Dk. Slaa awindwa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Dk. Slaa awindwa

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Ujengelele, Sep 5, 2010.

Thread Status:
Not open for further replies.
 1. U

  Ujengelele JF-Expert Member

  #1
  Sep 5, 2010
  Joined: Jan 14, 2008
  Messages: 1,256
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Dk. Slaa awindwa
  • Mikakati ya kumchafua yashika kasi

  na Asha Bani

  MGOMBEA wa urais kwa tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), hivi sasa ndiye anayeonekana kuwindwa, kukamiwa na kuandaliwa mikakati ya kumchafua kwa kutumia mbinu mbalimbali, Tanzania Daima Jumapili imebaini.

  Dk. Slaa anaonekana kuwa tishio kwa Chama Cha Mapinduzi (CCM) tangu atangazwe kugombea nafasi ya urais katika Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 31, mwaka huu.

  Baadhi ya vigogo wa CCM wamekuwa wakihaha usiku na mchana kutafuta tuhuma za kumhusisha nazo Dk. Slaa, ikiwamo ile ya ndoa yake, kwa lengo la kummaliza kisiasa ili mgombea wa chama tawala apate ushindi wa kishindo.

  Dk. Slaa amekuwa mwiba mkali katika kampeni za mwaka huu, tofauti na wagombea wengine wa vyama vya upinzani kutokana na umaarufu wake aliojijengea ndani na nje ya Bunge, hasa kutokana na kusimamia hoja ya ufisadi pamoja na ile ya wizi wa fedha katika Akaunti ya Malipo ya Madeni ya Nje (EPA).

  Hoja ya wizi wa EPA iliyoibuliwa tena hivi karibuni na kada wa CHADEMA, Mabere Marando, kwa kuwataja baadhi ya vigogo walio madarakani na waliomaliza muda wao, kuwa ndio waliobariki wizi huo ambao fedha zinadaiwa zilisaidia kampeni za CCM, 2005, imezidisha utete wa kampeni.

  Mara kadhaa vigogo wa CCM akiwamo Katibu Mkuu, Yusuf Makamba na Mwenyekiti wa timu ya kampeni ya mgombea urais wa CCM, Abdulrahman Kinana, kwa nyakati tofauti wamejaribu kujibu tuhuma hizo, huku wakisisitiza kuwa hakuna kigogo aliyeshiriki kwenye wizi huo.

  Mkakati mwingine unaoonekana kummaliza mgombea huyo ni ule wa kusambazwa kwa magazeti katika mikoa ya Kilimanjaro na Arusha ambayo yanagawiwa bure kwa wananchi.

  Hadi juzi jumla ya nakala 3,500 za gazeti moja linalotoka kila wiki zilikuwa zimechapwa na kusambazwa zikiwa na habari zinazodai kuwa Dk. Slaa amepora mke wa mtu.

  Mkakati huo unadaiwa kutumiwa na vigogo kadhaa ambao ni wapinzani, umewahusisha wauzaji wa magazeti katika mikoa hiyo, ambao wameelekezwa kuyagawa bure katika maeneo yenye mikusanyiko ya watu kama vile stendi za mabasi.

  Wakati matukio hayo yakitendeka, Dk. Slaa jana alimkabidhi mikoba yake aliyokuwa anaitumia bungeni mgombea ubunge wa Jimbo la Singida Mashariki, Tundu Lissu.

  Akimnadi mgombea huyo katika mikutano mitatu tofauti ya kampeni jimboni humo, Dk. Slaa alisema mbunge huyo mtarajiwa, atakuwa Dk. Slaa mwingine atakapoingia bungeni kutokana na umakini wake.

  Huku akishangiliwa na maelfu ya wananchi, Dk. Slaa alisema Lissu ambaye ni mwanasheria maarufu nchini, amekuwa mwiba kwa serikali hata kabla ya kuingia bungeni.

  "Serikali yenyewe tayari ina mwogopa Lissu, hivyo akiingia bungeni, atakuwa Dk. Slaa mwingine, naomba mpeni kura zenu, huyu ndiye baba wa kulinda haki za wanyonge," alisema Dk. Slaa.

  Katika hatua nyingine, Dk. Slaa amesema endapo ataingia madarakani, serikali yake itashirikiana na hospitali za taasisi na madhehebu ya dini kuziendesha.

  Dk. Slaa, alitoa kauli hiyo jana kwa nyakati tofauti wakati wa mikutano yake ya kampeni, iliyofanyika eneo la Makyungu, Dungunyi, Ntuntu na Mang'onyi, katika Jimbo la Singida Mashariki.

