja tu
 
Huyu prof. wa Kichina kikubwa anachofanya ni kuwezesha wananchi kukosa huduma badala ya kuwaletea huduma:
1. Anatumia hela yetu kuzurura, na wakati fulani kwenda kubembea nje.
2. Serikali yake jukumu lake kubwa ni kulinda majizi ya chamani mwake (ref. EPA, ESCROW,etc)
3. Kuwapa vyeo ndugu/maswahiba hata kama hawana uwezo wa kuongoza
4. Kuetetea sheria na mifumo inayosaidia wizi kutendeka na kulinda wahusika

Nyie anawalisha na kuwafanya muishi leo unajifanya hujui yuko wapi.
 
Wapumbavu CCM ni wengi sana. Maana hawajui hata haki za msingi za raia za kuilazimisha serikali kutimiza wajibu wake. Wanadhani kuilazimisha serikali kutimiza wajibu wake ni lazima uwe kiongozi wa CCM kama Kinana. Aibu kubwa!

Wananchi tuna haki, siyo tu kumtaka Rais amfukuze mkuu wa wilaya, tuna haki na uwezo wa kumtaka Rais amfukuze kiongozi yeyote yule alimradi ikithibitika utendaji wa kiongozi huyo hauna maslahi kwa umma. Na hapo Rais anachotakiwa au atekeleze matakwa ya umma au yeye mwenyewe aondoke.

Mzee slaa kwani yeye nani mpaka anaiagiza serikali mpaka anaigiza serikali yeye akomee kwa josephine tu kuagiza serikalini asitie mguu atapigwa tifu.
 
Ndugu,
Hoja hapa ni yule anayekemea au kutoa ushauri kwa Rais wa Tanzania na siyo matukio yanayofanyika.

Dk. Slaa hana moral authority, political authority and political obligation ya kumwambia Rais Kikwete amwajibishe Mkuu wa Wilaya wakati hamtambui kama ni Rais wa Tanzania, otherwise, atueleze ni lini alimtambua Rais Kikwete kama Rais wa Tanzania.

wewe ni msukule hoja hapa ni vifo vya watu ww unataka amtambue raisi au kwa vile lowasa ndo mfadhili wa silaha kwa wafugaji
 
Back
Top Bottom