Distance Love

Distance Love

yuleeee

Member
Joined
May 25, 2013
Posts
57
Reaction score
11
Wanajamvi msaada
Nina mpenz wangu tumedumu naye muda mrefu (miala minne) mpaka baadhi ya ndugu zake wananifahamu. Tatizo la mchumba wangu huyu anasema hawez kuvumilia mapenz ya kukaa mbali kwani fimbo ya mbali haiui nyoka. Nimechanganyikiwa mno kwani tunakaa mikoa ya mbalimbali mpaka nimfikie natakiwa kutumia nauli ya elfu 70. Please nifanyeje kuokoa penz langu kwani nina mpenda mno sipo tayar kumpoteza?
 
Fanya kila liwezekanalo uwe naye karibu.
 
Hapa panahitajika maamuzi magumu mmoja wenu ahamie kwa mwenzie ili muweze kuendelea na penzi lenu. Mnabidi pia muangalie vigezo mbali mbali kama upatikanaji wa ajira, gharama za maisha, vipato vyenu n.k. ili kufikia muafaka wa nani ahame huko aliko.
 
Wanajamvi msaada
Nina mpenz wangu tumedumu naye muda mrefu (miala minne) mpaka baadhi ya ndugu zake wananifahamu. Tatizo la mchumba wangu huyu anasema hawez kuvumilia mapenz ya kukaa mbali kwani fimbo ya mbali haiui nyoka. Nimechanganyikiwa mno kwani tunakaa mikoa ya mbalimbali mpaka nimfikie natakiwa kutumia nauli ya elfu 70. Please nifanyeje kuokoa penz langu kwani nina mpenda mno sipo tayar kumpoteza?

Kama ni kweli kakwambia hv achana nae kabisa, nakuhakikishia kuna fimbo ingine iko karibu hapo inayoua huyo nyoka. Achana nae.
 
Miaka minne mingi bans tafuta hila upate ajira aliko au fanya yeye aje kwako. Aisee anamoyo huyo dada kusubiri muda wote....mie ningeshakutosa zamani
 
Mimi nimeajiriwa na serikali naye huko alipo yupo kwenye sector inayomlipa vizur..... ndio maana imekuwa shughuli kufuatana. Moto unawaka moyoni sielewi cha kufanya
 
Hilo penzi limeshaanza kua na ufa fwata ushauri ulioshauriwa hapo juu kwamba ufanye juhudi uwe nae kama kweli unampenda na unataka uwe nae kwa sababu kama ameshaanza kusema hivyo kuna kitu cha hatari hiyo ni indicator rafiki, ni ishara mbaya sana kwenye mahusiano ya umbali., sikukatishi tamaa ila hapo kuna mtu ameshaomba nafasi na kama umekaa miaka minne mii nakupa miezi miwili, la sivyo una msaidizi huko, na hapo penzi limeshaanza kupungua au ameshakuchoka..
 
Mimi nimeajiriwa na serikali naye huko alipo yupo kwenye sector inayomlipa vizur..... ndio maana imekuwa shughuli kufuatana. Moto unawaka moyoni sielewi cha kufanya

Oaneni ili iwe rahisi kwa mmojawapo kuhama na kumfuata mwenzake.
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Wanajamvi msaada
Nina mpenz wangu tumedumu naye muda mrefu (miala minne) mpaka baadhi ya ndugu zake wananifahamu. Tatizo la mchumba wangu huyu anasema hawez kuvumilia mapenz ya kukaa mbali kwani fimbo ya mbali haiui nyoka. Nimechanganyikiwa mno kwani tunakaa mikoa ya mbalimbali mpaka nimfikie natakiwa kutumia nauli ya elfu 70. Please nifanyeje kuokoa penz langu kwani nina mpenda mno sipo tayar kumpoteza?

Aahh Mkuu!!!yani karibu ivyo?sasa kama nauli elfu sabini si inabidi uwe unaenda kushinda nae kila wkendi huku unatafuta kazi karibu nae, alafu si kuna ile kampuni ya fastjet ina gharama nafuu ama,huko haina route????
 
Back
Top Bottom