Mwanahabari Huru
JF-Expert Member
- Mar 9, 2015
- 14,243
- 34,903
DIWANI wa Kata ya Kikuyu Kasikazini, Islael Mwansasu (CCM) anadaiwa zaidi ya Sh. 34 milioni kama kodi ya pango la nyumba inayomilikiwa na Kampuni Hodhi Rasilimali za Reli (RAHCO) nchini.
Mbali na kudaiwa fedha hizo RAHACOimesema, mpangaji huyo amekiuka makubaliano na kufanya upanuzi wa jingo hilo na kusababisha kuvamia hifadhi za reli kinyume na sheria ya hifadhi ya maeneo ya reli ya mwaka 2002.
Hayo yalielezwa na Catherine Moshi, Ofisa Habari wa RAHCO alipozungumza na waadishi wa habari wakati wa ukaguzi kwa baadhi ya watu ambao wamevamia hifadhi ya shirika hilo.
Amesema, mpangaji huyo amekiuka mkataba wa upangaji kwa kuwa ameshindwa kulipa pango kwa zaidi ya miaka miwili sasa na kusababisha deni la zaidi ya Sh. 34 milioni.
“Tunamshangaa mpangaji wetu kwa kufanya upanuzi wa jingo bila hata kutuambia kama mkataba unavyoeleza, lakini kibaya zaidi amejenga vibanda zaidi ya 15 na anavipangisha na anatoza kodi jambo ambalo ni kinyume na makubaliano.
“Mkataba wetu unasema wazi kuwa, mpangaji anaweza kufanya maboresho na kabla ya kufanya maboesho ni lazima awasiliane na kampuni husika ambayo imempangisha.
“Lakini yeye hakufanya hivyo na matokeo yake alianza kuwasiliana na Mamlaka ya Ustawishaji Makao Makuu (CDA),” amesema.