Diploma Holders Selection ni Tarehe 5 October

Diploma Holders Selection ni Tarehe 5 October

sime

Senior Member
Joined
Jul 14, 2016
Posts
146
Reaction score
86
Nacte.PNG
 
Hiyo ni kwa diploma na certificate mkuu, mbona naona kama tangazo linajieleza kabisa isee
 
Uwe makin kijana, tangazo lako haliwahusu Diploma holders.

Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE) linapenda kuwaarifu wote walioomba kudahiliwa katika kozi za Astashahada (Cheti) na Stashahada (Diploma) na Umma kwa ujumla kuwa dirisha la maombi lilifungwa mnamo tarehe 15 Septemba 2016 ili kuruhusu uteuzi wa awamu ya pili kwa waombaji wa kozi hizo.

Uteuzi wa awamu ya tatu kwa waombaji wa Astashahada na Stashahada unatarajiwa kutangazwa mnamo tarehe 5 Oktoba 2016, hivyo basi waombaji wanaombwa kuwa na subira ili kutoa muda kwa Baraza kukamilisha taratibu za uteuzi huo.

Maombi mapya ya Udahili
Baraza linapenda kutoa taarifa kuwa Mfumo wa Pamoja wa Udahili (CAS) utafunguliwa tena tarehe 5 Oktoba 2016 hadi tarehe 15 Oktoba 2016 ili kujaza nafasi za udahili zilizobaki wazi baada ya uchaguzi wa awamu ya pili. Hatua hii itawezesha kuruhusu machaguo mapya kwa wale ambao hawakuchaguliwa katika kozi walizoomba pamoja na kuruhusu waombaji wapya ambao kwa njia moja au nyingine hawakuweza kuomba hapo awali.
 
Hilo tangazo ni kwa cert na diploma waliokosa first na second round na c diploma holder
 
Back
Top Bottom