Damaso
JF-Expert Member
- Jul 18, 2018
- 6,132
- 10,514
Ni wazi kuwa katika miaka ya hivi karibu mivutano baina ya Israel na Palestina imekuwa mikubwa huku watu wengi wakipoteza maisha katika mashambulio kadha wa kadha haswa ukanda wa Gaza.
Dj Khaled akiwa kama anafahamika kwa majina ya Khaled Mohammed Khaled ni mtoto wa wazazi waliokimbia Palestina na Dj Khaled kuzaliwa New Orleans, Louisiana mwaka 1975, kifupi asili ya huyu mwamba ni Mpalestina.
Katika hiki ambacho wasanii wanaonesha kuinga mkono Palestina kwa kile ambacho kinaendelea ukanda wa Gaza ni kama vile, Dj Khaled amekuwa mfano wa Yuda Eskarioti kwani hajazungumza chochote na amekuwa kimya. Wengine wakidai kuwa akitetea ndugu zake Wapalestina basi muziki wake utapata changamoto.
Watu wameamua kumtolea uvivu wakati alipopanda kwenye show moja Marekani. Watu wamemuonesha upande wa pili wa shilingi. Ni kipande cha video ambacho kiukweli kinaumiza sana.