Hakika huu ni muujiza mkuu wa Mungu
Kwa huyu Tundu Lissu kuvivuka hivi vikwazo vyote vigumu sans, kimoja baada ya kingine, hakika huu ni muujiza mkuu wa Mungu.
Huu mpambano wa Lissu VS Magufuli katika uchaguzi mkuu ujao mwaka huu, naufananisha na ule mpambano wa kwenye Biblia wa Daudi VS Goliath.
Hakika kama vile Daudi alivyomshinda yule mbabe wa kivita, kwa manati peke yake, yule kiumbe wa kutisha katika medani za kivita, Goliath, kwa uwezo wa Mungu, vivyo hivyo naamini huyu Tundu Lissu atamshinda huyu mbabe ambaye ambaye anatumia nguvu zote za vyombo vya dola hapa nchini, John Magufuli, kwa uwezo ule ule uliompa ushindi Daudi kwa nguvu za Mungu!
Tutarajie kuuona muujiza mkuu wa Mungu katika uchaguzi mkuu wa mwaka huu!