Dk. Shein: Maneno yao hayanisumbui, mimi ni Rais kwa mujibu wa Katiba

RobyMi

JF-Expert Member
Mar 4, 2012
848
863
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein amesema yeye hatishiki na maneno yanayosemwa dhidi yake na kusisitiza kuwa atabaki kuwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi kwa kuwa hakujiweka mwenyewe bali ni kwa mujibu wa Katiba na Sheria.

Nimeyasikia maneno yanayosemwa lakini hayanitishi nami nitaendelea kubaki kuwa Rais wa Zanzibar. Umri huu sitishiki tena na kama wao wana ubavu wa kikatiba wajaribu kuniondoa” Dk. Shein alisema wakati akizungumza na vijana wa Chama cha Mapinduzi (CCM) katika uwanja wa Maisara mjini Unguja jana.

Alibainisha kuwa Zanzibar inaongozwa kwa mujibu wa Katiba na Sheria wala si utashi wa mtummoja anayetaka kuongoza nchi na kwamba hakuna njia ya mkato katika hilo.

Katika mnasaba huo alieleza kuwa Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) ndio yeye mamlaka ya kisheria katika suala la uchaguzi hivyo vyama vyote havina budi kutii maamuzi yake likiwemo la kufuta uchaguzi wa tarehe 25 Oktoba 2015.

Tangazo la Tume la kufuta uchaguzi ni halali na limekuwa la kisheria baada ya kutangazwa katika gazeti rasmi la serikali hivyo sisi CCM tunasubiri Tume itangaze tarehe nyingine ya uchaguzi ili tushiriki” Dk. Shein alieleza.

Alibanisha kuwa kukubali au kukataa kushiriki katika uchaguzi wa marudio ni uamuzi wa kila chama hivyo kama wengine wataamua kutoshiriki huo utakuwa uamuzi wao binafsi wala CCM haiwezi kuwaingilia.

ZEC ndio yenye mamlaka yote sisi tutaridhia na wasipotaka hiyo ni hiari yao katika chama chao” Dk. Shein alisema huku akishangiliwa na vijana na wananchi waliohudhuria hafla hiyo.Aliongeza kuwa yamesemwa mengi kuhusu yeye na uchagazi na kwamba yeye naye anayo mengi ya kusema lakini atafanya hivyo wakati ukifika.

yako mengi yamesemwa na yanaendelea kusemwa nami ninayo mengi lakini nitasema siku ikifika na nitasema kweli siku hiyo ikifika” Dk. Shein alisisizitiza na kuonesha anayo mengi moyoni yanayomkereketa.

Kabla ya kuzungumza na vijana Dk. Shein ambaye aliambatana na Makamu wa Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan na Makamu wa Pili wa Rais
wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alipokea maandamano ya vijana hao kutoka mikoa ya Zanzibar na Tanzania bara.



Chanzo: Tovuti ya Ikulu Zanzibar
 
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein amesema yeye hatishiki na maneno yanayosemwa dhidi yake na kusisitiza kuwa atabaki kuwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi kwa kuwa hakujiweka mwenyewe bali ni kwa mujibu wa Katiba na Sheria.“Nimeyasikia maneno yanayosemwa lakini hayanitishi nami nitaendelea kubaki kuwa Rais wa Zanzibar.Umri huu sitishiki tena na kama wao wana ubavu wa kikatiba wajaribu kuniondoa” Dk. Shein alisema wakati akizungumza na vijana wa Chama cha Mapinduzi (CCM) katika uwanja wa Maisara mjini Unguja jana.


Alibainisha kuwa Zanzibar inaongozwa kwa mujibu wa Katiba na Sheria wala si utashi wa mtummoja anayetaka kuongoza nchi na kwamba hakuna njia ya mkato katika hilo.Katika mnasaba huo alieleza kuwa Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) ndio yeye mamlaka ya kisheria katika suala la uchaguzi hivyo vyama vyote havina budi kutii maamuzi yake likiwemo la kufuta uchaguzi wa tarehe 25 Oktoba 2015.

