Dk. Philip Mpango: Bajeti ijayo itatekelezwa kwa fedha za ndani

MsemajiUkweli

JF-Expert Member
Jul 5, 2012
13,171
23,991
Serikali imesema bajeti ya mwaka ujao, hususani utekelezaji wa miradi yote ya maendeleo, itatekelezwa kwa fedha za ndani.

Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Philip Mpango alisema miradi mikubwa kama vile ujenzi wa reli ya kisasa ya kati na miradi mingine mikubwa, ndiyo itajengwa kwa fedha za msaada kutoka nje kwa kuwa nchi haiwezi kukwepa kuomba msaada kutoka nje.

Alisema hayo jana katika mji mdogo wa Holili mpakani mwa Tanzania na Kenya, baada ya kuangalia shughuli za utendaji kazi katika mpaka huo na baadaye kuzungumza na wafanyakazi wa Mamlaka ya Mapato (TRA) katika mji huo.

Alisema makusanyo ya sasa ya Sh trilioni 1.7 kwa mwezi yanayokusanywa kwa sasa nchi nzima, fedha zake zitaelekezwa kwa shughuli za maendeleo kwa mikoa yote nchini. Waziri huyo alisema si kweli kwamba serikali ya Rais John Magufuli haitahitaji msaada wa fedha kutoka nje. “…la hasha! ila msaada huo hautakuwa mkubwa kama zamani,” alisema waziri.

Akizungumzia bajeti ijayo, alisema fedha zake nyingi zitatokana na makusanyo ya fedha za ndani na sio za msaada kutoka nje. Waziri huyo alisema kwa asilimia kubwa bajeti ya miradi ya maendeleo katika mikoa yote nchini, fedha zake zitakuwa ni za ndani zilizokusanywa na kiasi kidogo cha fedha kitatoka nje.

Aliwataka watumishi wote wa umma, wanaokusanya mapato katika maduhuli ya serikali, kuacha mara moja kushika na kukusanya fedha kizamani kwa kutumia stakabadhi na kuandika kwa mkono ili kuepuka ushawishi wa kutumia fedha hizo kwa njia isiyokuwa halali.

Alisema anasikitishwa na utaratibu wa ofisa uhamiaji wa kitengo viza cha mji wa Holili, kukaa na fedha zaidi ya siku tano na kutoa stakabadhi kwa mkono.

Waziri alikemea na kumtaka ofisa wa uhamiaji wa mji wa Holili, kuacha mara moja kukaa na fedha za serikali kwa zaidi ya wiki, tofauti na mtunza fedha wa TRA anayepeleka fedha benki kila siku. Alisema utaratibu huo ulishapigwa marufuku miaka mitatu iliyopita, lakini nasikitika unaendelea katika mji wa Holili. Alimwagiza Mkuu wa Uhamiaji Mkoa wa Kilimanjaro, kubadilisha hali hiyo kwa maslahi ya serikali.

Akizungumzia uadilifu, Waziri Mpango aliwataka wafanyakazi wa TRA, kuacha kufanya kazi hiyo kwa kuwanyanyasa wafanyabiashara, kwani kufanya hivyo ni kosa kisheria. Alisema uadilifu si wa mali tu, bali uko pia katika kutenda kazi za kila siku.

Alisema pia wananchi wanapaswa kulipa kodi kwa kufurahia na kuona kodi wanayolipa inawanufaisha, ikiwa ni pamoja na kufanya maendeleo katika miradi mbalimbali.

Chanzo: Habarileo
 
Unaweza ukawa na nchi huru bila ya watu kuwa huru, kwa maana kwamba hawana uwezo wa kujiamulia mambo yao wenyewe. Ingawa nchi yao ni huru, lakini bado wanajikuta kwamba kuna kundi au tabaka dogo la watu wanaowatawala na kufanya maamuzi kwa niaba yao au kwa ajili ya waliowengi.

Katika nchi yetu iliyo huru, tabaka-tawala la ndani limekuwa bado chini ya himaya ya ubeberu na kwa hiyo watawala wetu wanakuwa vibaraka wa matabaka-tawala ya kibeberu.

