Diploma third round

Diploma third round

MEKADDISHKEM

Senior Member
Joined
Sep 15, 2016
Posts
153
Reaction score
150
TAARIFA KWA UMMA KUHUSU UTEUZI WA AWAMU YA TATU, UHAMISHO NA KUONGEZWA KWA MUDA WA KUFANYA MAOMBI KATIKA KOZI ZA ASTASHAHADA (CHETI) NA STASHAHADA (DIPLOMA) KWA MWAKA WA MASOMO 2016/2017

Date Posted: 2nd October 2016 22:35:00
Posted By: NACTE
BARAZA LA TAIFA LA ELIMU YA UFUNDI (NACTE)

Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE) linapenda kuwaarifu wote walioomba kudahiliwa katika kozi za Astashahada (Cheti) na Stashahada (Diploma) na Umma kwa ujumla kuwa dirisha la maombi lilifungwa mnamo tarehe 15 Septemba 2016 ili kuruhusu uteuzi wa awamu ya pili kwa waombaji wa kozi hizo.

Uteuzi wa awamu ya tatu kwa waombaji wa Astashahada na Stashahada unatarajiwa kutangazwa mnamo tarehe 5 Oktoba 2016, hivyo basi waombaji wanaombwa kuwa na subira ili kutoa muda kwa Baraza kukamilisha taratibu za uteuzi huo.

Maombi mapya ya Udahili
Baraza linapenda kutoa taarifa kuwa Mfumo wa Pamoja wa Udahili (CAS) utafunguliwa tena tarehe 5 Oktoba 2016 hadi tarehe 15 Oktoba 2016 ili kujaza nafasi za udahili zilizobaki wazi baada ya uchaguzi wa awamu ya pili. Hatua hii itawezesha kuruhusu machaguo mapya kwa wale ambao hawakuchaguliwa katika kozi walizoomba pamoja na kuruhusu waombaji wapya ambao kwa njia moja au nyingine hawakuweza kuomba hapo awali.

Maombi ya Uhamisho
Mwombaji aliyechaguliwa ataweza kuomba uhamisho kutoka chuo ama kozi moja kwenda nyingine kupitia kwenye ukurasa wake binafsi (profile) tu. Uhamisho huu utategemea nafasi zilizopo , ushindani na
alama za chini za kujiunga na kozi (cut-off). Orodha ya Vyuo na Programu zenye nafasi zitatolewa hivi punde.

Hatua za kuomba uhamisho:
1. Ingia kwenye ukurasa wako binafsi (profile) kwa kutumia jina la mtumiaji (Username) na neno la siri (Password) ulivyopewa wakati wa usajili.
2. Bofya kitufye kilichoandikwa “Transfer Request/Kuomba uhamisho”, na punde ukurasa utafunguka
3. Utafunguka ukurasa unaokuonesha chuo na kozi uliyochaguliwa awali
4. Chagua kada unayohitaji kuhamia
5. Chagua chuo unachohitaji kuhamia
6. Chagua kozi unayohitaji kuhamia
7. Mfumo utatathmini kama una sifa za kujiunga na kozi uliyochagua. Iwapo una sifa za kujiunga na kozi hiyo mfumo utakuomba ulipie Sh.
30,000/- kama ada ya maombi ya uhamisho.
Kiasi hiki hakitarudishwa (non-refundable)
8. Bofya kitufye kilichoandikwa “Confirm Transfer Request/Kamilisha maombi”.
9. Utapewa muhtasari wa maombi yako ya uhamisho pamoja na kutumiwa ujumbe mfupi wa maandishi kwenye namba ya simu ya mkononi uliyoweka wakati wa usajili na barua pepe kukujulisha kwamba umekamilisha maombi.

Jinsi ya kulipia (Malipo yatafanywa kwa M- pesa tu)
1. Piga *150*00#
2. Chagua 4. LIPA kwa M-Pesa
3. Chagua 4. Weka namba ya kampuni
4. Tafadhali weka namba ya kampuni (No. 607070)
5. Weka namba ya kumbukumbu ya malipo (No. 1234)
6. Weka kiasi (e.g.30,000/=)
7. Weka namba ya siri
8. Bonyeza 1 kuthibitisha.

Angalizo (Disclaimer)
1. Kuhama chuo na kozi si lazima.
2. Uhamisho utafanyika kwa kozi zile tu zenye nafasi na kwa vyuo ambavyo bado havijafunguliwa na kuanza masomo.
3. Uhamisho ni kwa wale waombaji waliokwisha kuchaguliwa kupitia mfumo wa pamoja wa udahili tu.
4. Maombi ya uhamisho yanaweza kufanyika MARA MOJA na kwa kozi moja
5. Iwapo umefanikiwa kupata uhamisho, majibu yataonekana kwenye ukurasa wako binafsi (Profile). Majibu haya pia yatatumwa kwenye namba yako ya simu kwa njia ya ujumbe mfupi wa maandishi na kupitia barua pepe baada ya tarehe ya mwisho ya maombi (15 Oktoba 2016).
6. Uhamisho utategemea ufaulu wa waombaji na nafasi zilizopo. Hii
inamaanisha kwamba wenye ufaulu wa juu ndio wenye uwezo

COPYRIGHT © 2007 - 2015 THE NATIONAL COUNCIL FOR TECHNICAL EDUCATION.
 
TAARIFA KWA UMMA KUHUSU UTEUZI WA AWAMU YA TATU, UHAMISHO NA KUONGEZWA KWA MUDA WA KUFANYA MAOMBI KATIKA KOZI ZA ASTASHAHADA (CHETI) NA STASHAHADA (DIPLOMA) KWA MWAKA WA MASOMO 2016/2017
Date Posted: 2nd October 2016 22:35:00
Posted By: NACTE
BARAZA LA TAIFA LA ELIMU YA UFUNDI
(NACTE)
TAARIFA KWA UMMA KUHUSU UTEUZI WA AWAMU YA TATU, UHAMISHO NA KUONGEZWA KWA MUDA WA KUFANYA MAOMBI KATIKA KOZI ZA ASTASHAHADA (CHETI) NA STASHAHADA (DIPLOMA) KWA MWAKA WA MASOMO 2016/2017
Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE) linapenda kuwaarifu wote walioomba kudahiliwa katika kozi za Astashahada (Cheti) na Stashahada (Diploma) na Umma kwa ujumla kuwa dirisha la maombi lilifungwa mnamo tarehe
15 Septemba 2016 ili kuruhusu uteuzi wa awamu ya pili kwa waombaji wa kozi hizo.
Uteuzi wa awamu ya tatu kwa waombaji wa Astashahada na Stashahada unatarajiwa kutangazwa mnamo tarehe 5 Oktoba 2016, hivyo basi waombaji wanaombwa kuwa na subira ili kutoa muda kwa Baraza kukamilisha taratibu za uteuzi huo.
Maombi mapya ya Udahili
Baraza linapenda kutoa taarifa kuwa Mfumo wa Pamoja wa Udahili (CAS) utafunguliwa tena tarehe
5 Oktoba 2016 hadi tarehe 15 Oktoba 2016 ili kujaza nafasi za udahili zilizobaki wazi baada ya uchaguzi wa awamu ya pili. Hatua hii itawezesha kuruhusu machaguo mapya kwa wale ambao hawakuchaguliwa katika kozi walizoomba pamoja na kuruhusu waombaji wapya ambao kwa njia moja au nyingine hawakuweza kuomba hapo awali.
Maombi ya Uhamisho
Mwombaji aliyechaguliwa ataweza kuomba uhamisho kutoka chuo ama kozi moja kwenda nyingine kupitia kwenye ukurasa wake binafsi (profile) tu. Uhamisho huu utategemea nafasi zilizopo , ushindani na
alama za chini za kujiunga na kozi (cut-off). Orodha ya Vyuo na Programu zenye nafasi zitatolewa hivi punde.
Hatua za kuomba uhamisho:
1. Ingia kwenye ukurasa wako binafsi (profile) kwa kutumia jina la mtumiaji (Username) na neno la siri (Password) ulivyopewa wakati wa usajili.
2. Bofya kitufye kilichoandikwa “Transfer Request/Kuomba uhamisho”, na punde ukurasa utafunguka
3. Utafunguka ukurasa unaokuonesha chuo na kozi uliyochaguliwa awali
4. Chagua kada unayohitaji kuhamia
5. Chagua chuo unachohitaji kuhamia
6. Chagua kozi unayohitaji kuhamia
7. Mfumo utatathmini kama una sifa za kujiunga na kozi uliyochagua. Iwapo una sifa za kujiunga na kozi hiyo mfumo utakuomba ulipie Sh.
30,000/- kama ada ya maombi ya uhamisho.
Kiasi hiki hakitarudishwa (non-refundable)
8. Bofya kitufye kilichoandikwa “Confirm Transfer Request/Kamilisha maombi”.
9. Utapewa muhtasari wa maombi yako ya uhamisho pamoja na kutumiwa ujumbe mfupi wa maandishi kwenye namba ya simu ya mkononi uliyoweka wakati wa usajili na barua pepe kukujulisha kwamba umekamilisha maombi.
Jinsi ya kulipia (Malipo yatafanywa kwa M- pesa tu)
1. Piga *150*00#
2. Chagua 4. LIPA kwa M-Pesa
3. Chagua 4. Weka namba ya kampuni
4. Tafadhali weka namba ya kampuni (No. 607070)
5. Weka namba ya kumbukumbu ya malipo (No. 1234)
6. Weka kiasi (e.g.30,000/=)
7. Weka namba ya siri
8. Bonyeza 1 kuthibitisha.
Angalizo (Disclaimer)
1. Kuhama chuo na kozi si lazima.
2. Uhamisho utafanyika kwa kozi zile tu zenye nafasi na kwa vyuo ambavyo bado havijafunguliwa na kuanza masomo.
3. Uhamisho ni kwa wale waombaji waliokwisha kuchaguliwa kupitia mfumo wa pamoja wa udahili tu.
4. Maombi ya uhamisho yanaweza kufanyika
MARA MOJA na kwa
kozi moja
5. Iwapo umefanikiwa kupata uhamisho, majibu yataonekana kwenye ukurasa wako binafsi (Profile). Majibu haya pia yatatumwa kwenye namba yako ya simu kwa njia ya ujumbe mfupi wa maandishi na kupitia barua pepe baada ya tarehe ya mwisho ya maombi (15 Oktoba 2016).
6. Uhamisho utategemea
ufaulu wa waombaji na
nafasi zilizopo. Hii inamaanisha kwamba wenye ufaulu wa juu ndio wenye uwezo
COPYRIGHT 2007 - 2015 THE NATIONAL COUNCIL FOR TECHNICAL EDUCATION.
NACTE NI KITENGO CHA CCM HIYO TAREHE 05 HAMTATOA TUNAJUA TU HILO HAKUNA LOLOTE HAPO ACHENI UONGO
 
