Dirty Secrets

futikamba

JF-Expert Member
Jan 18, 2010
243
13
Habari ya maandalizi ya x-mas wakubwa?
Ikiwa tunaelekea kufunga mwaka, wengi tumepitia mengi ktk mahusiano yaliyotufunza namna ya kustahimili na kumudu hisia mbalix2 kwenye mahusiano. Natumai mwakani kila mmoja wetu amejiwekea malengo na nawaombea wote malengo yenu yatimie sawax2 na mapenzi yenu. Swali langu ni hivii ina maana gani kwa mkaka anayesaka mpenzi kusema 'dirty secrets' zake kwa yule anayemtokea? Yaani zinazohusu maisha yake ya kimapenzi? Naomba nisiende kwenye details, lakini namaanisha zile siri ambazo, pengine ni rafiki zake wa kiume tu nd'o wanajua na/au walitakiwa kujua. Yamenitokea, embu nisaidieni..
Akhsante!

MERRY X-MAS & HAPPY NEW YEAR!!
 
siri zote huwa zinaumiza
watu huzungumza ili kuutua mzigo
na sometimes ni kuchanganyikiwa na kutojua cha kufanya baada ya kuijua siri fulani....
 
Huyo anakuwa ni domo zege, kwani unapompiga sound demu/mwanamke lazima u-expose profile yako ya zamani?
 
siri gani hizo? ila unajua mie naona bora useme ukweli tuu maana zinaweza kujitokeza usipotegemea.
 
siri zote huwa zinaumiza
watu huzungumza ili kuutua mzigo
na sometimes ni kuchanganyikiwa na kutojua cha kufanya baada ya kuijua siri fulani....

Je kama hata anayeelezwa hizo siri, hajui kitu au hajawahi kushtukia chochote? Yaani jamaa anaanza tu kujielezea, hajaulizwa wala nini, imekaaje hiyo?
 
Sijui ndio udomo zege...ila kuna secrets zingine yaani hata kama unatongoza wala hazifai kusemwa kuna mmoja alinitolea yake kuwa alikuwa anatembea na binamu yake kabisaa..wala sio binamu wa kuunganisha,na anasema show za dada yake huyo ni balaa..ana nasty moves hajaziona kokote..Looh!!
 
siri gani hizo? ila unajua mie naona bora useme ukweli tuu maana zinaweza kujitokeza usipotegemea.

Zile siri nzito.. Sorry, siwezi kufafanua zaidi. But ni zile ambazo ukisikia unamwangalia m2 mara 2-2 na kujiuliza 'eeeh na huyu anaweza kweli kufanya hivi'?
 
Je kama hata anayeelezwa hizo siri, hajui kitu au hajawahi kushtukia chochote? Yaani jamaa anaanza tu kujielezea, hajaulizwa wala nini, imekaaje hiyo?

Hiyo inaboa kwakweli..maana ndo hayo unajikuta unaongea vitu ambavyo ingekuwa best ungebaki navyo..Sio kabisa kama hujaulizwa!
 
kama uliwahi kula s.h.o.g.a wala usiseme
kawaambie wanamme wenzio tu
mwanamke unayemfukuzia atakuogopa kama ukoma
 
Ni bora kuwa muwazi kwa mwenzio mapema kabla hamjafika mbali isije kuwa shida mbele, make waweza ficha alafu mwisho wa siku anakuja kusikia kwingine unakuwa ugomvi
 
Kila Binadamu hakosi SIRI, kuna siri ya Familia pekee, Siri ya Marafiki pekee, kuna Siri ya wewe na Mkeo, na SIRI yako mwenyewe!!. Ijapokuwa watu husema Siri isizidi watu wawili, hata zaidi waeza weka siri. Jambo kubwa kujiuliza, ni mwenye kupewa siri ataweza kuweka Siri??, kama si mtu wa kuweka siri ama mtu domo kaya kuna hatari ya kumwaga siri.

Wewe kama mwanaume, uta-amua siri utakazo mweleza mchumba/mkeo ikitegemea unavyo muona mwenzio na sio kwa wakati mmoja, na sio kila siri, umpe!!!. Kuna siri ambazo mtu huenda nazo kaburini!!
 
mi naona si vizuri kuropokwa tu, pale kaskia vitu juu yako akikuuliza ni bora kuwa muwazi lkn kuanza tu unaanza kumwaga mambo hadharani ni noma
 
Labda yeye anaona sifa, au anaona akisema hizo atajenga heshima Zaid
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom