Dk 45 ITV » Agrey Mwanry (Waziri ~ TAMISEMI) ageuka mbogo kwa wanaohujumu mali za umma

sir.JAPHET

JF-Expert Member
May 18, 2012
699
133
naibu Waziri agrey mwanry wa tamisemi ageuka mbogo na kuapa kuwanyoosha wanaohujumu mali na rasilimali za taifa.. Amekiri kujipanga na kuwashughulikia watumishi wote wanaoleta mizahaa katika nafasi mbalimbali serikalini.. Amejipanga kufanya maboresho ngazi zote kwenye halimashaur na taasis na kuchukua hatua ipasavyo kuhakikisha haki inapatikana na kuwatimua wote mafisadi na..ameomba ushirikiano kwa wananchi
 
Niliwasikia watu wa Halmashauri wakiongea wanamwita Mzee wa Vitasa kwani akienda kwenye miradi ya ujenzi anakimbilia kuangalia aina ya vitasa vilivyotumika.
 
"Niangalie macho yangu na midomo yangu.......... TUKIKUKAMATA, sukuma peleka polisi, sukuma peleka mahakamani hakuna cha mtoto wa Mungu..... asije mtu akasema tafadhali, tutakwenda mulika mpaka utumbo mdogo!"

Haya ni maneno yake Naibu Waziri – TAMISEMI, Mh. Aggrey Mwanri katika Dakika 45 ITV.

Mimi nampenda huyu Kiongozi na kweli toka moyoni ningependa kufanya naye kazi maana ubadhilifu si kitu cha kuchekea chekea! I salute you:clap2::clap2::clap2:! Tumuunge mkono kwa:

1. Kuwaumbuwa wezi huko katika Halmashauri na ofisi za umma
2. Tusimbeze na kumkatisha tamaa eti nguvu za soda na tumlinde na Mungu wetu amjalie afya njema ili mapambano aliyoyaanzisha yaendeleze kurasa za Mh. Sokoine (RIP).
 
Anajipanga kwani alikuwa wapi miaka yote? Huyu Mwanri kila leo yuko kwenye TV akionesha ufundi wake wa kufoka lakini madudu kwenye Halmashauri yako pale pale! So, why should we believe him this time?
 
Anatoka sehemu moja na mbowe machame!huyu lazima ana ukabila maneno ya viongozi wa ccm hayo!hawaangali uchapaji kazi wa mtu
 
huo unaitwa mkwara wa mbuzi tu huo, halafu huyu mzee hua akiongea utadhani akimkamata mtu atammeza kumbe wala hana lolote wala chochote, kwani ndio leo kapewa wizara? si alikuepo siku mingi? au ndio ile katuni ya kipanya ya leo kamchora yeye kuwa anakumbuka shuka kukiwa kunapambazuka na shuka lenyewe bado ni fupi??
 
Hakuna msafi ndani ya ccm! Kwanza alibebwa kwa sababu ndo mchaga pekee ktk baraza la mawaziri wa Jk, alibebwa kwani yeye na George mkuchika ni wazembe! Aombe Mungu tu yeye ni mchaga!
 
Alianza Kagasheki akageuka mbogo,
Akaja Kigoda akageuka mbogo,
Akaja Mwakyembe akageuka mbogo,
Na sasa Mwanri naye kageuka mbogo.

Usanii kweli hatari...naona kugeuka mbogo kumekuwa fasheni ya magamba wakati utekelezaji ni ziro. Namkumbuka kwa mbali Tibaijuka, sijui kapotelea wapi...kweli moto wa kifuu huzimika haraka. Na hapo hatujamwongelea Nape na siku zake tisini, hivi jamani huko CCM kuna mdudu gani? Hakika nachoka.
 
Usanii tuu mbona ktk mifano yake ya halmashauri ambazo mkurugenzi na watendaji waliohujumu mali ya umma hataji ILEJE ambako mil 86.2 imethibitika zilishaingia mikononi mwa watendaji hao? USANII MTUPU TENA HATA KTK BUNGE LA MWAKA JANA HUYU JAMAA ALIONGEA KWA UKALI HIVI HIVI UTADHANI ATACHUKUA HATUA. Kibaya zaidi kwa sasa yupo chini ya HAWA GHASIA. Unategemea nini kwa hawaa ghasiaaa!!!!!???????
 
naibu Waziri agrey mwanry wa tamisemi ageuka mbogo na kuapa kuwanyoosha wanaohujumu mali na rasilimali za taifa.. Amekiri kujipanga na kuwashughulikia watumishi wote wanaoleta mizahaa katika nafasi mbalimbali serikalini.. Amejipanga kufanya maboresho ngazi zote kwenye halimashaur na taasis na kuchukua hatua ipasavyo kuhakikisha haki inapatikana na kuwatimua wote mafisadi na..ameomba ushirikiano kwa wananchi

Huu si wakai wa maneno ni wakati wa vitendo, kwenda kwenye majukwaa na kuongea hadi unatiokwa na povu mdomoni haisaidiii, tunataka tuone matendo. Hao ambao wameishakula akiwemo yeye wanafanywa nini siyo kuita waandishi wa habari na kuwahadaa watazania kwa kauli tamu halafu ukitoka hapo matendo yako hayaendani na ulichokisema jukwaani.
 
"Niangalie macho yangu na midomo yangu.......... TUKIKUKAMATA, sukuma peleka polisi, sukuma peleka mahakamani hakuna cha mtoto wa Mungu..... asije mtu akasema tafadhali, tutakwenda mulika mpaka utumbo mdogo!"

Haya ni maneno yake Naibu Waziri – TAMISEMI, Mh. Aggrey Mwanri katika Dakika 45 ITV.

Mimi nampenda huyu Kiongozi na kweli toka moyoni ningependa kufanya naye kazi maana ubadhilifu si kitu cha kuchekea chekea! I salute you:clap2::clap2::clap2:! Tumuunge mkono kwa:

1. Kuwaumbuwa wezi huko katika Halmashauri na ofisi za umma
2. Tusimbeze na kumkatisha tamaa eti nguvu za soda na tumlinde na Mungu wetu amjalie afya njema ili mapambano aliyoyaanzisha yaendeleze kurasa za Mh. Sokoine (RIP).

Tumechoka kusikia tunajipanga. Angetuambia ile miradi alokuwa akitoa povu kwa TV si imebakia vile vile! Ni wangapi alofikisha mahakamani?

By the way, yeye ni naibu waziri tu, Waziri wake yuko naye au anawaambia watendaji kuwa huo ni upepo tu utapita tuendelee kutafuna?
 
huo unaitwa mkwara wa mbuzi tu huo, halafu huyu mzee hua akiongea utadhani akimkamata mtu atammeza kumbe wala hana lolote wala chochote, kwani ndio leo kapewa wizara? si alikuepo siku mingi? au ndio ile katuni ya kipanya ya leo kamchora yeye kuwa anakumbuka shuka kukiwa kunapambazuka na shuka lenyewe bado ni fupi??

...swadaktaaa
 
maneno tu hayo,tushawazoea,hakuna jipya!malizeni muda wenu muondoke tuanze upya!
 
jamani hata leo, mhe.mwanri ameonekana bungeni akijibu maswali kwa wabunge mbali mbali kuhusiana na utata .. Unajitokeza maeneo mbalimbali.. Amekuwa mkali haswaa na amesema ameanza kwa kuwatimua mafisadi na watendaji wabovu.. Na ameonya kuwa KAMWE KASI YAKE SI NGUVU YA SODA..
 
Back
Top Bottom