Tangazo la Tume la kufuta uchaguzi ni halali na limekuwa la kisheria baada ya kutangazwa katika gazeti rasmi la serikali hivyo sisi CCM tunasubiri Tume itangaze tarehe nyingine ya uchaguzi ili tushiriki” Dk. Shein alieleza.Alibanisha kuwa kukubali au kukataa kushiriki katika uchaguzi wa marudio ni uamuzi wa kila chama hivyo kama wengine wataamua kutoshiriki huo utakuwa uamuzi wao binafsi wala CCM haiwezi kuwaingilia.

ZEC ndio yenye mamlaka yote sisi tutaridhia na wasipotaka hiyo ni hiari yao katika chama chao” Dk. Shein alisema huku akishangiliwa na vijana na wananchi waliohudhuria hafla hiyo.Aliongeza kuwa yamesemwa mengi kuhusu yeye na uchagazi na kwamba yeye naye anayo mengi ya kusema lakini atafanya hivyo wakati ukifika.

yako mengi yamesemwa na yanaendelea kusemwa nami ninayo mengi lakini nitasema siku ikifika na nitasema kweli siku hiyo ikifika” Dk. Shein alisisizitiza na kuonesha anayo mengi moyoni yanayomkereketa.Kabla
ya kuzungumza na vijana Dk. Shein ambaye aliambatana na Makamu wa Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan na Makamu wa Pili wa Rais
wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alipokea maandamano ya vijana hao kutoka mikoa ya Zanzibar na Tanzania bara.


Source : Tovuti ya Ikulu Zanzibar
[M/mungu sio athumani kiroboto, kwa zulma hii atamlipa hapa hapa duniani, ni swala la muda tu.
quote my word, " malipo ni hapa hapa duniani, miaka 5 hatomaliza"
 
Huyu mzee nilikuwa namuona wa maana sana, hata sijui mdudu gani kamuingia..........
 
Sidhani kama kwa hali ilivyo hayo ni maneno yenye busara hata kidogo.

Na ni matamshi kama hayo ambayo huleta hasira kwa wananchi ambao wakoupande wa upinzani na viongozi wao pia.
 
muonekano wa shein ni dhahiri hapendi kuendelea na uongozi ila ndo ivo kaambiwa avumilie na wenyewe.
 
Suala si kutishika na maneno ama kukalia kiti kwa mujibu wa katiba, sheria nk. Suala ni kuwa na busara na kuangalia hatma ya taifa. Kung'ang'ania madaraka huku ukijua kwamba kunaweza kuhatarisha maisha ya wananchi wa taifa lako si hekima wala busara. Mimi nadhani Dr. Shein angejijengea heshima kubwa nchini na nje ya nchi kama angeamua kuachia madaraka ili kusaidia kuleta mwafaka ktk mvutano na mzozo wa Zanzibar.
 
Shein ana kiburi cha kawaida kwa mwanaadamu hasa unapoona nyuma yako pana AK 47, vifaru naajeshi yanayomlinda hata akienda uani !! Lakini anakosa kitu kimoja kikubwa anajua zaidi ya 60 percent ya wananchi wake hawampendi na jambo hilo lazima imsumbue na hawezi kuwa na amani na wananchi wake.

Angejifunza kwa wale waliojaribu kupora madaraka kwa mlango wa nyuma waliishiaje ???????????????!!
 
By the time akistuka ameshapoteza sana.Lakini kinachoisumbua CCM na Shein ni UTAWALA.Ona leo Wapinzani wanavyofanyiwa ndani ya bunge unadhani ni rahisi kutoa madaraka??? Fikiria pesa zikizotumika kuhonga ili tu wabunge wa CCM na rais spite,je huo siyo uwoga???
 
Nawazia baada ya tarehe 20 March 2016.Matokeo yote watakuwa yamekwisha kuhesabiwa na kutangaza tarehe 21 March 2016.Na rais ataapishwa tarehe 22 March 2016 nikiwa na jeshi kila mahali.Magazeti,TBC1,Star TV,TBC2,ZBC na ZTV zitasema hivi:CCM yashinda kwa kishindo Z'bar. CCM kidume,Machotara warudi kwao.
Na Pili Wapemba wajiandae kuondoka Unguja.Kama hamuamini mtaniambia.Kipindi cha sasa hivi kutakuwa ni mtoto.Cha baada ya Uchaguzi mtarudi Pemba ndugu zangu.Andaeni maeneo yenu msije mkashtukizwa.
 
Back
Top Bottom