Dk Mahanga matatani tena, mahakama yaamuru akamatwe

jacobinho

Member
Feb 10, 2017
6
12
Amri hiyo ilitolewa na Naibu Msajili wa Wilaya, Mahakama Kuu, Ruth Masambu wiki iliyopita baada ya Dk Mahanga kushindwa kufika mahakamani hapo bila taarifa.

Dar es Salaam. Aliyekuwa Naibu Waziri wa Kazi, Ajira na Maendeleo ya Vijana katika Serikali ya Awamu ya Nne, Dk Makongoro Mahanga ameingia matatani tena baada ya Mahakama Kuu kuamuru akamatwe na kufikishwa mahakamani hapo.

Amri hiyo ilitolewa na Naibu Msajili wa Wilaya, Mahakama Kuu, Ruth Masambu wiki iliyopita baada ya Dk Mahanga kushindwa kufika mahakamani hapo bila taarifa.

Dk Mahanga ambaye alikuwa mbunge wa Ukonga na baadaye Segerea kwa tiketi ya CCM, alitakiwa kufika mahakamani hapo Alhamisi iliyopita ili kulipa Sh2 milioni, ikiwa ni sehemu ya deni la zaidi ya Sh11 milioni anazodaiwa.

Mwanasiasa huyo ambaye sasa ni kada wa Chadema, anadaiwa kiasi hicho na mwanaharakati wa haki za binadamu, Kainerugaba Msemakweli ikiwa ni gharama alizozitumia katika kesi ya madai ya kashfa iliyofunguliwa dhidi yake na Dk Mahanga.

Dk Mahanga alifungua kesi ya madai namba 145 ya mwaka 2009 akidai kuwa kitabu alichoandika mwanaharakati huyo cha “Orodha ya Mafisadi wa Elimu Tanzania” kikimtaja kuwa ni mmoja wa vigogo wenye shahada za udaktari wa falsafa za kughushi, kilimdhalilisha.

Hata hivyo, kesi hiyo ilifutwa Julai Mosi, 2014 kutokana na Mahanga na mawakili wake kutofika mahakamani mara kwa mara.
 
Uwii na huyu aweke vyeti mezani
Avipate wapi? aliandikwa kwenye kitabu, akafungua kesi akifikiri Msemaukweli atakimbia kumbe alikuwa na ushahidi wote. Makongoro Mahanga na mawakili wake wakakimbia kesi waliyofungua wenyewe. Sasa anafikiri hiyo hela hatailipa kwa kuikimbia tena. Akalipe mambo yaishe
 
Uwii na huyu aweke vyeti mezani
yes huyu arudishe degree feki kwa waliomuuzia na awache kujiita dr. ndio maana wengi wenye Phd siku hizi hawajiiti dr so and so kwani hata waganga wa kienyeji wanajiita dr.
 
Povu la nini sasa ninyi wanaume tulizeni Mshono kwani Mahanga kachukua jina la mtu ?? Hata Kama PhD haiko sawa , si Kama Bashite kilaza kuanzia Primary
Apelekwe mahakamani haraka swala la kufoji halina chadema wala ccm kote wapo wakamatwe wapelekwe faster
 
Mjadala huu CHADEMA wanachungulia na kusepa
Ahhaah mkuu hata kule kwingine ulikuwa unachungulia na kusepa.

Mambo haya sio ya mchezo mchezo ila hii ujue ni zao la ccm hata kama yupo wapi kwa sasa
 
Mjadala huu CHADEMA wanachungulia na kusepa
Alikuwa ccm
Na uwaziri mkampa.
66f4dc15f4bf5c6cd88971a933368805.jpg
 
Back
Top Bottom