dubu
JF-Expert Member
- Oct 18, 2011
- 3,502
- 3,483
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Ustawi wa Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dk Kigwangalla, kumsomesha Getrude Clement kidato cha tano na cha sita kwenye shule za kisasa
"Huyu binti anaitwa Getrude Clement. Anatokea Jiji la Mwanza, nchini Tanzania. Alipata fursa ya kipekee kuongea kwenye Mkutano wa Umoja wa Mataifa, akikaribishwa na Mhe. Ban Ki Moon, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kama muwakilishi wa watoto na vijana wote duniani. Ana umri wa miaka kumi na sita.
Leo alikaribishwa kuongea kwenye kikao cha wabunge watetezi wa haki za watoto, alitoa hotuba iliyowatoa watu machozi. Baba yake ni kinyozi na mama yake ni mfanyabiashara mdogo mdogo wa nyanya na vitunguu, na yeye anasoma kidato cha tatu, shule ya sekondari Mnarani (shule ya sekondari ya kata).
Kwa kuthamini kipaji chake na mchango wake, na kutambua nafasi yangu kama Naibu Waziri kwenye Wizara inayosimamia mambo ya Watoto, na kama Mbunge na Mzazi wa mabinti, lakini zaidi kama mtu kutoka kwenye background ya maisha ya chini na ninayethamini mchango wa elimu kwenye maisha yangu, nimeamua kujitolea kumsomesha kidato cha tano na cha sita kwenye shule za kisasa.
Taasisi yangu ya misaada ya kijamii ya Hamisi Kigwangalla Development Foundation itamlipia ada za masomo yake ya high school."
Kujua Mtoto huyu aliongea nini UN, soma=>Mtoto Mtanzania wa miaka 16 alivyoongea kwa kujiamini mbele ya viongozi wa dunia umoja wa mataifa