Diwani ccm amtishia maisha mbunge cdm iringa. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Diwani ccm amtishia maisha mbunge cdm iringa.

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by WISTON MWINUKA, May 22, 2012.

 1. WISTON MWINUKA

  WISTON MWINUKA Member

  #1
  May 22, 2012
  Joined: Apr 29, 2012
  Messages: 82
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Katika hali isiyo ya kawaida diwani wa CCM kata ya Nduli manispaa ya Iringa Mh.Chonanga amemtishia Mh.Msigwa mbunge wa CDM maisha yake,na taarifa kutoka kinywani kwa Mh.msigwa zina kiri kuhusiana na suala hili kwani Msigwa ameomba apewe ulinzi na vyombo vinavyohusika ili kuyanusuru maisha yake.Hali hii inakuja zikiwa ni siku chache tu zimepita tangu Diwani huyu wa CCM akisaidiwa na watoto wake kufanya fujo na kuwa katakata mapanga wafuasi wa CDM ambao bado wapo hospitalini na hali zao ni mbaya.Katika hali ya kushangaza baadhi ya wakazi wa Manispaa ya Iringa wamewataja vijana wa Mh.Chonanga kuwa wanahusika na mauaji yanayotokea mara kwa mara katika eneo la kona za mgongo manispaa ya Iringa.Hivi ni kitu gani anajivunia huyu diwani hadi kuwatishia watu maisha yao?Jana kafanya fujo eneo la manispaa Iringa akitaka kumpiga mmoja wa viongozi wa CDM. Eee mwenyezi mungu tunaomba utupe roho ya kuwapenda na kuwajali wenzetu,AMENI.
   
Loading...