Dk. Kigwangalla azindua rasmi huduma za CHF iliyoboreshwa (ICHF) Wilayani Babati-Manyara

kalulukalunde

JF-Expert Member
May 27, 2016
1,056
1,083
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dk. Hamisi Kigwangalla mapema leo Julai 11.2016 amezindua rasmi huduma za Afya za CHF iliyoboreshwa katika Wilaya ya Babati, Mkoani Manyara ambapo amewaagiza watendaji wa Serikali wakiwemo Maafisa wa Ustawi wa Jamii,

Walimu, Watendaji wa Serikali Kata, vijiji na Maafisa Maendeleo kuhakikisha wanasimamia zoezi la kuhamasisha wananchi wanachangamkia furza za kujiunga na mfuko huo haraka katika kuboresha afya za wananchi wote.

Dk. Kigwangalla ambaye alikuwa mgeni rasmi, amesema hayo katika Mji wa Bashnet ambao upo katika Wilaya hiyo ya Babati, Mkoani hapa.

“Natoa maagizo kwa watendaji wote kuhakikisha munausaidia kutoa taarifa sahihi ili wananchi wapate kujiunga na huduma hii ya ICHF. Na pia sitaki kusikia kama wananchi waliojiunga na hudua hii ya CHF iliyoboreshwa wanakosa dawa ama huduma huko Mahospitali ama kituo chochote cha Afya, ikibainika Serikali itachukua hatua kali.

Aidha. Watendaji wote wakiwemo muliopo kwa jamii huko, muhakikishe munahamasisha na kuwaingiza wananchi wote kwenye mfuko huu. Natoa miezi sita kwa Maafisa wa Ustawi wa Jamii, Maafisa Maendeleo, Watendaji wa Serikali za Vijiji, na Maafisa wengine wote nitakaporejea hapa baada ya miezi sita nikute huduma hii ya CHF iliyoboreshwa imekuwa kubwa na wananchi wengi wamejiunga na endapo kwenye eneo lako limekuwa la mwisho basi hatua kali zitachukuliwa dhidi yako” alieleza Dk. Kigwangalla.

Katika tukio hilo, lililofanyika katika viwanja vya minada vya Bashnet-Babati, Dk. Kigwangalla alipata wasaha wa kukabidhi vitendea kazi ikiwemo Pikipiki kadhaa kwa watendaji ambao watakuwa wakitoa huduma hizo za CHF iliyoboreshwa, ambapo pia alikabidhi kadi kwa wanachama waliojiunga papo hapo.

Katika shughuli hizo ambazo zimeratibiwa na Shirika la Kimataifa la PHARMA ACCESS, pia Dk. Kigwangalla aliweza kuzindua kituo cha Afya kilichofanyiwa ukarabati mkubwa na shirika hilo katika kituo cha Afya cha Dongobesh.

Mbali na kuzindua kituo hicho cha Afya cha Dongobesh kilichofanyiwa ukarabati mkubwa na PHARMA ACCESS, Dk. Kigwangalla pia aliweza kuweka jiwe la msingi katika jengo la chumba cha upasuaji wa kituo hicho ambapo alitoa miezi sita kwa Afisa Tawala wa Wilaya kuhakikisha wanakamilisha jengo hilo la chumba cha upasuaji.

DSC_0001.jpg
Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Dk Joel Bendera akizungumza wakati wa tukio hilo la uzinduzi wa huduma za CHF iliyoboreshwa (ICHF) iliyofanyika Wilayani Babati, Mkoani Manyara


DSC_0009.jpg
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dk. Hamisi Kigwangalla akihutubia wakati wa uzinduzi wa huduma za CHF iliyoboreshwa (ICHF) iliyoratibiwa na Shirika la Kimataifa la PHARMA ACCESS. Tukio hilo limefanyika mapema leo Julai 11.2016, Wilayani Babati katika mji wa Bashnet.


DSC_0035.jpg


Baadhi ya watendaji wa Serikali katika Miji na Vijiji pamoja na maafisa Ustawi wa jamii wakiwa mbele baada ya Dk. Kigwangalla kuwaita mbele haapo na kisha kuwapa angalizo la miezi sita wawe wamesimamia vizuri mradi huo

DSC_0025-2.jpg
DSC_0015.jpg


Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dk. Hamisi Kigwangalla akitoa maagizo kwa maafisa hao. ambao wanatoka katika Wilaya hiyo ya Babati.

DSC_0010.jpg


Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dk. Hamisi Kigwangalla akitoa hutuba hiyo
DSC_0038.jpg
DSC_0043-1.jpg


Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dk. Hamisi Kigwangalla akimkabidhi mmoja wa waancho kadi maalum ya CHF iliyoboreshwa ambayo alijiunga papo hapo wakati wa tukio hilo la uzinduzi.

DSC_0049.jpg


Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dk. Hamisi Kigwangalla akikagua pikipiki ambazo zilitolewa kwa watendaji watakaosimamia mpango huo wa CHF iliyoboreshwa

DSC_0050.jpg


Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dk. Hamisi Kigwangalla aki-test’ moja ya Pikipiki ambazo alizitoa kwa watendaji watakaokuwa wakisimamia mradi huo. pikipiki hizo zimetolewa na Shirika hilo la Kimataifa la PHARM ACCESS

DSC_0059.jpg


Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dk. Hamisi Kigwangalla akimkabidhi mmoja wa watendaji watakaokuwa wakiendesha huduma hizo kwa kutumia pikipiki

DSC_0065.jpg
DSC_0067.jpg


Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dk. Hamisi Kigwangalla akikabidhi Ipad maalum kwa ajili ya kutumika kwenye tukio hilo la CHF iliyoboreshwa

DSC_0074.jpg


DSC_0079.jpg


Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dk. Hamisi Kigwangalla alipata wasaha pia wa kujumuika katika huduma ya matibabu iliyokuwa ikitolewa bure katika tukio hilo la uzinduzi wa huduma za CHF iliyoboreshwa

DSC_0093.jpg
DSCRQ_0043.jpg

Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dk. Hamisi Kigwangalla pamoja na wageni wengine akiwemo Mkuu wa Mkoa wa Manyara wakiwasilia kwenye uwanja huo.
 
Back
Top Bottom