Hali hii inasababisha, sio tu tabaka-tawala la ndani kuwa tegemezi, lakini hata nchi yetu inakuwa tegemezi kwa sababu inakosa uongozi unaojitegemea na kufanya maamuzi kwa manufaa na maslahi ya watu wake.

Tunakoelekea kwa sasa chini ya serikali ya Rais Magufuli kunatoa nuru na matumaini zaidi ya kupata taifa linalojitegemea na kujiamulia mambo yake lenyewe bila kutegemea misaada ya fikra na pesa kutoka mabeberu wa nchi za Magharibi.

As a Nation, We can do it!

Pole pole ndio mwendo!
 
kwa mtazamo wangu ni bora tujibane wenyewe na kupunguza anasa katika matumizi yetu kuliko kutegemea nje...
 
Alisema makusanyo ya sasa ya Sh trilioni 1.7 kwa mwezi yanayokusanywa kwa sasa nchi nzima, fedha zake zitaelekezwa kwa shughuli za maendeleo kwa mikoa yote nchini. Waziri huyo alisema si kweli kwamba serikali ya Rais John Magufuli haitahitaji msaada wa fedha kutoka nje. “…la hasha! ila msaada huo hautakuwa mkubwa kama zamani,” alisema waziri.
Huyu Mwandishi na Mhariri wa Habari Leo inaelekea ni kilaza sana kwenye namba! TRA wamekusanya Trilion Moja na Bilioni 79 (1.079) lakini Habari Leo tangu juzi wamekuwa wakiripoti kwamba mapato ya mwezi uliopita ni Sh. Trilion Moja na Bilion 790 (1.79)... ongezeko la 73% ya mapato halisi!

Kuhusu misaada/mikopo ya nje; watu tulishaongea tangu zamani there's no way eti tunaweza kujitosheleza wenyewe kwenye bajeti at least for the next 3-5 years. Ukiangalia trend ya makusanyo, bado hatuna base yoyote ya kutuwezesha kukusanya japo Trilion 1.5 steadily.... most likely tutakuwa tunacheza between TSh. 900 Billion to 1.2 Trillion. Hapo hata ukichanganya na mapato yasiyokuwa ya kodi, bado hatutakuwa na uwezo wa kuwa na mapato angalau ya TZS 20 Trillion kwa mwaka! Lakini hata kama tunakuwa na huo uwezo bado TZS 20 Trillion ni pesa ndogo sana kwa nchi kubwa na maskini kama hii ambayo ina changamoto kwenye sekta zote! Infact, hata bajeti ya TZS 50 Trillion ambayo inakuwa fully funded (sio hizi za Trilion 15 lakini hata hiyo 15 yenyewe inakuwa kwenye makaratai tu) bado ni ndogo sana kwa nchi Tanzania!

Kwa hili naisifu serikali ya Magufuli manake hawakuta kuleta unafiki wa kisiasa kwamba bajeti yao itakuwa 100% kwa pesa za ndani. Sio kwamba hawawezi... politically katika kutaka kuwahadaa watu kwamba wanaweza they can do it but that's not an issue--- issue ni kwa kiasi gani unaweza kutatua changamoto zilizopo kwa pesa zako za ndani! Unaweza kwa makusudi ukasema bajeti yetu mwaka huu ni TZS 12 Trillion ambayo ni 100% from domestic sources! Issue inayofuata hapo ni kwa kiasi gani changamoto zilizopo zinaweza kutatuliwa kwa hiyo 12 Trillion.
 
Marekani ndiye mkopaji mkubwa kwa serikali ya uchina....ilimbidi kuuza bond china maana marekani ulaya alikosa wanunuzi.....mkopo ni lazima ila kwa miradi ya maendeleo kama barabara,reli nk.

Kukopa kuna faida pale tu unapoutumia mkopo kuzalisha bidhaa na kuuza ili uweze kulipa deni; lakini unapokopa halafu mkopo unautumia kwenda kubembea Marekani au kulipia mishahara wafanyakazi, unakuwa ni muhujumu uchumi wa nchi!!!

Marekani wanaweza kukopa na wasiwe na shida kwani ikibidi wataprint $$$$$; sisi hatuna advantage hiyo!!
 
