Diwani afumaniwa ugoni achezea kipigo

englibertm

JF-Expert Member
Joined
May 1, 2009
Posts
9,252
Reaction score
6,211
Katika hali isiyo kuwa ya kawaida diwani mmoja wa chama cha siasa jina laka na chama chake limewekwa kapuni kwa sasa amefumaniwa akivunja amri ya sita na mke wa mtu usiku wa leo na kuchezea kichapo .

Diwani huyo mpenda ngono anadaiwa kufumaniwa akiwa katika nyumba ya mpiga kura wake huyo katika kata kata moja ya wilaya ya Iringa Vijijini na ni diwani anayetokea katika wilaya ya Iringa mkoa wa Iringa na ni diwani mtanashati kweli kweli.

Mashuhuda wa tukio hilo wameudokeza mtandao huu wa kuwa kutokana na fumanizi hilo la mwaka wapiga kura wake wanaoishi jirani na nyumba hiyo ambayo mheshimiwa alifunaniwa waliizunguka nyumba hiyo na kuanza kumshikisha adabu mheshimiwa huyo.

Baada ya mheshimiwa huyo kuchezea kipigo kutoka kwa njema lenye mke huyo pamoja na wananchi alilazimika kutoka mbio na kukimbilia porini kabla ya kwenda kupatiwa matibabu katika moja kati ya zahanati mbili zilizopo katika eneo hilo ikiwemo ya Misheni na ile ya Kijiji .

Iwapo wataka kujua zaidi juu ya tukio hili endelea kufuatilia mtandao huu unapofanya jitihada za kumtafuta diwani huyo

Pichani ni moja kati ya picha ya fumanizi ambayo inafanana na fumanizi hili la diwani japo hainamahusiano na tukio hili
 
Hii picha japo haihusiani na tukio lazima itakuwa ya wasaani wa Tanzania.....angalia wahusika hasa Dada walivyorelax.....yaani hawajavaa kabisa uhusika wa tukio....
 
taja zahanat alipatiwa matibabu.taja chama, taja kata,taja tina,weka picha ya tukio sio hii ya bongo muv ukishidwa mpelekee shigongo humu hatutaki majungu kama vip chapa lapa.
 
Huyu mwanaume vipi,mbona mwanamke alikuwa ameshavua nguo alafu yeye bado amevaa nguo,au ni mngese nini?
 
atakuwa wa ccm huyo diwani
 
...Hadithi za 'jina limewekwa kapuni' daima dumu ni hadithi za kutunga tu! Peleka magazeti ya Udaku...kama sio umeitoa huko huko!!!:nimekataa
 

Hapo ndio umeandika nini ?
...... siku fulani, diwani fulani, wa kata fulani, amefuniwa sehemu fulani na mke wa mtu fulani, diwani huyo ni wa chama fulani .....
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…