  Katika pingamizi hilo lililotolewa na CHADEMA wiki iliyopita, chama hicho kinapinga kitendo cha Kikwete kutamka kuwa amepandisha mishahara pamoja na kutoa ahadi ya kununua meli kubwa ya kisasa kwa wakazi wa mikoa ya Kanda ya Ziwa.

  Katika pingamizi hilo, CHADEMA inadai Rais Kikwete ametoa ahadi hizo kwa lengo la kuwashawishi wapiga kura wamchague, jambo ambalo ni kinyume cha sheria ya gharama za uchaguzi.

  Wakati huo huo, Marando amesema ataendelea kusema ukweli wa kile ambacho Chama Cha Mapinduzi (CCM) kinawakosea Watanzania, hata kama chama hicho kitakimbilia kushitaki kwa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC).

  Kauli hiyo aliitoa katika uzinduzi wa kampeni za ubunge katika Jimbo la Segerea, ambapo alisema anawashangaa viongozi wa chama hicho wakiongozwa na Katibu Mkuu wao, Yusuf Makamba, kudai kuwa CHADEMA imewatukana.

  Alisema CHADEMA haitoi matusi bali inasema ukweli na kwamba mgombea wa urais kupitia chama hicho, Jakaya Kikwete, anawadanganya Watanzania kwa ahadi ambazo anashindwa kuzitekeleza.

  Alisema kwa sasa Kikwete anayoyoma kwa ahadi lukuki, huku akitoa mfano kwamba itafikia wakati atawaeleza wakazi wa Dodoma kuwa anaweza akauhamisha Mlima Kilimanjaro kutoka mkoani Kilimanjaro kwenda katika mji huo mkuu.

  Alisema hatashangaa siku akisikia wakazi wa mikoa ya Lindi na Mtwara wakiahidiwa kuhamishiwa maji kutoka Ziwa Victoria kwenda katika mikoa hiyo.

  "Tukisema ukweli, wanasema ni matusi, hebu ona leo mgombea urais anatoa ahadi kibao, tena mpya, wakati zile za mwaka 2005 hajafikia hata nusu yake, leo anasema kuwa atapelekea meli ya mv Victoria, wakati mwaka 2005 aliahidi lakini alishindwa kufanya hivyo, sasa ataweza?" alihoji Marando.

  Naye mgombea ubunge wa Jimbo la Kawe, Halima Mdee, alisema wakazi wa Segerea wanatakiwa kubadilika na kuchagua CHADEMA ili kuweza kuleta mabadiliko ya kweli bungeni na hata kwenye Wilaya ya Ilala.

  Alisema hata siku moja hakuna kiongozi anayeingia madarakani kwa fedha halafu akaweza kuwatumikia Watanzania vizuri, kwani ni lazima atafanya awezalo ili kuweza kururdisha fedha alizotumia.

  Aliwataka wakazi hao kuchukua fedha za wale wanaowania uongozi lakini siku ya uchaguzi Oktoba 31 wasiwape kura.

  Naye Mgombea ubunge wa jimbo hilo, Fred Mpendazoe, alisema CCM inatumia fedha zake nyingi hasa katika kura za maoni na hata kikiingia madarakani haiwezi kufanya kazi kwa umoja na mshikamano. Alisema kuwa Tanzania ni nchi tajiri, ina rasilimali za kutosha, lakini watu wake ni maskini kutokana na serikali iliyopo madarakani kutowajali wananchi wake, hivyo ni vyema wakazi wa Segerea kuikataa CCM kwa vitendo.

  Alisema utafiti unaonyesha zaidi ya wananchi milioni 13 hawapati milo mitatu na hiyo ni kwa ajili ya umaskini wa mafiga matatu ambayo CCM wamewalazimisha Watanzania kuwa nayo, huku wakiwa hawawapatii maendeleo wakazi hao.
   
 2. Njilembera

  Njilembera JF-Expert Member

  #2
  Sep 5, 2010
  Joined: May 10, 2008
  Messages: 1,423
  Likes Received: 154
  Trophy Points: 160
  Tanzania ni tajiri kuliko nchi yeyote Africa, takwimu wanazotupa ni za uongo. Hili nimeligundua baada ya kusikia na kuona jinsi nchi inavyoporwa. Wazungu wanaamini kabisa ni nchi pekee unayoweza kuitembelea ukiwa na tiketi, one way ticket na pesa kidogo ya kula kwa wiki chache na briefcase lakini utakarimiwa na utatoka katika muda usiozidi miaka miwili ukiwa mmilionea. Pamoja na hayo, bado utajiri wetu ni bado pale, lakini utaisha ndio maana tunahitaji viongozi waadilifu watupeleke nasi kwenye hali ya neema kama wenzetu!
   
Thread Status:
Not open for further replies.
Loading...