Sisi watanzania hatutaisha kulalamika, na nchi ujengwa na wsnanchi ndio maana kama taifa lazima kuwe na raslimali watu. Unakuta mtu anakwenda kununua kitu cha laki moja na kwenye rist anaandikiwa elfu kumi . Alafu kesho unakuja kulalamika
 
Magufuli na waziri wake Mpango hawana njia za mkato zaidi ya kutanua Tax Base. Kuna watu wanapangisha nyumba kwa kodi kubwa na hata kodi ndogo serikali hairambi hata shilingi moja. Mfano Sinza na Magomeni zaidi ya nusu ya nyumba zimepangishwa lakini serikali haipati kodi. Kwenye nyumba za kulala wageni, lodge na mahoteli wamiliki wanatia hela yote mfukoni hawana EFD, kuna wamiliki wa viwanja kodi wanalipa halmashauri zinaliwa. Then awabane majambazi wa kwenye madini.
Ukikusanya trilioni mbili kwa mwezi kinachofuata na kutukana wazungu tu maana hawana maana tena
 
Huyu Mwandishi na Mhariri wa Habari Leo inaelekea ni kilaza sana kwenye namba! TRA wamekusanya Trilion Moja na Bilioni 79 (1.079) lakini Habari Leo tangu juzi wamekuwa wakiripoti kwamba mapato ya mwezi uliopita ni Sh. Trilion Moja na Bilion 790 (1.79)... ongezeko la 73% ya mapato halisi!

Kuhusu misaada ya nje; watu tulishaongea tangu zamani there's no way eti tunaweza kujitosheleza wenyewe kwenye bajeti at least for the next 3-5 years. Ukiangalia trend ya makusanyo, bado hatuna base yoyote ya kutuwezesha kukusanya japo Trilion 1.5 steadily.... most likely tutakuwa tunacheza between TSh. 900 Billion to 1.2 Trillion. Hapo hata ukichanganya na mapato yasiyokuwa ya kodi, bado hatutakuwa na uwezo wa kuwa na mapato angalau ya TZS 20 Trillion kwa mwaka! Lakini hata kama tunakuwa na huo uwezo bado TZS 20 Trillion ni pesa ndogo sana kwa nchi kubwa na maskini kama hii ambayo ina changamoto kwenye sekta zote! Infact, hata bajeti ya TZS 50 Trillion ambayo inakuwa fully funded (sio hizi za Trilion 15 lakini hata hiyo 15 yenyewe inakuwa kwenye makaratai tu) bado ni ndogo sana kwa nchi Tanzania!

Kwa hili naisifu serikali ya Magufuli manake hawakuta kuleta unafiki wa kisiasa kwamba bajeti yao itakuwa 100% kwa pesa za ndani. Sio kwamba hawawezi... politically katika kutaka kuwahadaa watu kwamba wanaweza they can do it but that's not an issue--- issue ni kwa kiasi gani unaweza kutatua changamoto zilizopo kwa pesa zako za ndani! Unaweza kwa makusudi ukasema bajeti yetu mwaka huu ni TZS 12 Trillion ambayo ni 100% from domestic sources! Issue inayofuata hapo ni kwa kiasi gani changamoto zilizopo zinaweza kutatuliwa kwa hiyo 12 Trillion.
Thats true
 
Wamenyimwa mikopo kutokana na suala la ccm kupora ushindi wa wazanzibari na cuf, sasa wanadai bajeti itatokana na hela za ndani. Yaani Hawa jamaa wanatuona watanzania wote ni zero
 
Mtauona ni muujiza lakini JPM ni moto. Hayo ya zanzibar ni yenu Manyumbu.
 
Serikali imesema bajeti ya mwaka ujao, hususani utekelezaji wa miradi yote ya maendeleo, itatekelezwa kwa fedha za ndani.

Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Philip Mpango alisema miradi mikubwa kama vile ujenzi wa reli ya kisasa ya kati na miradi mingine mikubwa, ndiyo itajengwa kwa fedha za msaada kutoka nje kwa kuwa nchi haiwezi kukwepa kuomba msaada kutoka nje.

