naunga mkono .
kuna mengi ya kujifunza huko maana miaka michache iliyopita tulikuwa tunafanana kiasi vitu vingi.
ila hawa jamaa tuwe nao makini wako informed sana kuhusu resource zetu na udhaifu naubinafsi wa wengi wanaozisamia. ndio maana viatell maengineer wanakuwa treated kama vibarua.
umakini mkubwa inahitajika katika kujenga urafiki na hawa ndugu maana wao wanakimbia wakati sisi tunatambaa kimaamuzi na maadili. huku msingi mkuu wa maadili katiba umekwapuliwa na wabinafsi wachache ili nchi iendelee kuwa na matobo yanayovujisha mali zetu.
Sasa serikali ya awamu hii iende hatua nyingine.
Majipu iwe ni suala endelevu.hakuna haja ya kuendelea kuishi maisha ya kuviziana.uendeshaji wa shughuli za kisekta ziendelee,na taratibu za kushughulikia matatizo.
Fedha sasa inakusanywa vizuri,na hatua za ubunifu wa vyanzo vya mapato ufanyike.
Viongozi wajielekeze kwenye kutafuta maendeleo,maana viongozi wamekuwa waoga wanajikuta muda mwingi wanafanya maigizo ili kutaka sifa kwa wananchi kama tunavyoshuhudia kwenye vyombo vya habari.
Kama agenda ni viwanda,tulikuwa navyo,sasa jitihada za kufufua au kufuatilia viwanda vilivyobinafsishwa na havifanyi kazi tuone hatua zilizochukuliwa.
Ushawishi wa Serikali kwa uanzishwaji wa viwanda bado hakuna jitihada zinzoonekana.
Mikoa mingi maeneo hayajapimwa ili kubainisha maeneo ya viwanda.
Ili tuweze kuwafikia wenzetu au kushindana itabidi sasa tukubali kujifunza kutoka kwao.
Naona umuhimu wa safari za kwenda kujifunza nje kwa wenzetu .
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.