Mathanzua
JF-Expert Member
- Jan 4, 2017
- 17,038
- 22,714
Si muda mrefu sana uliopita Waziri Mkuu alitoa agizo la kusitisha uuzaji na matumizi ya pombe kali aina ya viroba ifikapo tarehe 01.03.2017.Hata hivyo Diwani mmoja katika kijiji cha Wami Dakawa hapa Mkoani Morogoro,jina tunalihifadhi, ambaye ana club moja iitwayo Dark Pub iliyokubuhu kwa matendo maovu, alishangaza watu pale alipowatukana askari Polisi wa Kituo cha Wami Dakawa kwa matusi ya nguoni ambao walikuwa kwenye harakati za kutekeleza agizo la Waziri Mkuu pale alipokutwa na lundo la viroba kwenye club yake.Wengi walijiuliza, iweje kiongozi ambaye alipaswa kuwa mstari wa mbele kutekeleza agizo la Waziri Mkuu awe kinara wa kulivunja tena kwa kutoa matusi ya nguoni?Iweje pia kiongozi huyo asikamatwe kana kwamba yeye yuko juu ya sheria?Kuna nini kinaendelea kati ya Diwani huyu na askari wa Kituo cha Dakawa?Nimekusikia IGP Mangu ukitamka ulipokuwa Mwanza kwamba wote watakaokiuka agizo la Waziri Mkuu la kusitisha uuzaji na matumizi ya viroba watashuhulikiwa.Tunasubiri kuona Diwani huyu akishuhulikiwa kwa kuwa hakuna aliye juu ya sheria.