Diwani afumaniwa ugoni iringa achezea kipigo...

Diwani afumaniwa ugoni iringa achezea kipigo...

Status
Not open for further replies.

nngu007

JF-Expert Member
Joined
Aug 2, 2010
Posts
15,860
Reaction score
5,803
.



Katika hali isiyo kuwa ya kawaida diwani mmoja wa chama cha siasa jina laka na chama chake limewekwa kapuni kwa sasa amefumaniwa akivunja amri ya sita na mke wa mtu usiku wa leo na kuchezea kichapo .


Diwani huyo mpenda ngono anadaiwa kufumaniwa akiwa katika nyumba ya mpiga kura wake huyo katika kata moja ya wilaya ya Iringa Vijijini na ni diwani anayetokea katika wilaya ya Iringa mkoa wa Iringa na ni diwani mtanashati kweli kweli.


Mashuhuda wa tukio hilo wameudokeza mtandao huu wa Francis Godwin Mzee Wa Matukio Daima kuwa kutokana na fumanizi hilo la mwaka wapiga kura wake wanaoishi jirani na nyumba hiyo ambayo mheshimiwa alifunaniwa waliizunguka nyumba hiyo na kuanza kumshikisha adabu mheshimiwa huyo.


Baada ya mheshimiwa huyo kuchezea kipigo kutoka kwa njema lenye mke huyo pamoja na wananchi alilazimika kutoka mbio na kukimbilia porini kabla ya kwenda kupatiwa matibabu katika moja kati ya zahanati mbili zilizopo katika eneo hilo ikiwemo ya Misheni na ile ya Kijiji .


Iwapo wataka kujua zaidi juu ya tukio hili endelea kufuatilia mtandao huu unapofanya jitihada za kumtafuta diwani huyo


Pichani ni moja kati ya picha ya fumanizi ambayo inafanana na fumanizi hili la diwani japo hainamahusiano na tukio hili.

KWA HISANI YA HABARI ZA JAMII BLOG

 
Kwanini CHAMA kinafichwa??? Hakuna DEMOKRASIA???
 
acha udaku angekuwa diwani wa CCM angewekwa wazi lakini kwa sababu wa chama chako unasita kuweka wazi
 
Huna haja ya kukitaja chama, chama cha wagoni kinaeleweka. Wanamuenzi marehemu Ditto a.k.a Mzee wa kula chapati.
 
Itakuwa ya kutunga!na kama sivyo wekeni mambo hadharani!!!Mbona ya Mwingulu{Lameck} hamkuficha!!!???
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom