Dk. Shein ajitetea, Asema ushindi wake ni halali

Mwanahabari Huru

JF-Expert Member
Joined
Mar 9, 2015
Posts
14,242
Reaction score
34,917
DK. Ali Mohamed Shein, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi visiwani humo amejitetea kwamba ushindi wake ni halali,anaandika Regina Mkonde.

Akizungumza kwenye Maadhimisho yaSiku ya Mashujaa iliyofanyika Dodoma jana, Dk. Shein amesema wapo wanaolalamikia ushindi wake na kwamba, licha ya malalamiko hayo ataendelea kufanya kazi kwa amani na Rais John Magufuli.

Hata hivyo amepiga kijembe kwamba, kelele za mlangoni hazimzuii mwenye nyumba kulala. Ingawa hakutaja moja kwa moja jina la Maalim Seif Sharif Hamad lakini bila shaka kauli hiyo inamlenga yeye (Maalim Seif) ambaye amekuwa akilalamikia kupokwa ushindi wake na kiongozi huyo wa CCM.

Safari za kutafuta haki nje ya nchi za Maalim Seif, Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF) pia aliyekuwa mgombea urais visiwani humo katika uchaguzi mkuu wa mwaka jana zinaonekana kuitia kiwewe CCM Zanzibar.

CCM visiwani Zanzibar imekuwa ikitoa matamko makali ikiwa ni pamoja na kutaka Maalim Seif akamatwe kwa madai ya kufanya uchochezi.

Baada ya kufutwa matokeo ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka jana na kurudiwa tarehe 20 Machi mwaka huu, Maalim Seif amekuwa akiilalamikia Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) kupoka ushindi wake na kumtunuku Dk. Shein.

Ndani ya nchi na katika jumuiya za kimataifa Maalim Seif amekuwa akitaka Serikali ya Dk. Shein isipewe ushirikiano wowote kwa madai ya kunyonga demokrasia.

Hata hivyo, zaidi ya mara moja Maalim Seif amekuwa akisema yeye ndiye mshindi na kwamba Wazanzibari wanatambua hivyo.

Pia amekuwa akisema ataendelea kudai haki yake ya ushindi wa uchaguzi mkuu wa tarehe 20 Oktoba mwaka jana kwa njia ya amani.
 
Majizi Chadema waliwadanganya wenzao cuf wasusie uchaguzi,

Hii ndio hasara ya kufuata ushauri Wa watu Wenye elimu ya hapa na pale
 
Akajitetee ICC....sisi hatuna msaada naye.
ICC haya tusubiri,labda tuanze na ICJ ilianzia wapi na ikaishia wapi vile ndugu??alishinda kesi kenyatta sembuse shein??mpaka sasa ICC wanahaha kumkamata rais wa sudan wameshindwa sembuse shein??rais wa burundi anafanya atakavyo sembuse shein??kuweni serious saa nyingine msitegee kila kitu kutoka kwa hao wazungu mambo mengine tuhimizane humu kwa humu kwetu kama kupambana tupambane humuhumu mpaka kieleweke,huku nchi za wazungu hamna kitu ni porojo tu hizi...............
 
Huyu Mzee akae atulie kwakuwa hadi watoto wa chekechea wanajua bao la bafuni la mkono alilojikakamaa hadharani huyu Mzee.
 
Ni mbaya sana kuongea kitu cha uongo huku dhamira ya ndani inakusuta..
 
Mbona naweweseka .mlango ukifanya kelele kisawaaawa huwezi ukalala .usingizi ndio hivo unaanza kumruka
 
Mbona kila siku maneno hayo tu anakosa vipi kujamini..!?
 
DK. Ali Mohamed Shein, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi visiwani humo amejitetea kwamba ushindi wake ni halali,anaandika Regina Mkonde.

Akizungumza kwenye Maadhimisho yaSiku ya Mashujaa iliyofanyika Dodoma jana, Dk. Shein amesema wapo wanaolalamikia ushindi wake na kwamba, licha ya malalamiko hayo ataendelea kufanya kazi kwa amani na Rais John Magufuli.

Hata hivyo amepiga kijembe kwamba, kelele za mlangoni hazimzuii mwenye nyumba kulala. Ingawa hakutaja moja kwa moja jina la Maalim Seif Sharif Hamad lakini bila shaka kauli hiyo inamlenga yeye (Maalim Seif) ambaye amekuwa akilalamikia kupokwa ushindi wake na kiongozi huyo wa CCM.

Safari za kutafuta haki nje ya nchi za Maalim Seif, Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF) pia aliyekuwa mgombea urais visiwani humo katika uchaguzi mkuu wa mwaka jana zinaonekana kuitia kiwewe CCM Zanzibar.

CCM visiwani Zanzibar imekuwa ikitoa matamko makali ikiwa ni pamoja na kutaka Maalim Seif akamatwe kwa madai ya kufanya uchochezi.

Baada ya kufutwa matokeo ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka jana na kurudiwa tarehe 20 Machi mwaka huu, Maalim Seif amekuwa akiilalamikia Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) kupoka ushindi wake na kumtunuku Dk. Shein.

Ndani ya nchi na katika jumuiya za kimataifa Maalim Seif amekuwa akitaka Serikali ya Dk. Shein isipewe ushirikiano wowote kwa madai ya kunyonga demokrasia.

Hata hivyo, zaidi ya mara moja Maalim Seif amekuwa akisema yeye ndiye mshindi na kwamba Wazanzibari wanatambua hivyo.

Pia amekuwa akisema ataendelea kudai haki yake ya ushindi wa uchaguzi mkuu wa tarehe 20 Oktoba mwaka jana kwa njia ya amani.
Mkuu kwa mawazo yako ulitegemea aseme nini?
 
Back
Top Bottom