Alisema hayo jana katika mji mdogo wa Holili mpakani mwa Tanzania na Kenya, baada ya kuangalia shughuli za utendaji kazi katika mpaka huo na baadaye kuzungumza na wafanyakazi wa Mamlaka ya Mapato (TRA) katika mji huo.

Alisema makusanyo ya sasa ya Sh trilioni 1.7 kwa mwezi yanayokusanywa kwa sasa nchi nzima, fedha zake zitaelekezwa kwa shughuli za maendeleo kwa mikoa yote nchini. Waziri huyo alisema si kweli kwamba serikali ya Rais John Magufuli haitahitaji msaada wa fedha kutoka nje. “…la hasha! ila msaada huo hautakuwa mkubwa kama zamani,” alisema waziri.

Akizungumzia bajeti ijayo, alisema fedha zake nyingi zitatokana na makusanyo ya fedha za ndani na sio za msaada kutoka nje. Waziri huyo alisema kwa asilimia kubwa bajeti ya miradi ya maendeleo katika mikoa yote nchini, fedha zake zitakuwa ni za ndani zilizokusanywa na kiasi kidogo cha fedha kitatoka nje.

Aliwataka watumishi wote wa umma, wanaokusanya mapato katika maduhuli ya serikali, kuacha mara moja kushika na kukusanya fedha kizamani kwa kutumia stakabadhi na kuandika kwa mkono ili kuepuka ushawishi wa kutumia fedha hizo kwa njia isiyokuwa halali.

Alisema anasikitishwa na utaratibu wa ofisa uhamiaji wa kitengo viza cha mji wa Holili, kukaa na fedha zaidi ya siku tano na kutoa stakabadhi kwa mkono.

Waziri alikemea na kumtaka ofisa wa uhamiaji wa mji wa Holili, kuacha mara moja kukaa na fedha za serikali kwa zaidi ya wiki, tofauti na mtunza fedha wa TRA anayepeleka fedha benki kila siku. Alisema utaratibu huo ulishapigwa marufuku miaka mitatu iliyopita, lakini nasikitika unaendelea katika mji wa Holili. Alimwagiza Mkuu wa Uhamiaji Mkoa wa Kilimanjaro, kubadilisha hali hiyo kwa maslahi ya serikali.

Akizungumzia uadilifu, Waziri Mpango aliwataka wafanyakazi wa TRA, kuacha kufanya kazi hiyo kwa kuwanyanyasa wafanyabiashara, kwani kufanya hivyo ni kosa kisheria. Alisema uadilifu si wa mali tu, bali uko pia katika kutenda kazi za kila siku.

Alisema pia wananchi wanapaswa kulipa kodi kwa kufurahia na kuona kodi wanayolipa inawanufaisha, ikiwa ni pamoja na kufanya maendeleo katika miradi mbalimbali.
Chanzo:Habarileo
Wacha kujidanganya au kuendelea kudanganywa kijana
 
Unaweza ukawa na nchi huru bila ya watu kuwa huru, kwa maana kwamba hawana uwezo wa kujiamulia mambo yao wenyewe. Ingawa nchi yao ni huru, lakini bado wanajikuta kwamba kuna kundi au tabaka dogo la watu wanaowatawala na kufanya maamuzi kwa niaba yao au kwa ajili ya waliowengi.

Katika nchi yetu iliyo huru, tabaka-tawala la ndani limekuwa bado chini ya himaya ya ubeberu na kwa hiyo watawala wetu wanakuwa vibaraka wa matabaka-tawala ya kibeberu.

Hali hii inasababisha, sio tu tabaka-tawala la ndani kuwa tegemezi, lakini hata nchi yetu inakuwa tegemezi kwa sababu inakosa uongozi unaojitegemea na kufanya maamuzi kwa manufaa na maslahi ya watu wake.

Tunakoelekea kwa sasa chini ya serikali ya Rais Magufuli kunatoa nuru na matumaini zaidi ya kupata taifa linalojitegemea na kujiamulia mambo yake lenyewe bila kutegemea misaada ya fikra na pesa kutoka mabeberu wa nchi za Magharibi.

As a Nation, We can do it!

Pole pole ndio mwendo!
Ndoto za alinacha au Abunuas
 
Back
Top Bottom