Na wa degree mtanfungua lini third round coz kuna wale waliokua na supplimentary ndo wanaziclear nao waweze kua na sifa je na hao pia TCU na NACTE wanawafikiria kweli?
 
So kama mty hana ufaulu wa juu hawezi kufanya transfer?sijaelewa hapo
unaweza kufanya lakini wenye uhakika zaidi ni wale wenye ufaulu wa juu sababu kutakuwa na competition kubwa sasa ikitokea wewe unaufaulu wa wastani System haitokuchagua kwasababu itapanga kuanzia ufaulu wa juu kabisa kwenda Chini
Kazi ni kwako lakini
 
Na wa degree mtanfungua lini third round coz kuna wale waliokua na supplimentary ndo wanaziclear nao waweze kua na sifa je na hao pia TCU na NACTE wanawafikiria kweli?
ONDOA hofu kiongozi
Tupo kwenye michakato ya mwisho
soon na nyie mtatangaziwa
 
Wanaposema transfer itafanyika kwa vyuo ambavyo havijafunguliwa sasa kuna chuo hakijafunguliwa kweli?
 
Wanaangalia ufaulu wa juu au point za koz unazotaka kama kuna MTU ana three lakini math B physics C chemi c halaf mingine D halaf mwingine ana math D phys D chemi D kiswahili A ana one Kali hapo inakuaje wadau????
 
NACTE NI KITENGO CHA CCM HIYO TAREHE 05 HAMTATOA TUNAJUA TU HILO HAKUNA LOLOTE HAPO ACHENI UONGO
TUPO KWENYE FINISHING KIONGOZI
KAZI HII NI KUBWA KULIKO UNAVYOIFIKILIA WEWE YATUHITAJI UMAKINI WA HALI YA JUU
KUHUSU DUKUDUKU LAKO ONDOA SHAKA
 
Wanaangalia ufaulu wa juu au point za koz unazotaka kama kuna MTU ana three lakini math B physics C chemi c halaf mingine D halaf mwingine ana math D phys D chemi D kiswahili A ana one Kali hapo inakuaje wadau????
Maombi ya Uhamisho
Mwombaji aliyechaguliwa ataweza kuomba uhamisho kutoka chuo ama kozi moja kwenda nyingine kupitia kwenye ukurasa wake binafsi (profile) tu. Uhamisho huu utategemea nafasi zilizopo , ushindani na
alama za chini za kujiunga na kozi (cut-off). Orodha ya Vyuo na Programu zenye nafasi zitatolewa hivi punde.
Tembelea Profile yako mara kwa mara
 
ONDOA hofu kiongozi
Tupo kwenye michakato ya mwisho
soon na nyie mtatangaziwa

Naomba kuuliza inamaana wale wa awamu ya 2 walishatoa ndio inafuatia awamu ya tatu au awamu ya pili watatolewa hiyo atrehe 5 na kukaribisha awamu ya tatu?
 
usichanganye mambo awamu ya tatu hapo Ni kwa ngazi ya cheti na stashahada
kwa degree Bado awamu ya pili haijatoka
 
OK, ila nilikua naongelea upande wa cheti, kuna kijana wangu alikua anangojea kubadilisha
ushauri wangu kwa Dogo afanye application za uhamisho soon system itakapo funguliwa labda nikuulize anataka kozi gani na ufaulu Wake upoje
 
Alichaguliwa National college of Tourism ila anataka Nursing.. ana DDD kwa phy,chem na Biology
 
sikukatishi tamaa lakini kozi za afya zina ushindani mkubwa watu Wengi wanataka hizo ushauri wa bure nafasi za uhamisho zikitoka kama anapenda afanye application lakini achague chuo kulingana na ufaulu Wake
yasije mkuta yaliyo wakuta wenzake mtu ana two kali kakosa chuo
NB: vingi kati ya vyenye nafasi ni Priavet so swala la Ada mjiandae
 
Back
Top Bottom