Mkuu Pinda hatumsakami kwa kuwa siyo mgombea, Lowasa yeye ni mgombea. Pia taarifa zinasema Baraza la mawaziri lilitoa maamuzi mchakato wa zabuni uendelee ila uzingatie sheria, halafu mheshimiwa hakuzingatia sheria, sawa na mwanao kumtuma akakununulie gazeti halafu yeye akaamua kununua pipi, hapo kosa ni la mzazi au la mtoto?
Kwanza suala hapa ni uadilifu, na kama kigezo mnachokitumia cha kuwa Waziri Mkuu basi kitumike kwa wote.
Pili unadai habari zinasema zipi? Kwa kauli ya Lowassa amesema baada ya magazeti kuandika kuhusu Richmond kuwa kampuni hewa aliitisha kikao cha makatibu wakuu wa wizara husika na kutaka kuuvunja mkataba huu, katibu mkuu kiongozi ambaye ni mteule wa Rais alitoka nje na baada ya muda akarudi na kusema mamlaka ya juu ilitoa maagizo kuwa mkataba wa Richmond usainiwe kama kawaida.
Kama ilichukua siku moja kwa kurugenzi ya habari ya ikulu kujibu madai ya Mengi alipodai Zitto na ikulu watamshughulikia kwa nini hili limewatia kigugumizi? Nilikuuliza nani ni Mwenyekiti wa baraza la mawaziri?
Sawa tutoke huko baada ya Lowassa kujiuzulu Richmond ilikuwa haijalipwa hata senti moja, so ni nani mwenye madaraka ambaye ali engineer kuhamisha umiliki kutoka Richmond kwenda Dowans? Na ni nani aliyehakikisha Dowans ianzekulipwa mabilioni? Maana Lowassa alikuwa nje ya serikali.
Ni nani aliyehakikisha kuwa serikali inashindwa kesi katika mahakama ya usuluhishi wa kibiashara ili Dowans kwa mkataba feki ilipwe mabilioni na serikali yetu hela za walipa kodi?
Nani aliyekataa ushauri wa Zitto kabwe wa kutaifisha mitambo ya kampuni feki ya Richmond /Dowans?
Nani aliyehakikisha Rais Obama wakati anaitembelea Tanzania anaitembelea mitambo ya Dowans? Unaweza ukajua mujibu sahihi ila kuipenda CCM ni kama vile uchawi, mchawi ukimwambia kula nyama za watu dhambi hawezi acha badala yake atakuroga akuangamize licha ya kujua ni dhambi.
Nadhani kuna uhusiano kati ya shetani na CCM,